01 November 2011

Lema ajipelela rumande

*Akataa dhamana, adai jela panamfaa kupigania haki
*Asema atashinda kwani vita anavyopiga ni vya Mungu
*Adai CHADEMA haitatishwa kwa silaha wala jela 


Na Said Njuki, Arusha

MBUNGE wa Arusha mjini Bw. Godbless Lema, (CHADEMA) ameamua kwa hiari yake kwenda rumande baada ya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumsomea mashitaka matano yanayomkabili na wenzake 18 licha ya dhamana kuwa wazi.

Mwanasiasa huyo alifikia uamuzi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha mbele ya Hakimu Bi. Judith Kamala, baada ya hakimu huyo kutoa masharti ya dhamana yaliyotaka kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua toka kwa mtendaji wa kata na fungu la dhamana la sh. 500,000 ambapo washitakiwa saba walitimiza masharti hayo.

Katika waraka wake aliousambazwa mahakamani hapo baada ya kukataa kuwekewa dhamana Bw. Lema alisema jela ni mahali pa kuishi kwa lengo la kupiga vita dhidi ya uonevu, ukandamizaji wa haki na utu wa binadamu.

Alisema hana wakati mgumu kuchukua maamuzi hayo kutokana na kile alichokiita kuwa ni upendo alionao kwa watu wa Arusha na nchi yake ambayo ni sababu  ya msingi ya kumfanya afikie maamuzi hayo.

“Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu, katika mazingira haya nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri atakayeweza kuona thamani ya watu wengine.

“Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi, tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, haki na ukweli hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya maana ya kuishi,”ilisema waraka huo.

Bw. Lema alisema alipoona mabinti wadogo wakifanya biashara ya ukahaba, akatafakari kisha akatafakari tena, dhahabu, almasi, milima na mabonde, tanzanite, samaki, ureniamu, makaa yam awe, utalii, ardhi na kilimo na zaidi utu na mahusiano mazuri akaona hawezi kukaa kimya tena lazima atoe sauti isikike.

Mbunge huyo aliongeza kuwa ni heri vita inayotafuta haki,usawa na amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu na kwamba katika msingi huo hofu na mashaka vimekosa thamani kwake na kusisitiza kauli yake ya juzi kuwa  hatamwogopa mtu yeyote mwenye silaha, mwenye cheo chohote na wala hataogopa jela yoyote ilihali anapigania haki na utu.

“Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendelea kutunyanyasa bila sababu ya msingi.

"Sisi tunajua tutashinda kwa sababu haki tunayoipigania ni makusudi ya Mwenyezi Mungu, leo nitaenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa nia ya kujitafutia utukufu,”alidai Mbunge Lema.

Bw. Lema na wenzake wanakabiliwa na mashitaka manne ya kutenda njama ya kufanya kosa mahakamani, kufanya maandamano yasiyo ya halali toka mahakamani hadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, kutokubali amri halali ya Polisi iliyowataka kutawanyika na kufanya mkusanyiko usio halali wa zaidi ya watu 100 katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Hata hivyo Bw. Lema kwa upande wake akikabiliwa na shitaka lingine la tano ambalo ni kuhamasisha watu kutenda kosa na kukataa amri ya Jeshi hilo. Washitakiwa wote walikana mashitaka hayo.

Washitakiwa haa ambao wote walitimiza masharti ya dhamana ni pamoja Diana Anthony, Gerald Majengo, Hassan Mdigo, Lomaiyan Nassi, Rashidi Shumbeti, Daudi Hamza na Bahati Daudi.

Wengine ni Kelvin Simon, Amendeus Chami, Meshack Betuel, Hamadi Shabani, Richard Mollel, Frank Daniel, Leonard Kiologo, Juliana Lukumay, Jafarry Samwel, Mussa Mwakilema, Dina Kamtoni na Joseph Simon.

Mwendesha mashitaka wa serikali, Bw. Augustine Komba, alisema upelelezi wa
kesi hiyo bado haujakamilike na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa shauri hilo hivyo hakimu kuliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 14 mwaka huu itakapotajwa tena.

15 comments:

  1. Lema umesema kweli,silaha,jela mabomu na vitisho haviwez kunyamazisha ummakudai haki yao

    ReplyDelete
  2. MHARIRI HII HABARI INA UPENDELEO WA KUMKANDAMIZA HUYU MHESHIMIWA MBUNGE, HAJAJIPELEKA JELA BALI MAMILLIONI YA WATANZANIA WAMEKUWA WAKIBAMBIKWA KESI NA POLISI! ALICHOFANYA NIKUONESHA HALI HALISI YA JESHI LA POLISI, NA POLISI HAO WATATUPELEKA PABAYA!

    ReplyDelete
  3. Mwalimu nyerere alipokuwa anavunja DUSO 1978 Pale chuo kikuu cha DaresSalaam alisema kuwa kuvunja Duso hakuna maana ya kuwanyima haki zao za kikatiba wanataaluma hao na akaenda mbali zaidi na kusema kuwa endapo wataona milango ya haki imefungwa basi waivunje ili wapate haki zao. Rais John Kennedy wa marekani wakati fulani alipokuwa anahutubia moja chuo kikuu nchini mwake alisema na namnukuu kwa kiingereza 'the hottest place in the hell will be maintained for those who in great moral crisis maintain their neutraulity' CCM naamini ni chama kinachoongoza serikali iliyowekwa kwa ridhaa ya wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa na ndio maana kura za rais zinazidi idadi ya wanaCCM. Hivi Arusha hakuna serikali? kwanini huyu bwana Godbless Lema amekuwa akisumbuliwa na polisi na kubambikiziwa kesi hawalishughulikii suala hili hivi wanataka kuona umwagikaji damu kama ulivyotokea hapo awali waanze kumpa ripoti za uwongo Mhe. waziri Mkuu? inashangazwa mtu anayetembea kwa miguu wanasema amepanga mkusanyiko wa watu basi wao wamuandalie ulinzi kama wanadhani anaweza kudhurika lakini si kweli kwani Lema ni kijana wa arusha palepale alitembea kwa miguu na kupata gari kusimfanye yeye asahau asili. niwatafadharishe POLISI Arusha Msiwe wavivu wa kufiki nakuwapa wakati mgumu makao makuu ya polisi nguvu ya umma hamuwezi kamwe kuzuiwa namna hiyo mtasababisha mauaji makubwa hapo arusha. Mhe.Godbles Lema uamuzi uliouchukua ni mzuri ukiwa waziri wa mambo kivuli ukaone watanzania wanavyobambikiziwa kesi, ukaone askari magereza wanavyofanya biashara na wafungwa, ukaone jinsi pesa za serikali zinavyopotea tofauti na ripoti nzuri za wakubwa wetu. mwisho ukaone wafungwa wasivyotibiwa kwa kukosa panadol katika zahanati zao. Mandela alifungwa lakini ukweli ulipochomoza akawa rais wa Afrika ya Kusini. Nakutakia mafanikio mema Bwana LEMA!!

    ReplyDelete
  4. polisi tendeni haki mbona Mh Sendeka alipokua na kesi wafuasi wake walifika mahakamani wengi sana mbona hakuwekwa chini ya ulinzi?au kwavile yeye ccm na lema chadema? Kamanda Lema Ukombozi Unakuja Usihofu

    ReplyDelete
  5. KAMA NI VITA BASI NAVIJE TUMEKANDAMIZWA YAKUTOSHA WATANZANIA

    ReplyDelete
  6. TANZANIA HII TULIYOKUWA TUKIJIVUNIA AMANI LEO ASKARI KUWA WAKWANZA KUVUNJA AMANI NA SERIKALI INABARIKI, JAMANI WATANZANIA TUNANGOJA NINI?

    ReplyDelete
  7. kaza moyo Lema hii ndiyo serikali kandamizi iliyo jaa uonevo rushwa na ufisadi, askari kutofuata maadili yakazi na kuifurahisha serikali iliyo madarakani kwa kuwakandamiza wanyonge na wapigania haki wa CHADEMA, makamanda msikate tamaa tuko nyuma yenu tunajipanga

    ReplyDelete
  8. WARAKA WA GODBLESS LEMA KWA WANA WAARUSHA NA WATANZANIA WAPENDA MABADILIKO KOKOTE KULE WALIPO ULIMWENGUNI

    JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.

    Wapendwa wapiga kura wangu na Watanzania wenzangu.

    Sina wakati mgumu kuchukua maamuzi haya yanayotokea leo. Upendo huu nilio nao kwa watu wa Arusha na nchi yangu ni sababu ya msingi ya maamuzi haya. Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu.

    Katika mazingira haya, nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri atakayeweza kuona thamani ya watu wengine. Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi.

    Tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, haki na ukweli. Hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya maana ya kuishi.

    Waliofungwa kwa kuonewa na kuteswa, waliokosa chakula na kulala nje, waliokwenda hospitali na kukosa madawa, waliokosa ajira na kipato mpaka kujikuta wametoroka familia zao, waliopoteza matumaini ya maisha, waliopora utajiri wa nchi yetu kwa manufaa yao binafsi, walionunua haki na sheria dhidi ya wajane na wanyonge na kuwapora vipato vyao vidogo na mashamba yao, USIULIZE SABABU NINI!

    Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati wajane na wanyonge wanaonewa.

    NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati hizi.

    Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani wanaomba chakula, nilipoona wazee wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TE NA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu, Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu.

    Na sasa siwezi kukaa kimya tena. NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote, mwenye silaha yoyote, mwenye cheo chochote na wala sitaogopa jela yoyote katika kupigania haki, utu wa kweli katika jamii yangu.

    Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasabil a sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.

    Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ,” JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.

    Kila mara nilipotishiwa nikagundua wanaonitishia, wananitishia kwa jela na mauti. Na mimi nikagundua na nikatambua ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu mwenzangu.

    Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu.

    Watakaotubeza na kututukana wasameheni kwani wanahitaji ukombozi wa fikra, watakaotupongez a na kutuonea huruma wafundisheni ujasiri na waambieni mapambano bado yanaendelea tunahitaji umoja wao. Nitarudi mapema. MSIOGOPE, MSIOGOPE, MSIOGOPE , MUNGU YUPO UPANDE WETU.

    Mhe Godbless Lema (MB) – Arusha Mjini 31 Oktoba 2011.
    Quote

    KAMA SIO JUHUDI ZANKO NYERERE, MAFISADI WANGESOMA WAPI, HOOO KAMA SIO

    ReplyDelete
  9. LEMA NI KICHWA NAMKUBALI SANA

    ReplyDelete
  10. hao kakangu lema ni kama nyayo za gadafi watu hawatatki wanangangania mungu atawaonyesha tena nataka kusema ndg watanzania kuna msemo mmoja mwujue wanasema mwogopeni mungu wahashimu binadamu hawa binadamu unaoishi nao ndio wa mana kuliko hizo pesa zako au hiyo amri yako siku moja hawa ccm wataona cha mtema kuni tupo tayari kwa lolote tumewachoka wapeni wengine pia wale wavimbe matumbo kama nynyi

    ReplyDelete
  11. Mungu akulaani Lema ikiwezekana ufie hukohuko jela. Arusha ni ya Waarusha na nyie wachaga mmetuletea kila aina ya balaa,huko kwenu Moshi husikii Mbunge Masanja au Ole Naiko ni akina Ndesamburo,Mbatia,Mtei,Mbowe,Kimario,Selasini, nawaombeni watu wa Arusha mbadilike mchague watu wa kwenu sasa,hata kama mtaniita mbaguzi sijali ila nawaambia wabaguzi ni wachaga. Huyo Lymo akifa leo anaenda zikwa Machame au Rombo ni muongo hana uchungu na arusha huyo,hivi kweli itokee jambo jema aambiwe achague Moshi au Arusha kweli huyo atachagua Arusha. Mungu muuwe huyu mtu huko jela na Waarusha its hightime now kuchagua mzawa wa Arusha kwa maana mbunge wenu atokane na kabila la mkoa wenu na si vinginevyo,wambulu waende mbulu,wa Moshi waende Moshi

    ReplyDelete
  12. Pole sana wewe unayesema Lema afie jela,kwanza ni mpumbavu sana, ana kosa gani lema? kwa kumtukana kiasi hicho?Wewe utaanza kufa kabla ya lema,Kuna washomari wako bungeni sio wazaliwa wa tanzania bali wamekuja na kuomba uraia wanaongoza nchi, kwanini huyo mtu wa moshi asiwe mbunge wa arusha na ni mkoa mmoja? ukatubu dhambi zako kama hutaki unakufa wewe ndani ya siku tano.

    ReplyDelete
  13. du watu wamekataa tamaa mpaka basi,usiogope kufikiri na kutoa wazo chanya kwa faida ya wote, watanzania siyo makabila ila ni utanzania wao, na pale ambapo upinzani umekomaa ndipo sehemu ambayo mamluki huwekeza kudhoofu nguvu ya umma kwa kupanda mbegu za chuki,Lema pigana onyesha hao wavivu wa kufikiri kuwa wanatakiwa kufikiri na kusimamia mawazo yao na si ya watu wengine,Nguvu ya umma itashinda ipewe muda,

    ReplyDelete
  14. asante kaka lema ,, nimefarijika sana kuona wapo bado watu wenye machungu na nchi hii.tuna mahangaiko mengi watz kwa sasa,, inabidi tuamke na tuseme imetosha. angalia ripoti za ubadhilifu wa fedha za wavuja jasho kila siku. then unaenda hospital na kukuta watu wamepanga foleni kusubiri kumuona daktari ambae akikuona anakwandikia msururu wa dawa ukanunue kwa pesa zako,, sijui tunaenda wapi, njaa, foleni za magari njiani, wao wanananeemeka tu, akikohoa kidogo yuko london kuchekiwa..... its too much, tuamke jamani,, wakati ndio huu

    ReplyDelete
  15. Huo Utanzania ni kwa Arusha tu,ndio makabila yote mbona kwenu Moshi ni Wachaga tu?

    ReplyDelete