26 October 2011

Kamati yaibana Wizara ya Viwanda

Na Peter Mwenda

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeitaka Wizara ya Viwanda na Biashara ieleze kwanini imedharau azimio la Bunge la
Muungano mwaka 2009, linalotaka ukaguzi wa magari nje ya nchi usitishwe ili kuokoa fedha nyingi zinazopotea kwa ujanja.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. John Cheyo aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa kikao cha kamati hiyo.

Alisema kuendelea na ukaguzi huo ni kulidharau Bunge na kusababisha hasara kwa Serikali Kuu.

“Ukaguzi unaofanywa kwa magari yanayoagizwa Tanzania kutoka nje ya nchi ni wizi, Wizara ibuni njia nyingine ya kufanya katika soko la Afrika Mashariki badala ya kuwabughudhi wafanyabiashara.

“Hivi karibuni tumeshuhudia matatizo ya sukari kuvushwa usiku kwa njia ya magendo, neno magendo limekwisha siku nyingi, kama majirani wanataka sukari yetu, pelekeni na wao walete bidhaa zao,” alisema Bw. Cheyo.

Aliiagiza Tume ya Ushindani, ikutane mara kwa mara ili kutafuta njia mbadala ya kufanya biashara yenye tija kwa wakulima.

Aliitaka Wizara hiyo ifahamu kuwa, tabia ya kuzuia watu kufanya biasha imepitwa na wakati ambapo Serikali inapaswa kusaidia wananchi ili kukidhi ushindani wa soko la pamoja. Na Peter Mwenda

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeitaka Wizara ya Viwanda na Biashara ieleze kwanini imedharau azimio la Bunge la Muungano mwaka 2009, linalotaka ukaguzi wa magari nje ya nchi usitishwe ili kuokoa fedha nyingi zinazopotea kwa ujanja.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. John Cheyo aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa kikao cha kamati hiyo.

Alisema kuendelea na ukaguzi huo ni kulidharau Bunge na kusababisha hasara kwa Serikali Kuu.

“Ukaguzi unaofanywa kwa magari yanayoagizwa Tanzania kutoka nje ya nchi ni wizi, Wizara ibuni njia nyingine ya kufanya katika soko la Afrika Mashariki badala ya kuwabughudhi wafanyabiashara.

“Hivi karibuni tumeshuhudia matatizo ya sukari kuvushwa usiku kwa njia ya magendo, neno magendo limekwisha siku nyingi, kama majirani wanataka sukari yetu, pelekeni na wao walete bidhaa zao,” alisema Bw. Cheyo.

Aliiagiza Tume ya Ushindani, ikutane mara kwa mara ili kutafuta njia mbadala ya kufanya biashara yenye tija kwa wakulima.

Aliitaka Wizara hiyo ifahamu kuwa, tabia ya kuzuia watu kufanya biasha imepitwa na wakati ambapo Serikali inapaswa kusaidia wananchi ili kukidhi ushindani wa soko la pamoja.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Na Peter Mwenda

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Joyce Mapunjo, alisema Wizara yake imeagiza tani 120 za sukari ili kukabiliana na uhaba huo  ambapo ili kukidhi ushindani ya kibiashara, Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), imekubali kutoa mkopo wa kujenga masoko mipakani.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Leandri Kinabo, alisema shirika hilo linafanya kazi kwa karibu na Wizara ili kuangalia njia ya kufuta ukaguzi wa magari ya nje.Bw. Joyce Mapunjo, alisema Wizara yake imeagiza tani 120 za sukari ili kukabiliana na uhaba huo  ambapo ili kukidhi ushindani ya kibiashara, Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), imekubali kutoa mkopo wa kujenga masoko mipakani.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Leandri Kinabo, alisema shirika hilo linafanya kazi kwa karibu na Wizara ili kuangalia njia ya kufuta ukaguzi wa magari ya nje.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Joyce Mapunjo, alisema Wizara yake imeagiza tani 120 za sukari ili kukabiliana na uhaba huo  ambapo ili kukidhi ushindani ya kibiashara, Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), imekubali kutoa mkopo wa kujenga masoko mipakani.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Leandri Kinabo, alisema shirika hilo linafanya kazi kwa karibu na Wizara ili kuangalia njia ya kufuta ukaguzi wa magari ya nje.

1 comment:

  1. Hivi huwa nanyi mnayasoma mliyoyaandika? Hii kitu gani sasa!

    ReplyDelete