Na Grace Ndossa
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt. John Ndunguru, amesema Wizara hiyo inatarajia kujenga daraja katika Mto Kilombero ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.Dkt. Ngunguru
aliyasema hayo mwishoni mwa wiki baada ya kutembelea kivuko hicho ili kuangalia jinsi kinavofanya kazi.
Alisema katika mwaka wa fedha 2011/2012 Wizara hiyo imepanga kuanza ujenzi wa daraja katika kivuko hicho ili wakazi wa Mahenge waweze kwenda Kilombero kwa urahisi zaidi.
“Ujenzi huu unatokana na kivuko kuharibika mara kwa mara hivyo tumepanga kujenga daraja la kudumu ambalo litaweza kuwaunganisha wakazi wa Mahenge wilayani Ulanga kufika kwa urahisi wilayani Kilombero,” alisema.
Alisema upembuzi yakinifu utafanyika mwaka huu ili kujua gharama zake ambapo ujenzi huo utachukua miaka mitatu hadi kukamilika.
Aliongeza kuwa, matengenezo yaliyofanywa katika vivuko vinavyotoa huduma katika mto huo, yatasaidia vivuko hivyo kufanya kazi hadi ujenzi huo utakapokamilika.
Tumechoshwa na ahadi, toka 2005 Rais Kikwete aliahidi hadi leo hakuna kilichotekelezwa.Serikali tafadhali timizeni ahadi kwa wananchi wenu.
ReplyDelete