08 September 2011

TBS yakanusha uzushi wa kwenye mtandao

Na Rehema Mohamed

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS)limekanusha taarifa zinazosambazwa katika mtandao kuwa kuna maji ya kunywa aina ya 'Dew' yanayozalishwa nchini ambayo
yaliingizwa nchini Nigeria na kusababisha vifo kwa watumiaji.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TBS Bw.Charles Ekelege, alisema taarifa hizo ni za uzushi, hazina ukweli wowote kwa kuwa hakuna maji ya aina hiyo yanayozalishwa hapa nchini.

Bw.Ekelege alisema taarifa za maji hayo walizipata kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini Zambia tangu Julai mwaka huu na kuanza kufuatilia ukweli wake.

Alisema katika kipindi hicho waliwasiliana na Mashirika ya Viwango ya Afrika Mashariki (EAC) na Nchi za Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili  ambayo yalithibitisha kutoona maji ya aina hiyo.

"Pamoja na mashrika hayo pia Shirika la Viwango la Nigeria tuliwasiliana nao kujua ukweli kuhusu maji hayo yaliyouzwa kwenye soko lao, lakini nao walikanusha vikali,jitihada hizi tulizozifanya zinatufanya tuamini kwamba taarifa hizi ni za kizushina, uongo mtupu zinazolenga kuchafua biashara ya Tanzania kimataifa,"alisema Bw.Ekelege

Alisema serikali inajipanga  kutumia njia za kiintelegensia kubaini chanzo cha taarifa hizo zilizosheheni uzuhi na uongo.

Alisema TBS  inashauri wananchi na umma kwa ujumla waendelee kunywa maji ambayo ubora wake umethibitishwa na shirika lake. Alisema nchini kuna maji yanayozalishwa na kampuni 48.

No comments:

Post a Comment