*Mkurugenzi awaondoa wana CUF ofisini
*Ni wakati wa kuchukua fomu za kugombea
Na Mwandishi Wetu, Igunga
WAFUASI wa Chama cha Wanachi (CUF) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wanaonesha kuwa na
upinzani mkubwa katika kinyang'anyiro cha kiti cha ubunge wa Jimbo la Igunga wametunishiana misuli kutishiana wakati wakirejesha fomu za wagombea wao kwa ajili ya kuanza kampeni za ugunge wa jimbo hilo.
Hata baada ya kufikia muafaka na kuanza msafara wa kurudisha fomu hizo wafuasi wa vyama hivyo waligongana tena wakati wakirudisha fomu zao kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Jimbo la Igunga, Bw. Protas Magayana aliyelazimika kuwaondoa wafuasi wa CUF waliokuwa wameingia ofisini kwake wakati CHADEMA nao wakiwasilisha fomu.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata hilo, mgombea ubunge kupitia CUF, Bw. Leopold Mahona alidai kuwa ameshangaa kuona vurugu hizo za mashabiki wa vyama akidai wanachama wa chama chake hawawezi kuleta vurugu za kupigana wala kutunishiana misuli.
"Hawa walioleta vurugu ni wageni, hakuna mwananchi wa Igunga anayeweza kunifanyia vurugu wala CHADEMA kwa sababu chama changu ndicho kilipata nafasi ya pili nikiwa mimi mgombea hawa jamaa zetu hawakushiriki,"alisema Bw. Mahona.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Bw. Protace akizungumzia urudishaji wa fomu za wagomea alisema kati ya vyama tisa vilivyochukua fomu za ubunge, ni mmoja tu ambaye hakurudisha fomu zake.
Alisema mgombea ambaye hakurudisha fomu hizo ni Bw. Ndegeye Lazaro wa chama cha UMD ambaye mpaka muda wa mwisho wa kuresha fomu hizo hakuonekana na kudaiwa alikuwa akihaha kutafuta wanachama wa kumdhamini.
Wakati huo huo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Hamad ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Igunga kuacha kuingilia shughuli za uchaguzi katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.
Akizungumza na Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Igunga ambayo Mweenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Bibi Fatuma Kimario, Maalim Seif alisema kamati hiyo ihakikishe kuwa vyombo vya ulinzi na usalama haviingilii uchaguzi huo wala kupendelea chama cha siasa.
Alisema vyama vya siasa viachiwe vijinadi bila kuingiliwa ili atakyechaguliwa kuwa mbunge wa Igunga atokane na kura halali za wananchi wa jimbo la Igunga.
"Siasa ni hisia hivyo wito wangu hasa tusizipe nafasi hisia zetuzisitokee kabisa kama mtasimamia shughuli zenu bila upendeleo hatimaye tutampata mbunge ambaye tunataka achaguliwe kwa taratibu za uwazi kabisa na maamuzi yafanywe na wananchiƔlisema Maalim Seif.
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF alisema wakati mwingine uchaguzi unapomalizika utata unajitokeza wa kujumlisha kura na kutumika nguvu ambazo hazistahili kutumika,wakati mwingine wasimamizi wanapokuja na matokeo yao kutoka kata wanakuta matokeo mengine ambayo hayapo.
Alisema Tanzania nzima inaangalia uchaguzi wa Igunga na kumtaka Mkuu wa wilaya kuwa makini na kuvitaka vyama vya siasa walivyoweka wagombea wa ubunge katika jimbo hilo vifuate ratiba zao bila kuingiliana na kuacha vurugu.
"Ukiona hapa mwenzako yupo na wewe ni zamu yako kufanya mkutano hakuna haja kugombana,tumepangiwa utaratibu wadau wote tufuate, tushirikiane kuondoa kasoro hizo"alisema Maalim Seif.
Katika ziara ya Makamu wa Rais Zanzibar, aliyefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Bw. Abedi Mwinyimsa alipokea taarifa fupi za wilaya ya Igunga na kufanya kikao cha ndani na viongozi wa CUF waliopiga kambi Igunga kabla ya kuanza kampeni za ubunge.
Awali Mkuu wa Wilaya,Bibi Kimario alisema wilaya ya Igunga inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa chakula.
CUF imemsimamisha Bw.Leopold Mahona kugombea kiti cha Ubunge katika jimbo hilo lililoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Bw.Rostam Aziz (CCM) aliyejiuzulu nyadhifa zake katika chama hicho.
Vyama tisa vya siasa vimewasimamisha wagombea,chama cha CHAUSTA kimemsimamisha Bw. Hassan Ramadhani, Bw. Hemed Ramadhani (UPDP),John Magona (SAU),Dkt. Kafumu Dalaly (CCM).Chadema, Bw.Joseph Kashindye,Bw.Steven Mshuyi wa AFP,Bw. Lazaro Ndegeya (UMD) Bw. Said Cheni (DP).Kampeni za uchaguzi huo zinaanza leo katika kata 26 za Jimbo la Igunga mkoani Tabora.
Jimbo la igunga walizoea kupewa rushwa na Mh.Rostam Aziz.Nina toa taarifa kwa wagombea wa vyama vingine viweke pesa kwa ajili kuwapa wapiga kura rushwa.
ReplyDelete