22 September 2011

Vijana 26 wajitokeza kushiriki tenisi

Na Addolph Bruno

WATOTO 26 wamejitokeza kushiriki mashindano ya tenisi ya Goldstar ya vijana wenye miaka chini ya 18, yatakayofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa
Gymkhana, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha wa tenisi wa klabu Gymkhana, Salum Mvita, alisema wanatarajia kupata vijana zaidi ya 60 kutoka mikoa mbalimbali kuanzia kesho.

"Mpaka sasa ni vijana 26 waliojitokeza, lakini wengi ni kutoka Dar es Salaam, tunatarajia yatakuwa na mvuto sana," alisema.

Mvita alisema kuwa, kesho wanatarajia kuwapokea vijana wengi kutoka mikoani, wanaokadiliwa kuifikia 60, na kwamba maandalizi ya michuano hiyo yanaendelea kufanyika.

Mashindano ya Goldstar yatashirikisha vijana kuanzia  miaka 18, 14, 12, 10 na nane, ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa na waandaaji.

No comments:

Post a Comment