08 September 2011

Marekani yatoa sh.bil 1.1 kuendeleza Kilwa

Na Godfrey Ismaely

UBALOZI wa Marekani nchini kupitia Kitengo cha Mambo ya Kale (WMF) na Idara ya mambo ya Utamaduni katika ubalozi huo (AFCP),umejitolea kudhamini
utunzaji wa mji wa Kilwa Kisiwani kwa kutoa zaidi ya dola za Marekani milioni 700,000 (sh. bilioni 1,132,000).

Udhamini huo ulitangazwa Dar es Salaam jana na Mkurugezi Mipango wa Mambo ya Kale Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw.Stephen Battle, wakati  akizungumza na waandishi wa habari.

"Ni jambo jema kutangaza mbele yenu kuwa Tanzania ni moja wapo ya nchi tatu duniani, kati ya nchi zote ambayo mwaka 2011 imepatiwa ufadhili mkubwa kwa ajili ya kuhifadhi na kutunza mambo ya kale hususan katika mji wa Kilwa Kusini," alisema na kuongeza;

"Nchi nyingine ni India na Jordan tunaamini mara baada ya kukamilisha taratibu zote za uhifadhi na usimamizi bora, utakuwepo pia misingi ya sheria itazingatiwa ili kutunza maeneo hayo, kwa kuwa watu wa Marekani wanaamini kuwa utunzani wa mji wa Kilwa Kisiwani utakuwa na maslahi makubwa kwa umma," alisema Bw. Battle.

Aliongeza kuwa kupitia mpango huo wa kuhifadhi uasilia na kumbukumbu mbalimbali za kale katika mji wa Kilwa Kisiwani utasaidia kuvutia watalii  kutoka ndani na nje ya Afrika, hivyo kuliongezea taifa pato .

"Kupitia mradi wa kujitolea kutunza mji huu ambao una historia ndefu Afrika ya Mashariki na hata duniani tutahakikisha kingo za bahari ya Hindi ambazo zinamomonyoka mara kwa mara na kuharibu uasili wa mji zinafanyiwa matengenezo," alisema.

No comments:

Post a Comment