29 September 2011

Waandishi kuanza kufundwa kesho

Na Zahoro Mlanzi

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), imeteua washiriki 40 kwa ajili ya mafunzo ya waandishi wa habari za
michezo yatakayofanyika mkoani Morogoro kuanzia kesho hadi Oktoba 2, 2011.

Washiriki hao wataondoka Dar es Salaam kesho saa 8 mchana kwa usafiri wa pamoja na watarejea Oktoba 2, mwaka huu baada ya mafunzo kufungwa jioni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Amir Mhando alisema
uteuzi huo umezingatia zaidi wale ambao hawakuwahi kushiriki mafunzo yoyote, yaliyoandaliwa na TASWA na pia umezingatia mahitaji ya chombo husika cha habari.

Mhando alisema pia umezingatia mafunzo mengine yatakayofanyika Novemba mwaka huu mkoani Arusha, ambayo yatakuwa na idadi kubwa ya washiriki.

"TASWA inaishukuru Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kuwa mdhamini mkuu wa mafunzo haya, pia kampuni ya mabasi ya Al Saedy kwa kuwa mdhamini mwenza, tunaamini mchango wao ni mkubwa zaidi," alisema Mhando.

Akiyatolea ufafanuzi zaidi mafunzo hayo, alisema yatazingatia masuala ya maadili ya uandishi wa habari, mambo ya uandishi wa makala za michezo na habari za sheria za michezo mbalimbali nchini.

Aliwataja washiriki wa mafunzo hayo na vyombo vyao katika mabano ni Zaituni Kibwana (Bingwa), Olipa Assa (Dimba), Jennifer Ulembo (Mtanzania), Sweetbert Lukonge (Mwananchi), Doris Malyaga (Mwanaspoti) na Suleiman Jongo (The Citizen).

Wengine ni Renatha Msungu (Nipashe), Steve Wills (The Guardian), Maulid Kitenge (Redio One), Jimmy Tara (ITV), Master Tindwa (Capital Redio), Hassan Mvula (Star TV/Redio Free), Alex Luambano (Clouds Media), Mbozi Katala (TBC1), na Shadrack Peter (Chanel Ten).

Pia wapo Sigori Paul (Redio Uhuru), Crecensia Tryphone (Tanzania Daima), Japhet Kazenga (Daily News), Crecence Kunambi (Habari Leo), Adolph Bruno (Majira), Shaaban Mbegu (Spoti starehe), Shaaban Kondo (Times FM), Hamis Shimye (Uhuru), Erasto Stanslaus (Mseto), Ezekiel Kitula (Championi), Selemani Mkangara (Changamoto), Salome Milinga(Jambo Leo) na Anwar Mkama (Mlimani TV).

Wanaotoka Pwani ni Omary Mngindo na Masau Bwire, wakati wa Morogoro ni Nickson Mkilanya, Idda Mushi, Ratifa Ganzel, John Nditi, Abeid Dogoli, Titus Munga, Ramadhan Libenanga, Samuel Msuya, Jimmy Mengele na Lilian Lucas.

No comments:

Post a Comment