26 September 2011

Fundisheni wanafunzi madharaya Rushwa-Ng'enda

Na Agnes Mwaijega

WALIMU nchini wametakiwa kuwaelimisha wanafunzi juu ya kupambana na rushwa ili waweze kuwa viongozi bora wa baadaye wenye maadili mema.Wito huo umetolewa
Dar es Salaam jana na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es salaam, Bw.Kilumbe Ng'enda, kwenye mahafali ya nne ya Shule ya Sekondari Heri.

Alisema upo umuhimu wa wanafunzi kuelimishwa juu ya madhara ya rushwa katika maendeleo ya nchi ili waweze kusaidia vita hivyo mapema tangu wakiwa mashuleni.

"Ni lazima wanafunzi waelimishwe juu ya madhara ya vitendo vya rushwa kwa manufaa ya taifa," alisema Bw. Ng'enda.

Kuhusu teknolojia alisema elimu ya kompyuta ni muhimu kwa wanafunzi ili waweze kuendana na ulimwengu wa sasa wa utandawazi hivyo kuutaka uongozi wa shule kuzingatia suala hilo katika taaluma.

Bw.Ng'enda, aliahidi kutoa kompyuta seti mbili ikiwa njia moja wapo ya kuhamasisha suala hilo.

Alitoa wito kwa wanafunzi kuwa na fikra za kujiendeleza zaidi ili waweze kujiajiri wenyewe na kuepuka kukaa vijiweni badala ya kupambana na maisha.

No comments:

Post a Comment