22 September 2011

Villas-Boas alia na waamuzi

LONDON, England

KOCHA wa Chelsea, Andre Villas-Boas amesema amewasilisha malalamiko katika bodi ya waamuzi wa Ligi Kuu England, kuhusu kiwango kilichooneshwa na maofisa wake
katika mchezo ambao timu yake ilifungwa na  Manchester United.

Villas-Boas alishikwa na hasira Jumapili, baada ya Manchester United kuongoza kwa mabao 2-0 kwa goli ambalo ikirudiwa linaonekana lisingekubalika kutokana na kuwa mfungaji anaoneka alikuwa ameotea.

Kocha huyo wa Chelsea, alisema juzi mbele ya waandishi kwamba ameshawasilisha malalamiko yake kwa Mkuu wa waamuzi, Mike Riley tangu mechi hiyo ilipomalizika kwa ushindi wa mabao 3-1.

"Sikufahishwa sana na kiwango kibovu cha waamuzi, ambacho kilisababisha matokoe mabaya," alisema Villas-Boas. "Unatakiwa kumwamini mwamuzi kufanya kazi yake na nimeshalichukulia hatua kwa kuzungumza na watu sahihi," aliongeza katika mahojiano yake na Reuters.

Mbali na kulalamikia waamuzi, Villas-Boas alikwepa swali aliloulizwa kuhusu kiwango cha Fernando Torres, ambaye alikosa nafasi muhimu ambayo ingefanya matokeo kuwa 3-2, nafasi ambayo inaelezwa inaweza kuwa moja kosakosa mbaya katika historia ya Ligi Kuu, akisema kuwa swali hilo halikua muhimu kwa kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja.

No comments:

Post a Comment