06 September 2011

Taarifa za Wikileaks ni uzushi-Ikulu

Na Grace Michael

OFISI ya Rais (IKULU) imekanusha madai yaliyoandikwa katika mtandao wa kimataifa wa Wikileaks ya kuwa Rais Jakaya Kikwete, aliwahi kununuliwa suti tano na
mmiliki wa Hoteli ya zamani ya Kempinski Kilimanjaro na kueleza kuwa ni za kumchafua kiongozi huyo.

Taarifa hiyo inanayotokana na ripoti ya aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Bw. Michael Retzer, pamoja na mambo mengine pia inadai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichangiwa dola za marekani milioni moja katika uchaguzi wa mwaka 2005.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salvator Rweyemamu, alisema habari hizo si za kweli kwa kuwa zimejaa uongo na viashiria vinavyolenga kuchafua jina la Rais na Taifa.

“Ni jambo la kusikitisha na la kukatisha tamaa kuwa balozi mwenye heshima kiasi hiki
anaweza kushiriki katika uzushi wa aina hii hii.

...kurugenzi inasema kwa uwazi kuwa
rais hajapokea zawadi kutoka kwa Bw. Ali Albwardy na kama kuna ushahidi basi
utolewe hadharani,” alisema Bw. Rweyemamu.

Alisema Rais Kikwete hajawahi kusafirishwa na mtu yoyote kwenda London akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na badala yake safari zake zote ziligharamiwa na serikali.

“Suala la CCM kuchangiwa dola milioni moja, rais hakuwahi kuchangisha fedha za kampeni kwa kuwa si kazi ya mgombea, lakini hata kwenye orodha ya waliochangia kampeni hiyo Kempinski Kilimanjaro haikuwemo na wala haijaombwa kuchangia,” alisema.

Akizungumzia uamuzi wa Kempinski kununua hoteli ya Kilimanjaro na ruhusa ya kujenga
hoteli nyingine mbili mpya katika eneo la Ngorongoro Crater na Hifadhi ya Serengeti,
Bw. Rweyemamu alisema maamuzi hayo yalifanyika katika awamu ya tatu.

“Rais huyu huyu ambaye wanadai alihongwa suti lakini ndiye aliyekataa kujengwa kwa hoteli katika eneo la Ngorongoro kwa sababu ya mazingira, rais hajawahi kutembelea hoteli hiyo binafsi isipokuwa amefanya hivyo kwa shughuli za kazi,” alisema.

Alisema Ofisi ya rais imesikitishwa na tabia ya kupakazia kiongozi huyo na kwamba wahusika wanalenga kuichafua Tanzania kwa ujumla.

Meneja na Mkurugenzi wa Habari wa hoteli hiyo Bw. Lisa Pile ambaye alidaiwa kumwambia maneno hayo balozi huyo, alikanusha suala hilo.

10 comments:

  1. Hakika haya ni maskandali yana bashasha zake katika siasa.

    ReplyDelete
  2. Wikileaks haisemi uwongo. Aibu kubwa hii.

    ReplyDelete
  3. kama ni uongo basi wachukue hatua na sii kulalamika tu ! Nchi hii ni ya malalamiko kuanzia juu hadi chini nani sasa wakuchukua hatua?

    ReplyDelete
  4. HIVI WANATAKA NINI KUMCHAFUA KIONGOZI WETU BILA SABABU? UKWELI UNAWEZEKANA UKAWEPO KWA NJIA MOJA AU NYINGINE HAWEZI MTU AKAZUSHA TUU!!NA HUYO AFISA HABARI LAZIMA AKANUSHE YUPO KIKAZI NA KASHFA INAMHUSU RAISI WA NCHI HATA KAMA NI WEWE UNATEGEMEA NINI? HUWEZI KUKUBALI NGOJA AONDOKE HAPA NCHINI KAMA HAJAKIRI.IFATILIWE IKIBAINIKA NI UZUSHI WAHUSIKA WACHUKULIWE HATUWA ZA KISHERIA, KWA NINI JAMBO KUBWA KAMA HILI LIACHWE HIVIHIVI? HUU MTANDAO UNA HAKI GANI KISHERIA KUKASHIFU WATU UKAACHWA HIVIHIVI? NA KAMA HAUJACHUKULIWA HATUWA BASI KUNA UKWELI NDANI YAKE!!

    ReplyDelete
  5. Utetezi wa kurugenzi ya mawasilio ni dhaifu sana. Kwa wale ambao wamesoma habari hii kwenye Wikileaks, watalkubaliana kwamba, wikileaks haina uhasama wala na Kikwete wala na CCM ili kuichafua. Mtandao huu umetua nyaraka nyingi sana na viongozi mbalimbali wa dunia ambao imegundulika kuwa ni ukweli mtupu. Kwamba uamuzi wa kuizua K'njaro hotel kwa Kempiski ni wamu ya tatu hata wikileaks wmesema hivyo ila ushawishi wa Kikwete ulikuapo kutokana na kununuliwa suti 5. Nchi nyingine TAKUKURU ingeanzisha uchunguzi wa kufatilia risiti za hizo suti hapa kwetu ni kuteteana tu

    ReplyDelete
  6. Kwani ni ripoti ipi ya siri iliovuja ya wiki leaks ilikubalika? kila ripoti imepingwa, imelaaniwa, imesingiziwa uzushi lakini Mimi binafsi nina iamini wiki leaks na repoti zake! Hizi ni ripoti za siri za US ambazo hazikukusudiwa kuwarejea mwahusika! na hii ni matokeo ya kazi ya umbea wa wikileaks, thanks to Assange! Na kama mjuavyo umbea ni tofauti na uongo! Umbea ni pure truth ambayo ikimrejea muhusika humuuma sana!

    ReplyDelete
  7. Huyo ndiye na Urais wake. Ana kashfa lukuki - ni pamoja na ile ya kutolewa mtandaoni na mzee wa Utamu

    ReplyDelete
  8. uuuwiiiiiiiiiiiiiiii.

    ReplyDelete
  9. haahahaa..huo ni ukweli...kipi ambacho hakiwezekani Tanzania kuanzia juu mpaka chini...

    ReplyDelete
  10. Hivi Wewe Mtanzania mwenye akili timamu unaweza kuamini rais kuhongwa suti,ama kweli masikini hawa watz wanadhihirisha upumbavu wao mbele ya dunia. Hivi Mmarekani akikuambia mama yako alikuwa malaya na hata wewe wewe si mtoto halali wa baba yako utamuamini. NI NCHI ILIYOJAA MAJINGA MATUPU HATA WAKISOMA WANAFELI NA KWENDA KUFOJI MAVETI

    ReplyDelete