21 September 2011

Wanazuoni wa Kiislamu waivaa CHADEMA

Rehema Mohamed na Ngaillo Ndatta

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewekwa kitanzini baada ya Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania (HAY-AT) kutoa muda wa
siku tatu kwa viongozi wake wa taifa kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitara yake na kumdhalilisha.

Pia umoja huo umeonya kuwa iwapo CHADEMA hawatafanya hivyo wataandaa maandamano nchi nzima kutangaza chama hicho kuwa adui mkubwa wa dini hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bw. Sherally Sherally alisema kitendo kilichofanywa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA ni udhalilishaji kwa mwanamke wa kiislamu hivyo ni lazima viongozi wake wa juu walaani waliohusika na kuomba radhi.

Tayari watu watatu wakiwamo wabunge wawili wamefikishwa mahakamani mkoani Tabora wakituhumiwa kwa kumshambulia Bi. Kimario na kumwibia simu yake yenye thamani ya sh 400,000. Watuhumiwa hao waliachiwa juzi kwa dhamana hadi Agosti 10, mwaka huu.

Bw. Sherally alisema iwapo chama hicho kitapuuza agizo hilo kwa muda waliowapa umoja huo utapita nchi nzima kutafakari hatua stahiki za kukabiliana na dharau hizo dhidi ya mwanamke.

"Tunalaani na kupinga kwa ukali kabisa kitendo kilichofanywa na wanaodaiwa kuwa ni wafuasi na viongozi wa CHADEMA kumvua hijabu Bi. Kimario na kumuacha bila stara huko Igunga Septemba 15," alisema Bw. Sherally na kuongeza:

"Kitendo hiki kumvua hijabu Bi. Kimario, kumsukasuka na kumtolea maneno yasiyofaa ni kitendo kiovu sana mbele ya Mwenyezi Mungu, Waislam na Watanzania wote wapenda haki na amani na wanaojiheshimu," alisema.

Katika hatua nyingine Bw. Sherally alisema wamesikitishwa na kushitushwa na kukaa kimya kwa asasi za kijamii zinazodai kutetea haki za binadamu na wanawake kwa kutolaani kitendo hicho cha mwanamke mwenzao kudhalilishwa kijinsia.

"Kuendelea kukaa kwao kimya kutatulazimisha kuwaona kuwa wanaafiki na ndumilakuwili," alisema.

18 comments:

  1. msitake kudhalilisha uislam uenda kuna lenu janmbo. uislam sio kuvaa nguo. uislam ni nguzo tano mengine yote to satisfy your needs

    ReplyDelete
  2. BWANA SHERALLY USIFANYE KANA KWAMBA NCHI YETU INAONGOZWA NA .IMANI YA UISILAMU. ACHA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE .NA SIO KUTETEA UISILAM WAKATI MTU ANAPOFANYA MAKOSA.KUMBUKA DC NI SEREKALI HANA CHAMA NA HATAKIWI KUEGEMEA UPANDE WA CHAMA CHOCHOTE TENA TUNAJUA KUWA AMANI YA NCHI YETU IVURUGWA NA NYINYI WENYE ITIKADI KALI. TUMIENI BUSARA ZAIDI KULIKO NGUVU

    ReplyDelete
  3. Bw. Sherally, Acha mamlaka zinazohusika zifanye kazi yake ikiwa ni pamoja na mahakama. Jaribu kutenganisha siasa na masuala ya dini. Acha tafsiri potofu. Unatia chachu nbaya kwa waumini wa kiislamu na hata dini nyingine kuzijengea fikra za tafsiri za ajabu ajabu kwa kila tukio litokeapo. Tafadhali toa mkono wako ili haki ipatikane. Ni vema ukaviamini vyombo vilivyopewa mamlaka kufanya kazi zake kwa maslahi ya Taifa.

    ReplyDelete
  4. Hawa wanazuoni wa kiislamu HAYAT wanaonekana kuwa kuwa mouth speaker ya CCM na kwa mtindo huu wanakosa credibility kwa sisi waislamu wote MAKINI.

    Imagine majuzi kiongozi mkuu wa kampeni wa CCM Igunga Mwigulu Nchemba alishikwa LIVE akifanya uzinzi na mke wa kada mwezanke wa CCM ustaadhi Rashid. Kwa dini yetu ya kiislamu hili ni kosa kubwa sana kuliko la kuvuliwa hijab. Adhabu ya uzinzi ni kupigwa mawe hadi kufa kwa mjibu wa sharia.

    Lakini ajabu hawa HAYAT hadi hii leo hawajatoa tamko lolote lile la kulaani kitendo alichofanya Kiongozi huo mkubwa wa CCM.

    Leo DC amevuliwa mtadao teana ktk harakati za kumkata wakati alipokuwa akitenda uharifu wa kupanga mikakati ya kuiba kura (ambalo pia ni kosa kwa mjibu wa dini yetu), HAYAT wamelishikia bango na kutoa ultimatum.

    Waislamu wenzagu tuwe macho na hawa wanazuoni uchwara na njaa wanaotumika kwa masilahi ya kisiasa vinginevyo waislamu nchi hii tutaendelea kuwa watu wa kutumika kwa malengo ya kisiasa.

    ReplyDelete
  5. Ama kweli CCM wameishiwa sera. Sasa wanababaika na kuanza kuleta udini kwenye uchaguzi. Hivi ni lini hawa majambazi wa CCM wataweza kizisoma alama za nyakati na kukubali kuwa wananchi wamewachoka na wanahitaji mabadiliko?
    Nyie CCM mtuibie, mtudhulumu, mtutese mtudhalalishe na bado mnataka kututawala kwa nguvu? Hilo haliwezekani. Ikibidi tutaifanya nchi isitawalike tena kama nchi za Uarabuni. Nadhani mnachohitaji sasa ni mkon'goto wa nguvu za umma mmetuibia vya kutosha, mmetudhulumu vya kutosha mme tudhalalisha vya kutosha, sasa tunaitaka nchi yetu.
    Inshalah! Mungu yupo.

    ReplyDelete
  6. HAYAT kuvuliwa kilemba huo siyo uislaam, tafuteni jambo jingine la kufanya maandamano kwa hilo bado.Kwanza nyie mnataka kuleta mambo ya udini.Shame upon you.

    ReplyDelete
  7. Bw. Sherally, hii nchi inaendeshwa kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu. unaposema utahamasisha waislamu nchi nzima ili CHADEMA kionekane hakifai hauoni kuwa ni makosa kwa suala hilo kwanilipo mahakamani na mtu yeyote haruhusiwi kuingilia uhuru wa mahakama, kwa nini nyinyi mnauingilia? Uislam ni zaidi ya hijabu. BW. SHERALLY NA WENZAKO MSIKUBALI KUTUMIWA.

    ReplyDelete
  8. Hivi sisi waislamu tumelogwa na nani? tumekuwa tukiwapigia debe CCM kila kukichwa lkn wakipata ulaji hata hawatujui, TUNAFAIDIKA KWA LIPI? Ndg zangu waislamu, mbona kuna mambo mengi yanafanyika hatuongei?

    ReplyDelete
  9. Huyu jamaa ni mpuuzi sana;ina maana kama DC wa Igunga angekuwa mkristo na angedhalilishwa wasingetoa tamko lolote?Kinachofanya watoe tamko ni kwa saabu DC ni mwislam?Acha udini wewe mwendawazimu!

    ReplyDelete
  10. Hawa wattu hawana akili kabisa wao sasa wamakuwa makuwadi wa ccm mbona kuna mambo mengi yanayotendeka na wanayotendendewa na serikali hii ya ccm mbona hata siku moja sijawahi kusikia wakilaani na hata kutoa muda kwa serikali kuomba radhi? iweje leo hii ishu ya hijab ilete kelele kiasi hicho mi naona hawa jamaa wana chuki tu na chadema na wala si kitu kingine.Na naiomba serikali iwe makini sana na mwenendo huu wanaokwenda nao hawa jamaa na cdhani kama ni waislam wote wanaoungana nao mkono ila ni kikundi cha watu wachache chenye maslahi tumbo ndiyo kinachotaka kuleta balaa katika hii nchi.Waislam tumieni hekima na busara za hali ya juu siyo kutoa matamko yasiyo na mashiko na swali je ingekuwa aliyefanyiwa vile ni kiongozi kutoka chadema mngetoa hayo matamko?

    ReplyDelete
  11. Huyu jamaa kakaosa cha kusema,kama anakumbuka vulugu za mwembe chai asikali waliingia na viatu msikitini mbona hakusema mbona hajawatenga,serikali ya ccm imekataa mahakama ya sharia mbona hajaitenga,mbuge wa chadema tundu alichaniwa nguo na asikali musoma mbona hajawatenga,mbunge sakaya alilazwa selo moja na wanaume urambo mbona hajawatenga,inaoneka ww ni mwananchama wa ccm hauna kipya,kaseome shule upya uelewa zaid wa mambo siyo kukurupuka tu

    ReplyDelete
  12. Haya matusi ya kutukana hawa viongozi wa kiisalmu eti hawana kaili, mara wadini mara, wakuwadi wa ccm nk ndio yanaonesha kweli CHADEMA na wale wasio Waislamu walivyokuwa hawatambui uzito wa suala lenyewe! Ina maana wapo tayari kuwatenga Waislamu na kudharau viongozi wake kiasi cha kuwatukana hadharani! Nasikitika sana na maoni ya matusi na upotoshaji! Kuna wengine wanafikia kudai wao ndio wajuzi wa Uislamu kuliko hao mashehe! Kweli mjinga hata ukimtwanga katika kinu bado haelevuki!

    ReplyDelete
  13. Hawa waislam wanafikria nusu kweli, badala yakufikria maendeleo wanategemea JK aigeuze TZ taifa la kiislam.kwanza hijabu kitu gani bwana. utaandamana mwenyewe na wendawazimu wenzako...!!

    ReplyDelete
  14. Hawa si waisilamu. Ni wahuni fulani wanaotumika na CCM. Wanaendekeza njaa yao tu. Hawana mpango. Wewe Sheraly, acha kuleta mzaha hapa wa kutetea maovu ya DC. Kama ni uisilamu sisi ndio waisilamu tusioshabikia na hatutei uhuni. Toka lini ushungi ukawa mojawapo ya ngazi za kiisilamu? Ni aya gani ya Koroani inayosema hivyo. Tafadhali usichanganye mila za Kiarabu na dini ya Kiisilamu. Njaa yako itakufikisha pabaya. Sanasana utaambulia T-shirt, kanga, na elfu kumi ya feki!

    ReplyDelete
  15. Sherally ni tahira anataka kuleta vurugu na kuingiza masuala ya dini kwenye siasa huyu akili zake ni sawasawa na zile za Ponda.Ukiwaweka hawa watu wawili pamoja ni sawa na pipa na mfuniko wake.

    ReplyDelete
  16. Nyie mnaotoa maoni ya kijinga na kujifanya ni waislaam naomba mjue hamuisaidii Chadema bali mnazidi kuamsha hisia za chuki za waislaam.Maana baada ya kutenda kosa badala ya kujutia kosa mnazidi kutukana waislaam.Jueni mnachokifanya ni mauti kwa taifa la tanzania.Wewe unaelinganisha kosa la kuzini na kuvuliwa hijabu mama wa kiislaam tena ukijiita muislam umepotea saana najua sio we sio muislaam ila unajidanganya tu ngoja sasa nikuelimishe Wakati wa mtume saw wayahudi walimvua mama wa kiislam hijabu sokoni.Kwa kosa hilo mtume saw aliamusha jeshi zima la kiislam na likaingia vitani na wayahudi hao kwa kosa hilo.Wazinifu kipindi hicho walikuwepo wengi hakuwahi tokea akawaandalia jeshi sasa usifananishe mambo kiujinga na kibubusa

    ReplyDelete
  17. mchangiaji wa mwisho huna lolote.kama mtume aliagiza jeshi likapigane na wayahudi mwisho wa cku nini kilichotokea/kuna siku hata moja jeshi lake limewai kuwashinda wana wa uyahudi?kukamatwa dc kilemba kikamvuka huko si kuvuliwa mboa inatokea mara nyingi upepo unwavua izo hijabu apo tusemeje?hiyo chuki dhidi ya chadema ni wewe na mpuuzi mwenzio chdm siyo chama cha kidini hakiwezi kubebwa na dini moja ila kwa umoja wetu watz!!!!!

    ReplyDelete
  18. nyie wala nguruwe iko siku mama yako akikosa atavuliwa chupi nadhani mtasherehekea. siwashangai,mmekuja mjini mmejua kutumia internet kutukana watu. sawa lakini hadi leo tabia zenu za kishenzi bado mnazo tu,kunya kwenye rambo na kutupa popote tu,kukojoa kwenye chupa za maji na kutupa popote tu,mji wa Darisalama umeharibiwa na washenzi nyie msiojua baya na zuri. leo chekelea kuvuliwa yule mama hijab yake na kesho utachekelea mama yako kuvuliwa chupi. LAANATULLAAH

    ReplyDelete