21 October 2011

Mrwanda aishangaa TFF 'kumtolea macho'

Na Zahoro Mlanzi

SIKU chache baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuiachia Kamati ya Ufundi ya shirikisho hilo suala la
mshambuliaji wa timu ya taifa (Taifa Stars), Danny Mrwanda kudaiwa kuchelewa kambini, mshambuliaji huyo ameibuka na kulishangaa shirikisho kwa uamuzi huo.

TFF mwanzoni mwa wiki hii katika taarifa zake lilieleza kwamba Mrwanda, aliondoka mapema nchini Vietnam ambako anacheza soka la kulipwa, lakini amechelewa kujiunga na kambi ya timu ya taifa.

Kutokana na hali hiyo, shirikisho hilo lilisema haliwezi kuchukua hatua yoyote kwani suala hilo ni la Kamati ya Ufundi, ambapo baada ya kulijadili wataliwasilisha kwa Kamati ya Utenda ya TFF.

Akizungumza na kipindi cha michezo cha redio moja jijini Dar es Salaam juzi usiku, Mrwanda alisema anashangaa kuona taarifa hizo zinatolewa katika vyombo vya habari, yeye akiwa hana taarifa yoyote.

"Nasikitika mno kuona TFF, imetoa taarifa hii kwa vyombo vya habari bila kuwasiliana nami, hilo tatizo wanalosema lilikuwa lipo juu ya uwezo wangu na nisingeweza kufanya kama walivyotaka.

"Nilikuwa jijini (Dar es Salaam) nikifanya shughuli zangu, baada ya kupewa ruhusa na mwajiri wangu (timu yake ya DT Long), wakati nipo huku naona ndiyo timu ya taifa, ilikuwa kambini sasa nisingeweza kujiunga hadi nipewe ruhusa na klabu," alisema.

Alisema baada ya kumaliza mambo yake alirudi Vietnam, ambapo alipofika huko aliruhusiwa na klabu yake kujiunga na timu ya taifa na ndiyo maana akawa amechelewa tofauti na ilivyotarajiwa.

Mrwanda huyo alisema kikubwa kinachoonekana hakukuwa na mawasiliano mazuri, kati yake na TFF ndiyo maana anaonekana kama hakuwa na nia ya kuwahi kujiunga na wenzake Taifa Stars.

Aliongeza kwamba mpaka sasa ameshindwa kuondoka, baada ya kukosa viza ambayo awali aliahidiwa na TFF kushughulikiwa mapema pindi watakapotoka Morocco, lakini mpaka sasa kimya.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura kuzungumzia sakata hilo, alisema kuhusu viza si jukumu la shirikisho kumtafutia mchezaji bali ni la mwajiri wake.

"Shirikisho kazi yake kubwa ni kusaidia kuandika baadhi ya nyaraka, ili kumrahisishia mchezaji kupata viza, lakini si jukumu la moja kwa moja ambalo kama mchezaji akikosa basi lawama lipewe shirikisho," alisema Wambura.
 Na Zahoro Mlanzi

SIKU chache baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuiachia Kamati ya Ufundi ya shirikisho hilo suala la mshambuliaji wa timu ya taifa (Taifa Stars), Danny Mrwanda kudaiwa kuchelewa kambini, mshambuliaji huyo ameibuka na kulishangaa shirikisho kwa uamuzi huo.

TFF mwanzoni mwa wiki hii katika taarifa zake lilieleza kwamba Mrwanda, aliondoka mapema nchini Vietnam ambako anacheza soka la kulipwa, lakini amechelewa kujiunga na kambi ya timu ya taifa.

Kutokana na hali hiyo, shirikisho hilo lilisema haliwezi kuchukua hatua yoyote kwani suala hilo ni la Kamati ya Ufundi, ambapo baada ya kulijadili wataliwasilisha kwa Kamati ya Utenda ya TFF.

Akizungumza na kipindi cha michezo cha redio moja jijini Dar es Salaam juzi usiku, Mrwanda alisema anashangaa kuona taarifa hizo zinatolewa katika vyombo vya habari, yeye akiwa hana taarifa yoyote.

"Nasikitika mno kuona TFF, imetoa taarifa hii kwa vyombo vya habari bila kuwasiliana nami, hilo tatizo wanalosema lilikuwa lipo juu ya uwezo wangu na nisingeweza kufanya kama walivyotaka.

"Nilikuwa jijini (Dar es Salaam) nikifanya shughuli zangu, baada ya kupewa ruhusa na mwajiri wangu (timu yake ya DT Long), wakati nipo huku naona ndiyo timu ya taifa, ilikuwa kambini sasa nisingeweza kujiunga hadi nipewe ruhusa na klabu," alisema.

Alisema baada ya kumaliza mambo yake alirudi Vietnam, ambapo alipofika huko aliruhusiwa na klabu yake kujiunga na timu ya taifa na ndiyo maana akawa amechelewa tofauti na ilivyotarajiwa.

Mrwanda huyo alisema kikubwa kinachoonekana hakukuwa na mawasiliano mazuri, kati yake na TFF ndiyo maana anaonekana kama hakuwa na nia ya kuwahi kujiunga na wenzake Taifa Stars.

Aliongeza kwamba mpaka sasa ameshindwa kuondoka, baada ya kukosa viza ambayo awali aliahidiwa na TFF kushughulikiwa mapema pindi watakapotoka Morocco, lakini mpaka sasa kimya.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura kuzungumzia sakata hilo, alisema kuhusu viza si jukumu la shirikisho kumtafutia mchezaji bali ni la mwajiri wake.

"Shirikisho kazi yake kubwa ni kusaidia kuandika baadhi ya nyaraka, ili kumrahisishia mchezaji kupata viza, lakini si jukumu la moja kwa moja ambalo kama mchezaji akikosa basi lawama lipewe shirikisho," alisema Wambura.

Alisema kwa kawaida wanapomhitaji mchezaji wa nje, huwa wanawasiliana na timu yake pamoja na shirikisho la soka la nchi husika na baadaye mchezaji, hivyo wao walituma tiketi kwa wakati, lakini DT Long hawakuwaeleza kwamba mchezaji huyo hayupo.

No comments:

Post a Comment