06 September 2011

TFF yaigeuzia kibao Vodacom

*Yataka vielelezo sakata la jezi Yanga

Na Zahoro Mlanzi

SAKATA la Klabu ya Yanga kutovaa jezi zenye nembo nyekundu, limezidi kuchukua sura mpya ambapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sasa limeigeukia
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom na kuitaka iwasilishe vielelezo vinavyoonesha kukubaliana na Yanga.

Yanga tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara, Januari 20 mwaka huu haijavaa jezi zilizotolewa na Vodacom, ambazo kifuani zina nembo ya kampuni hiyo ambayo ndiyo mdhamini mkuu wa ligi hiyo.
Kutokana hilo, Yanga katika michezo yake miwili dhidi ya JKT Ruvu na Moro United, wachezaji wake hawakuvaa jezi hizo za Vodacom, badala yake walivaa zenye nembo ya Kilimanjaro Lager ambao ni wadhamini wao.

Akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu sakati hilo, Ofisa Habari wa shirikisho hilo Boniface Wambura, juzi alisema waliiandikia barua Yanga kuhusu msimamo wa TFF kuhusu ulazima wa kuvaa jezi hizo kama kanuni inavyoeleza.

"Pamoja na Yanga kuiandikia barua hiyo, lakini pia tumewaandikia Vodacom tukitaka watueleze makubaliano waliyofikia kati yao na klabu hiyo kwa maandishi ndipo tutakapojua la kufanya," alisema Wambura.
Alisema Yanga ilijieleza juu ya hilo na kutoa sababu ambazo hazina msingi kwani Ligi Kuu Bara inaongozwa na kanuni, hivyo haina budi kuzifuata, kwa kuwa Yanga ikikubaliwa, timu nyingine zinaweza kuomba rangi wanazotaka.

Wambura alisema kama yapo makubaliano mengine yaliyofikiwa tofauti na kanuni zinavyoelekeza, Vodacom ndiyo wanaotakiwa waoneshe ni makubaliano ya aina gani waliyofikia.
Wiki iliyopita viongozi wa Yanga, walithibitisha kwamba timu hiyo ilishakubaliana na Vodacom kwamba watavaa jezi zenye nembo nyeusi.

Baada ya taarifa hizo, TFF ilisema  kinachotakiwa ni Yanga kukubali hali iliyopo na ikizingatiwa kwamba mkataba wa Vodacom unamalizika msimu huu.
Alisema ni bora kuendelea na msimamo kama kanuni inavyoagiza kuliko kutoka nje ya kanuni kwani kunaweza kuleta matatizo makubwa.

6 comments:

  1. Yanga wachumba tu hao. Mnasingizia mnafungwa kwa sababu ya rangi nyekundu. Teehe!tehe!tehe.
    Mtasingizia sana mwaka huu. Maana sasa mnaelekea kuanza kuruka 'running track' nyekendu ya uwanja wa Taifa kwa kuwa tu ni nyekundu.
    Hoooovyo!

    ReplyDelete
  2. hahahaha wataweza kuziruka hizo running track?Yebo ni Yebo tu hatawakiwekewa rangi ya mawingu kichapo kipo pale pale

    ReplyDelete
  3. Pambafu walahi! wamenasa hao hawana ujanja kwani rangi ndiyo inayocheza? wasitafute mchawi wao ndio wachawi.wasilete mambo ya vijiweni kwenye masuala ya Msingi. TFF kuweni wakali kwenye mabo kama haya, Umbumbumbu wa Viongozi wa yanga usiwafanye ninyi pia mkaonekana hamnazo. Yanga acheni Ufinyu wa Mawazo Vaeni Jezi za Wadhamini hiyo ndiyo nembo yao Nyekundu sasa mnataka Black & White?

    ReplyDelete
  4. Du hiyo nayo ishakuwa sooo, hawaoni wenzao ulaya? mambo ya Rangi siyo issue, wao wanachotaka Mdhamini wao anatekeleza kinachotakiwa. Ushamba tu wa Viongozi wa Yanga. Yanga kama Yanga haina tatizo hata wakivaa Jezi za ajabu itabakia kuwa Yanga. Mdhamini nembo yake ni Nyekundu na Nyeupe sasa wewe kwakuwa mjinga sana na Juha unataka Nyeusi Timu ya Babako hiyo? TFF wembe kama kazi unanyoa kama hauna akili nzuri, wanyoeni hao mnasubiri nini?

    ReplyDelete
  5. YANGA inatutia aibu!! hata Jezi tu na Mambo ya uchawi yataingizwa. ACHENI USHAMBA YANGA. Kweli ni YEBO YeBO !!

    ReplyDelete
  6. sasa nina imani kuna timu nyingine itaibuka na kudai matakwa yake hapo. Tuone hao Vodacom watakavyojikanyaga kanyaga, maana washajirahisisha kwa Yanga. Hongera TFF kwa kuonesha uimara

    ReplyDelete