Na Zahoro Mlanzi
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeanza kuikunia kichwa Morocco kwa kuanza kuiandalia mikakati ya kuhakikisha timu ya Taifa 'Taifa Stars', inaifunga
timu hiyo katika mchezo wa mwisho wa Kundi D.
Mbali na hilo, shirikisho hilo limeanza kufanya mawasiliano na Chama cha Mpira wa Miguu Morocco, kujua tarehe maalumu watakayocheza kati ya Oktoba 7, 8 na 9, mwaka huu ili kuanza taratibu za safari.
Timu hizo zitakutana kati ya siku hizo kuwania kucheza fainali za Mataifa ya Afrika (CAN 2012), zitakazofanyika katika nchi za Guinea ya Ikweta na Gabon.
Katika kundi hilo, Stars na Algeria zina pointi tano na Afrika ya Kati na Morocco zinaongoza kundi hilo zikiwa na pointi nane, hivyo michezo ya mwisho ndiyo itakayotoa timu zitakazocheza fainali hizo.
Akijibu swali Dar es Salaam jana, baada ya kuulizwa shirikisho limeanza mikakati ya kuiandaa timu kuhakikisha inashinda mchezo wa mwisho, Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura, alisema tayari wameanza na wanachosubiri ni Kocha Mkuu, Jan Poulsen kuwasilisha programu zake kwa ajili ya mchezo huo.
"Unajua Poulsen alikata tamaa baada ya kupata matokeo yale (bao 1-1 dhidi ya Algeria) na kusema, hawana nafasi tena ya kufuzu, lakini baada ya Afrika ya Kati na Morocco kutoka suluhu, ni dhahiri tuna nafasi ya kufuzu kama tutashinda mchezo wa mwisho," alisema Wambura na kuongeza;
"Na tayari alianza kujiandaa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Chad wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, lakini hivi sasa ameelekeza nguvu zake katika mchezo huo," alisema.
Alisema mwezi huu pia kuna mechi zile za FIFA date (mechi maalum za kujipima zinazoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu), hivyo watahakikisha wanapata timu ambayo inawiana kiuchezaji na Morocco.
Mbali na hilo, alisema wakijua siku ambayo watacheza na Morocco itakuwa rahisi kwao kuandaa safari na kujua idadi ya watu watakaokwenda, kwani usafiri wa nchi zilizo Kaskazini mwa Afrika unasumbua.
Hao TFF hawana mpango wowote wao ndio walio changia kuifikisha stars pabaya wanachojali wao kukusanya mapato ya mechi basi. Nashangaa kuona watu wanawalaumu wachezaji kwa matekeo wanayoyapata kweli ulimwengu wa leo wa soka utegemee kushinda mechi ya ushindani bila maandalizi? TFF kazi yao kuipangia timu ya taifa mechi hewa za majaribio kazi kupiga siasa tu mara oo! hatukuwa na ticket za kuisafirisha timu,mara nyengine oo! yanga imekataa wachezaji wake bado wamelala katika usingizi wa 1950 na kurudi nyuma, wazee wamesema nguo ya ijumaa haifuliwi alhamis kuamkia ijumaa bali inapomalizika ijumaa tu matayarisho ya ijumaa nyengine inaanza wao kazi yao kupiga domo tu. watoto wanastahili pongezi hasa katika mechi ya mwisho na algeria ikumbukwe algeria wanapenda mechi za ushindani na wanazimudu walikuwa hawana wasiwasi wala shaka kwamba wataifunga taifa star lakini walichokiona hawakuamini macho yao.kama ningekuwa na uwezo ningetimuwa TFF nzima kabla mechi ya mwisho hawa ndio wanazoretesha maendeleo ya soka si kwa vilabu si timu ya taifa wapumbavu wakubwa hawa.
ReplyDeleteLugha za kiistaarabu zinatakiwa katika kutoa maoni, inashangaza mtu anatoa kauli za kutukana je ndio utanzania tulionao na kulelewa nao? Inasikitisha sana. Ustaarabu katika kutoa maoni ni mzuri kuliko kitu chochote, mbona hukuchaguliwa wewe ukaongoze hiyo TFF, siio vizuri kutukana, toa maoni kwa lugha nzuri na ya kiistaarabu. Naitakia kila la akheri timu yetu ya Taifa Mungu ibariki nchi yetu na watu wake pia.
ReplyDeleteMatayarisho mabovu ndio matatizo ya timu zetu.Wenzetu wanajua kuandaa timu zao mpaka kuweka kambi hata ulaya.Lakini sisi tumebakia na maneno mengi tu.Vilevile unaangali timu unayocheza nayo na kujipangia ni timu ipi inafaa kwa ajili ya maandalizi.Nikisema hivi nina maana ya kuwa kwa mfano unacheza na Egypt alafu unakwenda kujipima nguvu na Palestina.Huku ni kupoteza wakati na pesa pia.Kila siku tunarudia makosa yaleyale.
ReplyDelete