*CUF watinga kamili kunyakua jimbo
Na Mwandishi Wetu
KATIBU wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Nape Nnauye, amewatemea cheche wapinzani wa
chama chake wanaotarajia kushiriki kinyang'anyiro cha ubunge Jimbo la Igunga, kutambua kuwa wananchi wa eneo hilo wanahitaji jibu la matatizo yao na siyo vitisho vya kisiasa.
Mwanasiasa huyo ametoa kauli hiyo siku chache baada ya chama mojawapo kinachoshiriki uchaguzi huo kutishia kumlipua Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, anayetarajia kuongoza CCM katika uzinduzi wa kampeni zake.
Akizungumza na Majira kwa njia ya simu kutoka Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma jana, Bw. Nnauye alisema amesikitishwa na baadhi ya vyama vya siasa kutanguliza vitisho kwa baadhi ya viongozi badala ya kutanguliza jinsi ya kutatua kero za wananchi wa Igunga.
"Nimesikitika sana baadhi ya vyama wanatanguliza vitisho kwa viongozi wetu, wana Igunga wanataka majibu kwa matatizo yao siyo vitisho dhidi ya Rais Mstaafu Mkapa (Benjamin), wanafanya hivyo kwa kuwa hawana sera, imekula kwao,"alisema Bw. Nnauye.
Wakati huohuo leo ndio siku ya mwisho kwa wagombea wa vyama mbalimbali wanaotarajia kuwania kiti hicho cha ubunge kurudisha fomu zao kuthibitisha ushiriki wao, anaripoti Peter Mwenda, kutoka Igunga.
Hadi jana jumla ya vyama tisa vya siasa vilijitokeza rasmi kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge kupitia uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Octoba 2 mwaka huu.
Akizungumza na Majira jana Msimamizi wa uchaguzi huo Bw. Protase Magayane, alitaja vyama hivyo kuwa ni CCM, CUF, CHADEMA, UPDP,DP,Sauti ya Umma,UMD,AFP na CHAUSTA.
Kwa upande wake CUF, jana waliamua kufanya tukio la tathmini ya awali kwa kusafisha mji kwa kuwasalimia wakazi wa mjini hapa baada ya kuwasili katika jimbo hilo kabla ya kufanya kapeni rasmi.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Bw.Julius Mtatiro, ingawa uchanguzi huo unaonyesha dalili ya ushindani mkali lakini kwao wanachojua ni kunyakua jimbo hilo.
Tayari msafara wa viongozi waadamizi wakiwemo baadhi ya wabunge wa chama hicho waliwasili mjini Igunga jana kwa ajili ya kampeni rasmi katika mitaa mbalimbali.
NAPE NI MTU WA AJABU SANA YAANI HATAKI WAPINZANI WAWEKE RECORD ZAO ZA UBADHIRIFU HADHARANI WALIOUFANYA WALIPOKUWA MADARAKANI, SORRY NAPE HIYO NI RECORD ZA VIONGOZI WAKO LAZIMA ZIWEKWE HADHARANI KWANI ZILICHANGIA KWA KIASI KIKUBWA KWA WANANCHI WA IGUNGA KUKOSA MAJI, UMEME, BARABARA NA WATOTO WAO KUSOMEA CHINI YA MITI.
ReplyDelete