Na Timothy Itembe, Tarime
WILAYA za Tarime na Rorya Mkoani Mara zimejipanga kumkomboa mtoto wa kike kielimu ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.Hayo yameonekana katika juhudi
zinazofanywa na wananchi wa wilaya hizo kwa kuchangia ujenzi wa mabweni hususan hostel kwa wanafunzi wa kike.
Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kidato nne katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Samaritan mjini hapa, Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime Bw. Simion Wangwe, alisema suala la kumwezesha mtoto wa kike kielimu ni muhimu katika maendeleo ya taifa.
amedhamiria kuona watoto wakike wanajaliwa katika elimu ambapo wakisomeshwa wanakuwa wakwanza kuwajali wazazi punde wanapo pata kazi tofauti nawatoto wakiume
Pia aliongeza kuwa dhamira yake nikuona kuwa watoto wakike anapewa kipaumbele katika elimu iliyo mkombozi kwamtoto na kwajamii kwaujumla
Alisema maendeleo ya wilaya hizo mbili yataletwa na wananchi wa maeneo wenyewe kwanza ndipo wageni wafuate kushirikiana nao na si vinginevyo.
Aliwataka wananchi kuwa na uchungu na maendeleo yao badala ya kusubiri mtu wa nje kwa kuchangia juhudi za serikali ili kufikia malengo.
katika mahafali hayo yaliyoambatana na haramabee kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana, Bw. Wangwe alichangia sh. milioni tano.
Marafiki walioungana na mgeni huyo kuchangia harambee hiyo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Bw. Chirstopha Kangoye. Jumla ya sh. milioni 20 zilichangwa katika maafali hayo kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule hiyo.
Kwa upande wake Mchungaji John Maguge wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mkoa wa Mara Usharika wa Tarime alisema wanatarajia kujenga mabweni ya Gorofa tatu kwa gharama ya zaidi ya sh. milioni 860.
Alisema ujenzi huo utakuwa na awamu nne na kwamba awamu ya kwanza ya msingi utagharimu sh. 230,340,000.
Kwa upande wa Wilaya ya Rorya katika Shule ya Sekondari Charya Kata ya Kitembe Mbunge wa jimbo hilo Bw. Lameck Airo, ameahidi kujenga
hosteli ya wasichana yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 40-60.
No comments:
Post a Comment