*Yaichapa Toto 4-2 *Asamoah aibuka shujaa
Na Zahoro Mlanzi
MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Yanga imeendeleza wimbi lake la ushindi kwa kuichapa Toto African ya
Mwanza mabao 4-2 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga imepanda kwa nafasi moja mpaka ya tatu kwa pointi 18 sawa na Azam FC ila zinatofautina kwa mabao huku Simba ikiendelea kuongoza kwa pointi 24 ikifuatiwa na JKT Oljoro yenye pointi 19.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo wa jana yalifungwa na mshambuliaji Kenneth Asamoah ambaye alifunga mawili na kumfanya afikishe mabao saba akiongoza katika orodha ya wafungaji akifuatiwa na John Bocco ambaye amefunga sita.
Mabao mengine ya Yanga yalifungwa Jerryson Tegete na Haruna Niyonzima.Licha ya kufunga bao hilo Tegete hakushangilia kutokana na timu hiyo kufundishwa na baba yake John Tegete.
Dakika 10 za mwisho ndizo zilizoifanya Toto kupata mabao hayo ya kufutia machozi ambapo mabao yote yalifungwa na Mohamed Soud.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa upande mmoja kipindi cha kwanza, Yanga iliwachukua dakika nane kufunga bao la kwanza lililofungwa na Niyonzima kwa shuti nje ya eneo la hatari ambapo kipa Maganga Seif aliruka bila mafanikio.
Dakika nne baadaye, Asamoah alifunga la pili akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Godfrey Taifa na kujaa wavuni.
Yanga iliendelea kutawala mchezo huku ikionekana kama inafanya mazoezi kutokana na kutokuwa na ushindani ambapo dakika ya 16, Tegete alifunga la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi ya Idrisa Rashid.
Baada ya kufungwa mabao hayo, dakika ya 39, Toto alizinduka na kufanya shambulizi baada ya Phabian James kupiga shuti dhaifu lililodakwa na kipa Yaw Berko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Toto ikianza kuonesha ushindani ambapo dakika ya 66, Ladislaus Mbogo alishindwa kukwamisha mpira wavuni kutokana na krosi ya Soud.
Toto iliendelea kucheza kwa kujiamini na dakika ya 81, Soud aliifungia timu yake bao kwa shuti lililomuacha kipa Berko akishangaa na mpira kujaa wavuni.
Yanga ilifanya mabadiliko ambapo iliwatoa Tegete na kuingia Hamis Kiiza, Rashid na kuingia Rashid G*Yaichapa Toto 4-2 *Asamoah aibuka shujaa
Na Zahoro Mlanzi
MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Yanga imeendeleza wimbi lake la ushindi kwa kuichapa Toto African ya Mwanza mabao 4-2 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga imepanda kwa nafasi moja mpaka ya tatu kwa pointi 18 sawa na Azam FC ila zinatofautina kwa mabao huku Simba ikiendelea kuongoza kwa pointi 24 ikifuatiwa na JKT Oljoro yenye pointi 19.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo wa jana yalifungwa na mshambuliaji Kenneth Asamoah ambaye alifunga mawili na kumfanya afikishe mabao saba akiongoza katika orodha ya wafungaji akifuatiwa na John Bocco ambaye amefunga sita.
Mabao mengine ya Yanga yalifungwa Jerryson Tegete na Haruna Niyonzima.Licha ya kufunga bao hilo Tegete hakushangilia kutokana na timu hiyo kufundishwa na baba yake John Tegete.
Dakika 10 za mwisho ndizo zilizoifanya Toto kupata mabao hayo ya kufutia machozi ambapo mabao yote yalifungwa na Mohamed Soud.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa upande mmoja kipindi cha kwanza, Yanga iliwachukua dakika nane kufunga bao la kwanza lililofungwa na Niyonzima kwa shuti nje ya eneo la hatari ambapo kipa Maganga Seif aliruka bila mafanikio.
Dakika nne baadaye, Asamoah alifunga la pili akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Godfrey Taifa na kujaa wavuni.
Yanga iliendelea kutawala mchezo huku ikionekana kama inafanya mazoezi kutokana na kutokuwa na ushindani ambapo dakika ya 16, Tegete alifunga la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi ya Idrisa Rashid.
Baada ya kufungwa mabao hayo, dakika ya 39, Toto alizinduka na kufanya shambulizi baada ya Phabian James kupiga shuti dhaifu lililodakwa na kipa Yaw Berko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Toto ikianza kuonesha ushindani ambapo dakika ya 66, Ladislaus Mbogo alishindwa kukwamisha mpira wavuni kutokana na krosi ya Soud.
Toto iliendelea kucheza kwa kujiamini na dakika ya 81, Soud aliifungia timu yake bao kwa shuti lililomuacha kipa Berko akishangaa na mpira kujaa wavuni.
Yanga ilifanya mabadiliko ambapo iliwatoa Tegete na kuingia Hamis Kiiza, Rashid na kuingia Rashid Gumbo mabadiliko yaliyofanya kupata bao la nne lililofungwa na Asamoah akiunganisha krosi ya Kiiza.
Ikiwa imebaki dakika moja kabla ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, Soaud aliifungia timu yake bal pili kwa shuti nje ya eneo la hatari.
Yanga:Berko, Taifa/Fred Mbuna, Abuu Ubwa, Nadir Haroub, Ibrahim Job, Juma Seif, Shamte Ally, Niyonzima, Asamoah, Tegete/Kiiza na Rashid/Gumbo.
Toto:Seif/Mustapha Mabrouk, John Bosco, Philemon Mwandesile, Peter Mutabuzi, Mbogo, Lulanga Mapunda, Soud, Tonny Ndollo/Castor Mumbala, Bakari Kigodeko, Enyinna Darlington/Mwita Kamaronge na James.umbo mabadiliko yaliyofanya kupata bao la nne lililofungwa na Asamoah akiunganisha krosi ya Kiiza.
Ikiwa imebaki dakika moja kabla ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, Soaud aliifungia timu yake bal pili kwa shuti nje ya eneo la hatari.
Yanga:Berko, Taifa/Fred Mbuna, Abuu Ubwa, Nadir Haroub, Ibrahim Job, Juma Seif, Shamte Ally, Niyonzima, Asamoah, Tegete/Kiiza na Rashid/Gumbo.
Toto:Seif/Mustapha Mabrouk, John Bosco, Philemon Mwandesile, Peter Mutabuzi, Mbogo, Lulanga Mapunda, Soud, Tonny Ndollo/Castor Mumbala, Bakari Kigodeko, Enyinna Darlington/Mwita Kamaronge na James.
Waandishi wa Tanzania kweli mmechoka. Hivi hii habari imehaririwa kweli!!!! Waandishi wa habari wa gazeti hili, Mwananchi na Sports ni wachovu, maskini wa kisomo chao na wasiojali kazi yao.
ReplyDeleteWanaonesha wazi kabisa ni jinsi gani walivyo kuwa ni mashabiki wa Yanga.
ReplyDeletewanaonesha ni jinsi gani walivyokuwa ni mashabiki wa Yanga na sio waandishi wa habari wanaoijua kazi yao vizuri.
ReplyDelete