02 November 2011

SAKATA LA MBUNGE LEMA- CHADEMA watoa tamko

Na Heri Shaaban

*Wasema uamuzi wake ni ushindi wa harakati za ukombozi
*Wasisitiza hakuna silaha, jeshi linaloshinda vita ya haki

SIKU moja baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema (CHADEMA), kukataa asiwekewe dhamana katika Makahama ya Hakimu Mkazi Arusha na kwenda rumande siku 14 katika Gereza la Kisongo, uongozi wa chama hicho Mkoa wa Dar e Salaam umesema uamuzi huo ni ushindi tosha katika harakati za ukombozi wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, Katibu wa chama hicho mkoani humo, Bw. Henry Kilewo, alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeamua kutekeleza mkakati wa kuwatesa viongozi wa chama hicho kwa siri.

“Mheshimiwa Lema kama Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, amekuwa akifuatwa na Jeshi la Polisi mara kwa mara na kufanyiwa vitendo vingi vya udhalilishaji na unyanyasaji,” alisema.

Aliongeza kuwa, Oktoba 28 mwaka huu, Bw. Lema wakati akitoka mahakamani alisindikizwa na wanachama wake kutoka mahakamani hadi ofisini kwake na kukuta wananchi wakimsubiri ili awahudumia kama mbunge wa jimbo lao.

Alisema wakati akiendelea kuongea nao, ghafla polisi walifika eneo hilo na kuwakamata wananchi aliokuwa akiwahudumia ambao walipelekwa Kituo Kikuu cha Polisi ambapo Bw. Lema alipokwenda kuwawekea dhamana, naye aliwekwa chini ya ulinzi kwa madai ya kufanya maandamano bila kibali.

“Mandamano yapi ambayo Bw. Lema ameyafanya wakati alikuwa ofisini kwake, maandamano wanayosema ni hayo ya kutoka mahakamani hadi ofisini kwake? Kama kuondoka kwake mahakamani na wafuasi ni kosa kisheria.

“Mheshimiwa Ole Sendeka (Mbunge wa Simanjiro), alipokuwa akitoka mahakamani alikuwa akiondoka na kundi kubwa la wafuasi wake, Mwenyekiti wa UV-CCM Mkoa wa Arusha naye alikuwa akienda Kituo Kikuu cha Polisi na kundi kubwa la wafuasi,” alihoji Bw. Kilewo.

Wasisitiza hakuna silaha, jeshi linaloshinda vita ya haki

Alisema hakuna silaha au jeshi lolote duniani ambalo limeweza kushinda vita dhidi ya ukweli, haki na uwazi hivyo chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, kiunawaunga mkono wakazi wa Arusha kwa kumpata mbunge anayetetea maslahi yao kwa mzigo na kuamua kwenda gerezani kwa ajili ya watu wake.

Bw. Kilewo alisema watu wnaopinga na kukejeli uamuzi wa Bw. Lema kukataa dhamana, wathubutu kufanya zira katika hospitali na kuvaa sura za uhalisia wa kibinadamu ili waone watu wanavyotaabika kwa kukosa matibabu mbali ya kuwa miongoni mwa walipa kodi.

“Kwanini Bw. Lema asiende rumande wakati anasimamia mambo ya msingi na hayatekelezwi, tukiandamana tunaonekana tunavunja sheria hivyo ni afadhali kwenda sehemu wanayodhani tunaogopa ili tukae kimya kumbe hatuogopi, Mungu yupo upande wetu na tunaelekea kushinda unyanyasaji huu,” alisema.

Alisema kwa kuonesha wako pamoja na Bw. Lema, wanampongeza Bw. Lema kwa kupeleka ujumbe kwa watawala wanaodhani wanaweza kutumia magereza kama sehemu ya vitisho ili kukwamisha harakati zao.

11 comments:

  1. Mh. usiogope wala usijali kunyanyaswa kwani saa ya ukombozi ndio hii. Hata Nelson Mandela alifungwa jela miaka 27 na hatimaye S.Africa ikapata ukombozi kutoka kwa Makaburu. TZ imekuwa ni ya unyanyasaji tu hata Polisi Mkoani Arusha wanashangaza ni kwamba hawana kazi? Mbona masuala ya uhalifu yanasikika kila kukicha hawafuatilii? Kazi yao ni kumfuata Lema matakoni tu? Kweli hatuna Jeshi la Polisi ila tuna Jeshi la CCM. Mh. Kikwete suala hili mtaliona dogo lakini....................!!!!! Mimi nashauri Polisi fanyeni kazi kwa ufanisi ni si kiushabiki. Kumbukeni Libya walianza hivi hivi, Tunisia nako hivi hivi.

    ReplyDelete
  2. Chadema badirisheni mikakati iliyopo inaanza kuchuja. I meaning change your positioning especially at village level, your competitor appears quite strong there, if you fail to arrest the situation you will fail again. Hire experts to study the problem its when you can come up with a strong approach. Hire marketers I am sure they can put you in a strong footing

    ReplyDelete
  3. 1. Lema this is a piece of advise to you

    2. Arusha is the stronghold of your party.

    3. Your party is now using you personally to keep the stronghold visible, present, happening and vibrant at your expenses.

    4.You should therefore be aware of it and react to this plight carefully.

    5. Arusha is vey sensitive to any type of unrest as it greatly affect its economic performance due to the reasons which are known to every one of us.

    6. I am not sure if all your wananchi will account what you are engineering as important to them.

    7. I see some of them will one day turn against you inasmuch as their economic activity will be negatively affected. Remember that in contemporary public leadership leader are measured by economic performance.

    8. Be careful your political future is at lisk.

    ReplyDelete
  4. Lema anajitafutia umaarufu wa kisiasa kupitia mgongo wa wanyonge.

    ReplyDelete
  5. Toka lini mchaga akakupa haki ? huyo anajitafutia umaarufu tu. Arusha mmejitakia,sasa mnakiona cha moto.hapo ni hivyohivyo tu hadi 2015,wachaga wana agenda ya siri. Arusha imeipiku Moshi kibiashara sasa kunapokuwa na matatizo kwenu Arusha kila siku hamna atakayefanya biashara hapo,ila hao majambazi watafanya. atababaisha na kiduka kidogo huku wakiua watu na kupora mali zenu. Arusha nia ya Waarusha,huyo Mangi akifa leo anaenda kuzikwa kibosho

    ReplyDelete
  6. Wanaodhiaki hali hii ya Arusha akili zao ni finyu wameona ccm wamefika kumbe upumbavu tu,ngoja watu wanyamaze ukadhani hawajui au hawaoni madhambi ya ccm na polisi wao,mwaka 2015,ccm na polisi mtaona nyota tu.Haya mabo si ya kudhihaki ccm na polisi wanachofanya si sahihi kabisa mimi ni ccm lakini nategemea kujiengua maana mambo mnayofanyia wenzio si mema kutokana na ufisadi tu,subiri Libya huyo Gadafi wenu na kule Misri wako wapi hao wanaume mnaowaona walifanya nchi haitawaliwi na mwingine??sasa subiri,vyuoni mikopo haitoki kihalali,hospital dawa ndo hizo,shule ndo hizo za kata,barabara ndo hizo zinajengwa asubuhi kesho rami hakuna,kila mahali ufisadi.Ninyi mnaodhiaki kweli sikio lakufa halisikii dawa.Mmeridhika tu eti Lema anajitakia.Watoto wako au ndugu zako wanaosoma hali wanaionaje we unashabikia eti Lema anajitakia si ujinga huo.Subiri ukadhani watu hawaoni.Itafika mwisho ccm yetu naamini kabisa kwa jina la Yesu aliyeumba mbingu na nchi,napongeza viongozi kama Mbunge wa Mwibara,ambaye wamekataa r5ipoti ya fedha ya shirika hilo unalolijua.Na akasema kesi ya kuku unapeleka mtu jela,kesi za mabilioni watu wanasema ilikuwa hali ya kibinadamu,mnapoambiwa ukweli mnatoa tu macho.Mbona nyie polisi mnashindwa kukamata majambazi wanaibia raia usiku na mchana lakini m,naangalia eti mnalinda raia na mali yake.Mali gani mnalinda ninyio au ninyi ndo wale wale usiku.Subiri mwakla 2015.Mtatenguliwa viongozi wote kuanzia mashina hadi ikulu.Ahsante.

    ReplyDelete
  7. Cheki yake ya mshahara wa mwezi wa 10 si imeshatuna kwenye Account yake? Mweny macho haambiwi tazama!!!

    ReplyDelete
  8. Kama hii ndiyo type ya uongozi wa chadema kama mngechukua madaraka, basi hamfai kwa mwendo huuu, Chadema ndio kimbilio la Watanzania kwa sasa, ila viongozi wake wengi wahuni kama huyu jamaa, zingatieni situational approach, someni nyakati msilewe na influence mliyonayo.

    ReplyDelete
  9. ninyie watoto wa wenyeviti,madiwani,wabunge na mawziri wa ccm kuenjoy kenu wachache matunda ya nchi hii wakati wananchi walio wengi wanaendelea kutaabika kutokana na mfumo mbovu wa serikali chini ya chama kilichozeeka mpaka macho yake hayaoni na masikio yameshaziba yasisikie vilio vya watanzania kama si kiburi na kulewa madaraka kusiwafanye kuwa mnakoment chochote mnachojisikia tena kwa dharau.hata mbuyu ulianza kama mchicha kila lenye mwanzo lina mwisho gadafi angelijua hilo tu mpaka sasa angekuwepo libya tena akiabudiwa kutokana na mazuri aliyokuwa amekwishawafanyia walibya ila kiburi kimemponza sasa the same applied to chukua chako mapema ni wakati wa kutengeneza mazingira ya kutoka kwa heshima kabla ya kuondolewa kwa aibu.acheni hilo jeshi la ccm lifanye kazi wasizopenda ila kwajili ya kutii order

    ReplyDelete
  10. Uchumi bila haki hauna maana, Libya ilikua na uchumi mzuri lakini hakukua na haki na matokeo yake mmeyaona. Arusha tunataka haki na uhuru viwepo ndio maendeleo ya kweli yatafikiwa.

    ReplyDelete
  11. chadema ni ma freemason hata sign zao zinaonesha mtaruhusu ushoga

    ReplyDelete