Na Salim Nyomolelo
MWENYEKITI wa Mtandao wa Asasi za watu waoishio na Virusi vya UKIMWI Tanzania (TANOPHA) Bw. Julius Kahaya, amesema dawa inayotolewa na
Mchungaji Ambilikile Mwasapile, wa Loliondo haitibu magonjwa sugu ikiwemo UKIMWI kama inavyodaiwa.
Akizungumza na Majira Ofisini kwake jana, Mwenyekiti huyo alisema dawa ya Mchungaji huyo mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) maarufu kama Babu wa Loliondo inapotosha watanzania.
Alisema yeye na wenzake 13 walikwenda kwa babu kama watu wanaoishi na Virus vya UKIMWI (VVU) na kufanikiwa kupata dawa na kuambiwa kupima kwa awamu tatu baadaye.
Alisema baada ya kupima mara tatu kama walivyoambiwa baada ya siku saba, siku 21 na miezi mitatu bado wameonekana kuwa na virusi hivyo.
Alisema Babu huyo hakuoteshwa na Mungu kwa kuwa dawa ya mungu inatibu kwa muda huohuo baada ya kuitumia.
"Babu ni muongo lakini uongo wake ni wa kitaalamu,inawezekana ameshirikiana na wakubwa serikalini",alidai Bw.Kahaya.
Alisema idadi kubwa ya watanzania wanaoishi na VVU waliacha kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARVs) na kuacha kuzingatia ushauri uliokuwa ukitolewa kwenye vituo vya afya baada ya tiba hiyo.
"Nasena Babu ana mbinu za Kigangakiganga tu, mimi simchukii lakini nayachukia madhara yaliyotokana na babu," alisema.
Alidai anasikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu kupoteza maisha baada ya kuacha kutumia ARVs huku wakiwa na matumaini ya dawa ya babu.
Kuhusu imani alisema kwa mazingira ya Loliondo ambapo kulikuwa na msongamano mkubwa wa watu kutoka nchi mbalimbali huku helkopta angani zikipishana ni lazima mtu ujawe na imani hata kama huna.
"Serikali ina kazi kubwa ya kuwarudisha watu wanaoishi na virus vya UKIMWI kuendelea kupata huduma katika vituo vya afya," alisema.
Babu huyu ni mjanja. Ameona maisha yanamwendea kombo aka amua abuni mbinu ya kujikwamua ili apambane na maisha ya kustaafu. Kiukweli wengi waliokwenda loliondo kwa magonjwa sugu wakitumaini kupona wameendelea kulazwa na wengine kufariki kabisa. Waliostuka mapema walirudi kumeza dawa zao za hospitalini.Pole kwa wale waliouza shamba, nyumba na mali zao walizozitafuta kwa jasho jingi ili kupata nauli ya kwenda Loliondo.
ReplyDeletemimi nimepona kabisa we kahaya huna imani na mungu
ReplyDeleteMimi, mtoto wangu, dada yangu na ndugu zetu walioenda Loliondo wamepona magonjwa kama ukimwi, kisukari, na pressure. Lazima niseme hivyo kwa sababu sasa hivi situmii tena dawa za kisukari, nilifuata maelekezo na nilipokuwa naenda huko nilikuwa natumia dawa zangu za hospitalini sikuziacha hadi nilipopima kama alivyoagiza na wote tuna afya njema Asante Yesu na Mungu azidi kutubariki.
ReplyDeleteMimi sisemi kitu kwasababu hamna hata mmjo akienda kupima anamchukua mwenzake kwa uhakikisho ila utasikia nimepima nipo mzima.
ReplyDeletekumbuka babu aliwatahadharisha wale wote ambao wamezoe rushwa hawatapona- kuna watu milikuwa mnohnga ili mfike loliondo mapema kupata kikombo - hakika hamtapona - ile dawa ni ya kiimimani - watch out!!!
ReplyDeleteNjia ya tapeli ni fupi. Tunaweza kujua ukweli wa kikombe cha Babu iwapo tutafanya kama ifuatavyo:
ReplyDelete1. Wapatikane (volunteers) 75 wenye ugonjwa wa Ukimwi (25), Kisukari (diabetics) (25)na Presha (hypertension)(25).
2.Vituo maarufu vya televisheni nchini visimamie zoezi hili na kulitangaza moja kwa moja. Tunaweza kufanya harambee kuchangia zoezi zima.
3. Wagonjwa hao wapimwe katika Zahanati maarufu nchini ili kuthibitisha ukweli wa maradhi yanayowasumbua.
4.Wagonjwa hao wasafirishwe hadi kwa Babu ili kupatiwa Kikombe cha dawa.
5. Mara baada ya kunywa kikombe hicho wapimwe tena katika Zahanati 3 tofauti katika muda maalum, tuseme every 3 weeks. Tunaweza kurejea zoezi hilo kwa mara tatu.
6. Kila kundi litowe individual results na kuona asilimia ngapi katika kila kundi limepata mabadiliko ya kupona.
7. Iwapo imepatikana atleast 30% ya kupona,then tunaweza kutangaza uwezo wa kuponesha wa dawa hii. Inawezekana kundi moja likatoa matokeo mazuri kuliko jengine, hio pia itakua ni habari yenye matumaini. Serikali iunde chombo maalum na kukipatia fedha ili kuboresha na kumsaidia Babu katika zoezi lake la utibabu na utafiti.
8. Iwapo hakuna effect yoyote katika kila kundi, hapana shaka Serikali italazimika kumpiga marufuku Babu kwa kudang'anya wananchi na ihakikishe amri yake inatekelezwa ipasavyo.
Kumbuka kama suala linahusu imani ukiliwekea hayo masharti ya control hupati kitu
ReplyDeletehayo masharti ya control hupati kitu
ndugu alieyetangulia ametoa wazo zuri. Hapa tunataka kuwalinda wananchi wasitapeliwe. Kuna tatizo gani kwa wagonjwa kufata masharti ambayo tumesoma yapo wazi na yanatekelezeka. Serikali lazima ioneshe uwezo wake wa kuwapigania wananchi
ReplyDeleteHizo habari za mimi na dada zangu wamepona ni uzushi tu, na inaonekana dhahiri yakua hao wote wanashirikiana na wajanja na huyo babu mbona sasa hakuna fujo ya kwenda kwa babu,huyo mtaalamu amenena kweli kabisa na sio kabisa kumdharau, na kama huamini basi nenda ukafie huko.
ReplyDeleteNaamini kuwa tunaingiza suala la Mungu na Imani, ili upone lazima uwe na Imani wewe kama wewe, Hata Yesu alipokuwa anawaponya watu aliwaambia imani yako imekuponya, hata sasa wewe ukiamnini kuwa Mungu anaweza kuponya ugonjwa ulio nao utapona tu, ni kweli kabisa watu wamepona tumewaona walikuwa na kisukali sasa wanakula na kunywa vyakula walivyo katazwa, ila Kahaya kumbuka Babu alitoa tahadhali kwa waathirika wa VVU, wasije wakasema wamepona wakaanza ngono zembe,no wasifanye,na wafuate masharti, sasa nyinyi kama mlienda kumjaribu basi mjue Mungu hajaribiwi, Hakuna ujanja hapo
ReplyDeletewehu na wajinga katika karne ya 21 wataamini mtu kuoteshwa na Mungu. mlipoambiwa mkasema Ukiristo unapigwa vita,amkeni nyie dunia ya tatu sijui ya mia huko,hivi wewe na akili zako haswa nikuambie nimeoteshwa na Mungu ukakubali? nitakuona kichaa
ReplyDeleteDini yoyote inayopingana na sayansi haina nafasi ktk dunia ya leo. Hakuna kipimo cha kupimia imani. Lakini sayansi inayo vipimo vya kupima uwezo wa mzizi wa Babu ktk kuponesha mwanadamu. Hatuna ugomvi na imani za kidini, lakini tunajali afya za watu wetu. Hatutaki kuona wajanja wachache wanachezea maisha yetu. Nakubaliana na alieshauri uwepo utafiti huru na ulio wazi utakaoweza kupima uwezo wa kikombe cha Babu.
ReplyDeleteMOST OF THE PEOLE DIES ONCE OR FEW MONTH AFTER RETURN TO BABU LOLIONDO.WHAT I CAN SAY THERE IS NO TRUE TREATMENT
ReplyDeleteHebu tuelimisheni. Nimeona dawa ya Babu kupitia kipindi maalum kilichotayarishwa na NTV,Nairobi. Umati mkubwa wa watu na foleni ya magari zaidi ya 2,000 yakielekea kwa Babu. Tokea kutangazwa kwa uwezo wa dawa hii, mamilioni tayari wameshakunya dawa hii na wengine bado wanaendelea kufurika. Tunasikia baadhi ya watu (wasiozidi 1,000) wamekufa au kudhuriwa na kikombe hiki. Ikiwa takwimu hizi ni sahihi, wahusika wachukue hatua mwafaka na watoe taarifa rasmi haraka iwezekanavo.
ReplyDeleteimani ni kitu cha thamani sana, tunaenda makanisani na misikitini kwa imani ya kwamba siku nikifa mungu anaipokee katika ufalme wake, nani anauhakika kama siku ya kiama ntapokelewa? IMANI tu, kata kikombe cha babu ni imani, ukiumwa na ukapewa maji ya kunywa ya bomba na ukayanywa kwa imani, kwamba mungu naomba uyafanye haya maji kama dawa, HAKIKA UTAPONA. lakini kama huna imani, ah hata ungefanyaje, Ng'o. MUNGU ATUSAIDIYE SANA. si ukimwi tu, mbona aliyetapita nyoka baada ya kunywa kikombe hamsemi? mbona mkenya aliibiwa simu na aliye iba akapigwa upofu, na alipoludisha, hali yake ililejea kama kawaida.
ReplyDeleteKuna wakati tunasema "Time will Tell) Lakini kwa sasa ni wakati timilifu. Tusijitahidi kukingia kifuajambo lililo wazi. Kubali utafiti uliopendekezwa kama bado hujabadili mawazo. Karne ya21 waafrika bado wanacheza na ushirikina badala ya taarifa za kisayansi. Ukishajihulisha na na maswala ya umma (public issues) kubali bia kufanyiwa utafiti. utafiti utatutoa gizani watanzania wote
ReplyDeleteVyombo vya habari vina nafasi nzuri iwapo vitafanya kama ilivopendekezwa. Utafiti uliowazi ufanyike tupate ukweli wa dawa hii. Masharti yake sio magumu:
ReplyDeleteKuweka IMANI
KUNYWA kikombe cha dawa
Matokeo ya uponyaji hayahitaji muda mrefu. Sio masharti magumu kwa wale wanaosumbuliwa. Tuacheni tabia ya kufata matukio (Reactive).
Tubadilike. Vyombo vya habari kuweni wabunifu na Pro-active.
Niwajibu wa serekali ya Tanzania na Wizara ya Afya kuingilia kati zoezi hili tusingoje janga hilo la waganga wakienyeji,mie naona hakuna siri kama ukweli utafanyiwa kazi na iwe faida kwa ote duniani,poleni waumini wa kuacha njia za kweli .Chuo cha waganga Muhimbili kinafanya nini?
ReplyDeleteNi vizuri kufanya utafiti wa kina kuhusu idadi ya watu waliopata kikombe cha babu, waliopona na ambao tiba haijawasaidia kabisa. Yatupasa kuepuka kauli za jumla jumla.
ReplyDeleteJamami mimi kuna watu nimewaona kwa macho yangu wamekwenda huko kwa babu kwa maradhi ya miguu wamerudi na sasa wamepona kabisa.
ReplyDeleteTukikumbuka wale wagonjwa wa mwanzo kabisa walitoa ushuhuda wao kuwa wamepona UKIMWI na baadhi ya madaktari walidhibitisha hayo.
NANI KAKULAZIMISHA KUNYWA DAWA? KAMA HAUTAKI WEWE ACHA KWANI KILA MTU NA IMANI YAKE NA NAFSI YAKE.PILI PILI USIYOKULA KWANINI INA KUWASHA?ACHENI PLOPAGANDA ZENU.
ReplyDeleteBabu hakujitangaza kutibu maradhi! Msimshambulie na kumwita tapeli! Alipewa maono usingizini na maelekezo nini afanye, waliokunywa kikombe chake wakapona ndio waliomtangaza, na pia kwanza uwe na imani kubwa juu ya hilo, si kumshambulia tu babu wa watu kawakosea nini?! we utafute ukimwi wako hukoo, ikesha uende kwa babu tu sababu eti umesikia ana dawa, utapona vipi wakati lengo lako ni kuwakomoa wote walio kunyanyapaa? Pole Kaaya, ya Mungu ni mengi labda uliandikiwa utakufanao
ReplyDelete