25 October 2011

Nchimbi kufungua tamasha Utamaduni

Na Mwali Ibrahim

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha  la
Utamaduni na Bongo Fleva litakalofanyika Novemba 11 hadi 12 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,  Arusha.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Tawala na Habari wa Endeleza Faundation, ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Ismail Mnikite, alisema lina lengo la kukutanisha vikundi vya utamaduni vya makabila ya Kanda ya Kaskazini katika kusherehekea utamaduni wao.

Ofisa huyo aliyataja makabila hayo ni Wamasai, Wapare, Wamang'ati na Wambulu kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, ambapo kila kabila litakuwa na ngoma zake.

Alisema kwa upande wa bongo fleva, wasanii Afande Sele, Mandojo na Domokaya, Godzilla, Mabaga Flesh, watapanda jukwaanbi kutumbuiza.

Ofisa huyo alisema Novemba 9, wataendesha semina ya mafunzo ya utamaduni kwa washiriki wa tamasha hilo itakayofundisha utamaduni wa makabila hayo.

Alisema tamasha hilo litasaidia kudumisha amani na kusameheana kwa makosa waliyotokea miaka ya nyuma, hasa ugomvi wa ardhi kwa upande wa wakulima na wafugaji.

No comments:

Post a Comment