07 October 2011

Jinamizi la Igunga laing'ang'ania CCM

*Mabalozi 18 wajiengua, wadai rushwa ilitawala
*Madiwani Songea wagomea kikao kupinga uchaguzi
*M'kiti Lushotoa ajiuzulu kwa tuhuma za ufisadi


Na Waandishi Wetu, Igunga, Songea

Madiwani wagomea kikao

Wakati hali ikiwa hivyo Igunga, baadhi ya madiwani wa Chama CCM Manispaa ya Songea wamesusia
kikao kilichoitishwa na viongozi wa chama hicho kwa kile kilichodaiwa ni mgomo wa kudumu kushinikiza kujiuzulu kwa Meya wao aliyechaguliwa hivi karibuni Bw. Charles Mhagama.

Kitendo hicho ni dalili ya mgawanyiko wa wazi ndani ya CCM Wilaya ya Songea ambao unatokana na kile kinachodaiwa kuwa 'ni kulazimisha mambo kwa maslahi ya watu fulani' katika mchakato wa kumpata meya huyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari juzi kwa nyakati tofauti nje ya ofisi ya chama hicho  ambako kikao hicho kilipangwa kufanyika, madiwani hao walisema wameshtushwa na taarifa ya kuitwa kwenye kikao hicho bila kuelezwa ajenda zake wala muda wa kukaa kwenye kikao hicho.

Walisema wamefika kwenye kikao hicho wameshindwa kuwaona baadhi ya viongozi wa chama waliowaita, kitendo ambacho kinaonyesha ni dharau dhidi ya madiwani.

Baadhi ya Madiwani hao Bw. Christian Matembo wa Kata ya SeedFarm, Bw. Kurabest Mgwasa, Kata ya Msamala na Bw. Faustine Mhagama wa Kata ya Mshangano walisema kiu yao kubwa ni kutaka kuona Bw. Mhagama anajiuzuru ili uchaguzi mpya uitishwe kwani kura alizopata wakati wa uchaguzi hazikuwa halali.

“Tumechoka kuogopana ndani ya chama kwa kuwaacha wachache wawaburuze wengi kwa maslahi yaliyojificha, hatuwezi kuvumilia vitendo vya uvunjifu wa demokrasia vya kuwatisha madiwani waliotimiza haki yao ya kupiga kura za hapana kwenye uchaguzi wa umeya kwa kuwaita ni wasaliti wa chama,” alisema Diwani Matembo.

Alisema kuwa madiwani wengi walimpigia kura za hapana Meya Mhagama lakini wanashangaa kuona mtu huyo anatembelea gari ya Mstahiki Meya na kufanya kazi wakati siku ya kupiga kura uchaguzi ulivurugika na kusababisha madiwani kupigana.

Alidai matukio yote yaliyotokea siku hiyo ya uchaguzi wa Meya yalitokana na kumkataa Bw. Mhagama.

Diwani wa Kata ya Mshangano, Bw. Faustine Mhagama ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wote wa CCM alisema kitendo cha viongozi wa CCM wilaya kupendekeza madiwani watano wa chama hicho wavuliwe uanachama ni kuongeza mpasuko ndani ya CCM.

Walisema kuwahukumu hao ni kuwanyanyasa na kuwanyima haki yao ya msingi kama wawakilishi halali wa wananchi na kwamba hawawezi kuvumilia hali hiyo.

Alisema kanuni za kudumu za halmashauri zina eleza jambo lolote litakalofanyika kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani halipaswi kuhojiwa wala kujadiliwa na mamlaka nyingine, hivyo CCM Wilaya ya Songea Mjini kupitia Kamati ya Maadili na ya Siasa kuwahoji kwa kile kilichotokea kwenye Baraza ni kukiuka kanuni na kuendekeza makundi bila sababu ya msingi.

“Ili kulinda heshima ya Chama ni vema Bw. Charles Mhagama aridhie kujiuzulu nafasi hiyo ili uchaguzi urudiwe upya badala ya kuwanyanyasa baadhi ya madiwani wanaodaiwa kupiga kura za hapana na kusababisha diwani huyo kupitishwa,” alidai Bw.Mhagama

Naye Diwani wa Kata ya Msamala, Bw. Mgwasa alisema CCM Wilaya imependekeza madiwani watano wavuliwe uanachama ambapo hatma yao ipo kwenye ngazi yachama  mkoa lakini cha kushangaza madiwani hao nao wameitwa kwenye kikao hicho jambo ambalo lingeweza kuleta vurugu kubwa.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Mjini, Bw. Alfonce Siwale, alikiri kuitisha kikao hicho ambacho kilipaswa kifanyike juzi lakini kilishindikana kutokana na mahudhurio hafifu ya madiwani ambao hawakufika hata nusu yao, kati yao walioitwa wakiwa ni wale walipendekezwa kufukuzwa.

Alisema kikao hicho kilikuwa na agenda za kutaka kutuliza hali ya hewa iliyochafuka kisiasa ndani ya chama hicho kutokana na vurugu za uchaguzi wa umeya uliofanyika Septemba 23, mwaka huu.

Hata hivyo, alisema madiwani hao hawana mgomo wowote bali wengi wameshindwa kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa wapo safarini, hivyo kikao hicho kiliahirishwa hadi Octoba 11, mwaka huu katika ofisi za CCM.

Chama hicho kina madiwani 21 lakini waliofika kwenye kikao hicho walikuwa wanane.

Mwenyekiti ahamishia ofisi baa

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Magamba, Bw. Benno Lyakunda (CCM) amelazimika kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na tuhuma mbalimbali zilizotolewa na wananchi dhidi yake ikiwemo kuhamishia ofisi baa.

Madai ya wananchi hao yalitolewa juzi mbele ya Mbunge wa jimbo hilo, Bw. Henry Shekifu ambaye alikwenda katika kitongoji hicho kukagua shughuli za maendeleo na kuzungumza na wananchi.

Moja ya kero iliyomfanya Bw. Lyakunda kufikia uamuzi wa kujiuzulu mbele ya Bw. Shekifu ni kushindwa kufikisha kero za wananchi katika ofisi ya kitongoji na kuhamishia ofisi baa.

“Mheshimiwa, kitongoji hiki kina mradi wa kiwanda cha mbao lakini mapato yake yanaingia mifukoni mwa watu, minara ya simu inalipiwa kodi na ushuru, lakini wananufaika wachache, mkaa unachomwa ovyo hivyo kuharibu mazingira.

“Kuna malori yanabeba mawe, kila lori moja inauzwa sh. 10,000, lakini fedha zinaishia katika mifuko ya watu, wanunuzi hawapewi lisiti yoyote,” alisema mkazi wa kitongoji hicho Bw. Mahamudu Koti.

Mkazi mwingine Bw. Samwel Sabuni, alisema baadhi ya wanawake wa kitongoji hicho wananyanyasika kwa kunyang'anywa mapanga yao na kupigwa faini ya sh. 20,000 pindi wanapoingia msituni kuokota kuni huku wengine wakiachwa bila kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake, Bw. Lyakunda alisema tuhuma hizo hazina ukweli, hivyo anaamua kujiuzulu ili kudhihirisha madai yake kuwa ameonewa.

“Mheshimiwa mbunge, kuanzia sasa najivua uenyekiti, tuhuma zilizotolewa dhidi yangu hazina ukweli wowote,” alisema.

9 comments:

  1. CCM acheni ubabe huo ni uporaji wa demokrasdia chini. Madiwani nawasihi kuunganisha mawazo yenu kwa pamoja ili mpate nguvu ya kumtoa huyo meya.

    ReplyDelete
  2. KILICHONISHANGA NI WACHAGA KUANDAA KILIMANJARO SHEREHE ZA KUSHEREKEA USHINDI IGUNGA WAKATI CCM ILIWATUKANA KUWA CHADEMA NIYAWACHAGA! KISA MBOWE NI MCHAGA HUU SIYO UBAGUZI? WACHAGA WANABAGULIWA NDANI YA NCHI YAO BADO WANAFANYA SHEREHE KUMBE WANAWEZA KUWA MAJUHA NAO?

    ReplyDelete
  3. MIMI SINA CHA KUSHAURI ZAIDI YA KUSEMA CCM NAONA HAMJUI KUWA KIFO CHENU KIKO USONI.JAMANI NAONA WATANZANIA TUFIKE MAHALI TUFANYE MABADILIKO KWANI TUKIAMUA MIMI NA WW TUNAWEZA FANYA MABADILIKO. KAULI MBIU NI KWAMBA CCM WAMECHOKA NI BORA WAKAKUBALI WAPUMZIKE

    ReplyDelete
  4. KUHUSU SUALA LA MATAMSHI ALIYETOA KIONGOZI MMOJA WA CCM HUKO IGUNGA WAKATI WA KAMPENI. TAMSHI HILI LINAHUSU KULETWA KWA MAKOMANDOO WALIOFUNZWA AFGHANISTAN N.K. JE, VIONGOZI WA SERIKALI VIKIWAPO VYOMBO VYA USALAMA NA ULINZI WANALICHUKULIAJE HILI SUALA? KAMA NI LA KIUTANI, KIUHUNI AU KIMMZAHA WATUAMBIE SISI WANANCHI.KAMA WANAFIKIRIA NAMNA YA KULISHUGHULIKIA WATUAMBIE. IKIWA HATALISHUGHULIKIA MAPEMA ITAKUWA JAMBO LA AJABU. HAYO YANGALISEMWA NA KIONGOZI MWINGINNE WA CUF, SAU AU CHADEMA AU MWANANCI WA KAWAIDA NA KUSAMBAZWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI TAYARI SERIKALI INGEKWISHA WARUKIA. AU
    KWA KUWA CCM NI BABA NA MAMA WA VIONGOZI WA SERIKALI NDIO WANANYAMAZA KIMYA? SERIKALI NI YA WOTE HIVYO HATUA ZICHUKULIWE AU WANANCHI WATAANZA KUWA NA MAWAZO TOFAUTI.

    ReplyDelete
  5. Ndugu Mhariri hakikisha una-moderate maoni yanayotolewa katika jukwaa hili kwani huyu anayejiita anonymous kila mara anatoa maoni yanayoashiria uvunjifu wa amani

    ReplyDelete
  6. Ndugu Mhariri hakikisha una-moderate maoni yanayotolewa katika jukwaa hili kwani huyu anayejiita anonymous kila mara anatoa maoni yanayoashiria uvunjifu wa amani

    ReplyDelete
  7. WEWE KRUGER UNAONGEA NINI SASA HAPO? NANI ALITETOA MANENO YA UVUNJIFU WA AMAN KAMA C YULE KIONGOZI WA SISIEM. JE ULICHUKUA HATUA GANI? HAO MAKOMANDOO WAKO WAPI KAMA HAIKUWA KUWATIA HOFU WANANCHI NA HIVYO KUWAONDOLEA AMANI. BE REALISTIC PLS.

    ReplyDelete
  8. Ama kweli Tanzania kumekucha asiye amka atasimuliwa kifo cha CCM. jamani amkeni wote tushiriki! binafsi naamini CCM hakuna mabadiliko positive ila kitakacho endelea ni gumzo kila mkoa mpaka NEC kumtafta rais wa 2015 hapo ndipo maiti ya CCM itazikwa rasmi, hata KIKWETE analijua hilo ndio maana jana kawaita na kuwashangaa ndugu zake yeye karibu anang'atuka.

    ReplyDelete
  9. haya wandugu!!!ninasoma comments zenu nying na karbu zote zina maana kubwa na faida kubwa endapo tu mtajiandikisha kwenye daftar la kupiga kura mwaka 2015!na kuwahamasisha watu wakajiandikishe!kwan hyo ndo njia ya halali na isiyo na majungu kumchagua kiongoz umtakaye!!!

    ReplyDelete