26 October 2011

Basi lateketea, laua abiria nane

Na Mwandishi Wetu

WATU nane wanahofiwa kufa papo hapo baada ya basi la Kampuni ya Deluxe Coach linalofanya safari kati ya Dar es Salaam na
Dodoma, kupata ajali katika eneo la Misugusu Malandizi, Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 9.30 alasiri baada ya basi hilo kupasuka taili la mbele likiwa katika mwenda mkali, kutumbukia kwenye korongo na kuwaka moto.

Habari kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa, basi hilo leye namba T 534 AAT lilikuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Dodoma likiwa na abiria 42 wakati ilitoka ubungo na kwamba waliookolewa na kukimbizwa Hospitali ya Tumbi, Kihaba walikuwa 17 tu.

Akizungumza na Majira, Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Andrew Lwali, majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo ni 34, kati yao wanawake nane, wanaume 26 na abiria wawili wamelazwa lakini hali zao zinaendelea vizuri.

“Hadi sasa tumepata mafuvu mawili ya watu waliokufa na kuungua moto vibaya, pia naona mwili mwingine hapa mbele yangu, ila bado tunaendelea kuangalia maana tayari umenyanyuliwa,” alisema shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Ernet Mangu, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa yuko katika eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment