08 September 2011

Serikali yatakiwa kufufua mpira wa kikapu

Na Livinus Feruzi, Bukoba

SERIKALI na wadau katika Manispaa ya Bukoba Mkoa wa Kagera, wameombwa kujenga viwanja vya kutosha vya mpira wa kikapu na kuweka utaratibu wa kufundisha
mchezo huo kuanzia  shule za msingi, ili kufufua mchezo huo.

Ombi hilo limetolewa na mwalimu wa mchezo huo mjini Bukoba Chapelina Gosbert, wakati wa utambulisho wa wanafunzi watatu wa shule za msingi waliochaguliwa kushiriki mafunzo ya mchezo huo yanayomalizika leo, Dar es salaam.

Mwalimu Chapelina alisema ili kufufua mchezo huo, serikali kwa kushikiana na wadau wanatakiwa kujenga viwanja ili hata vijana wakihamasika viwepo viwanja vya kuchezea, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha walimu.

Alisema ukosefu wa viwanja vya mpira wa kikapu ni moja ya sababu zinazochangia watu wengi mkoani Kagera, kutopenda kushiriki mchezo huo ikilinganishwa na ilivyo kwa mpira wa miguu.

Akizungumzia mchezo huo mkoani Kagera na ziara ya wanafunzi hao, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa  Kikapu mkoani Kagera, Idrisa Masalu alisema kuwa na wawakilishi katika mafunzo hayo ni moja ya harakati za kuufufua mchezo huo.

Aliwataka wakazi wa Manispaa ya Bukoba, kujitokeza mara kwa mara kwenye Uwanja wa Zamzam ambao ndiyo pekee mjini hapa kwa ajili ya mazoezi.

Baadhi ya wazazi walioudhuria utambulisho huo, wameishukru ubalozi wa Marekani kwa uamuzi wa kufadhili mafunzo hayo.

Wanafunzi waliopata nafasi ya kuhudhuria kliniki hiyo ambao wanatoka Shule ya Msingi Kashai.

No comments:

Post a Comment