21 October 2011

CUF yamjia juu Edward Lowassa

Na Grace Ndossa

CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema hakuna sababu ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa, kukaripia vyombo vya
habari na madai ya kuwaonea huruma Watanzania na kuwalaumu wenzake wakati na yeye ni sehemu ya matatizo yao.

Pia CUF imesema Bw. Lowassa hana sababu ya kulaumu umaskini wa Watanzania bali ashauriane na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wenzake namna gani waache maslahi binafsi na kutetea Mtanzania mnyonge anayeteseka kwa matendo yao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na kusainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Uchaguzi na Bunge wa CUF, Bw. Shaweji Mketo, ilieleza kuwa chama hicho kinamtaka Bw. Lowassa kutafakari utendaji wake kabla ya kujiuzulu uwaziri Mkuu.

Taarifa hiyo ya CUF iliseleza kuwa, Bw. Lowassa anajifanya kuwa na uchungu na matatizo yanayowakabili Watanzania wakati yanasababishwa na chama chake naye ni mhusika, hivyo dawa ni kukaa pamoja kuangalia jinsi ya kuyatatua.

Ilieleza kuwa Bw.Lowasa alikuwa kwenye serikali ya sasa kabla ya kujiuzulu na kwamba hadi sasa ni kiongozi muhimu ndani ya CCM kama mjumbe wa vikao vya juu vya chama hicho na  Mbunge wa Jimbo la Monduli hivyo matatizo ya Watanzania wanayowapata hivi sasa na yeye ni mmoja wapo kati ya watu waliochangia.

Chama hicho pia kilihoji sababu ya viongozi wa CCM ambao hawapo madarakani kwa sasa kujitokeza kukosoa mambo mbalimbali na kutoa mfano wa siku ya maadhimisho ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

"Mfano amesikika mkongwe wa CCM, Bw. Kingunge Ngombale-Mwiru alipokuwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mwalimu Nyerere akiikaripia CCM akiitaka ifuate misingi ya azimio la Arusha na mfumo wa CCM aliyoiacha mwalimu Nyerere," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya CUF.

Taarifa hiyo ilisema CCM inajitahidi kuitumia Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kama njia ya kuonesha kwamba wanavijana makini kama vile Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Bw.Ole Millya, aliyewarubuni Watanzania kuhusu uhalisia wa chama hicho.

Ilieleza kuwa tatizo la CCM ni mfumo wa chama hicho unaotengeneza viongozi wanaopatikana kwa fedha na kwa kuzingatia maslahi ya mtu na mtu ama mtandao kwa mtandao na kwamba haiwezi kujirekebisha na kuwa chama cha kuwasaidia Watanzania kuvuka kutoka kwenye umasikini.

"CCM ilizaliwa, ikakua, imezeeka na sasa inaelekea kufa, kwa hiyo CUF inawataadharisha Watanzania kwamba wasije wakadanganyika na vituko vya kauli zinazotolewa na baadhi ya wana CCM kwa lengo la kuhakikisha inabaki madarakani,"ilieleza taarifa hiyo.

10 comments:

  1. Off the point, mimi ninachukizwa na TBC1 kuhusu upotoshwaji wa mambo unaofanywa waziwazi, mifano

    Hivi Lowasa ni waziri mkuu MSTAAFU au waziri mkuu ALIYEJIUZURU?

    Pili hivi tunasherehekea miaka 50 ya UHURU wa TANZANIA BARA au UHURU WA TANGANYIKA?

    Hivi kwanini TBC1 wanapenda kupotosha historia ya nchi yetu? na ni kwa masilahi ya nani?

    ReplyDelete
  2. Hakika naungana na msomaji mwenzangu kuwa Kapiteni Mstaafu wa Jeshi Ndg. Edward Lowasa hakustaafu uwaziri mkuu, alijiuzulu baada ya kuona na kujutia aliyoyafanya yasiyofaa ktk uongozi wake. Hivyo endapo serikali inamchukulia kuwa ni mstaafu wa uwaziri mkuu na kumpa marupurupu yote yanayohusu wastaafu wenye kustaafu kwa utukufu serikalini hakika ni kutuibia sisi walipa kodi wa nchi hii.

    ReplyDelete
  3. Bora watanzania wenzangu mmeliona hilo mm binafsi ninakereka sana ninapoona wanamwita lowasa waziri mkuu aliye staafu wakati wanajua fika kuwa alijiuzulu kutokana na kashfa ya RICHMOND sijui hawa wandishi kama akili zao ziko zawa au wanalipwa sana sana TBC sijui wana maslai gani na huyu bwana KWELI NINAKEREKA SANA NA WANDISHI MUACHE HIYO TABIA

    ReplyDelete
  4. Lowasa is just one big thief who's rightful place should be a jail. End of story!

    ReplyDelete
  5. Designating Lowassa as retired PM indicates is being paid and enjoys all benefits contrary to law. Who gonna question that ccm is everything.

    ReplyDelete
  6. Lowassa ni mdudu mdogo aliyetuwahi kuwa na meno makali tu (Pesa) tena ya wizi lakini anacheza komeddy kuonesha anauchungu na sisi vijana wa Tz na wazee wetu ila hastahili yeye na mapacha wenzake wawili hata kama akitishia vyombo vya habari haisaidii kwani watanzania wote walishamjua ni mwizi hata familia yake wanajua ila wanafurahia kwa sababu wizi huo ndio umewasaidia wana - enjoy maisha bila tabu ila kweli sehemu nzuri ya yeye kukaa ni gerezani afu anaitwa aliyekuwa Waziri Mkuu akajiuzulu kwa taratibu za nchi ni sawa na kufukuzwa kwani hakutoka kwa mapenzai yake ndiyo maana alipojiuzulu alisema ni kutokana na kuonewa wivu kwa uwaziri mkuu wake.

    ReplyDelete
  7. huyo ndio Lowasa, wizi hakuanza leo wala jana toka alipokuwa cda dodoma.na kila wizara aliyokwenda alikuwa haiwachi na mavi.

    ReplyDelete
  8. Dear Brothers and Sisters, Yes Lowassa is the worst person ever you could say in TZ. I tell all today, You must be mads in your minds!! Why can't you see and reason about the source and leaving somebody at the top just doing the wrong things and yet still continuing untill tommorrow. Nobody in TZ who ever happened to be dedicated and loves TZ like Mwl. J.K Nyerere...Do have wht to talk?? Mining Sector, Wildlife, Energy and all alike are corrupted and the source comes frm the top management. Neither CCM nor CHADEMA leaders are real dedicated abt the poverty of this country. Cry before Lord so tht this curse of UFISADI goes away!! Th's it.

    ReplyDelete
  9. Nakuunga mkono Bro! Ni mangapi mazuri Lowassa amewafanyia na leo hamlioni? Mbona viongozi wa Makamishna wa Mikoa na Watendaji Serikalini wanamhara Lowassa alipokua madarakani? Ndio ni FISADI, je mafisadi wa leo waliopo madarakani mmewafanya nini? Jua chanzo cha tatizo, halafu tatua tatizo Watanzania wenzangu!

    ReplyDelete
  10. MMM
    nchi hiii itakuwa inaliwa hadi lini?
    50 yrs 2nazungumzia maji na umeme hatuma la zaidi ??

    ReplyDelete