Na Mwandishi Wetu
WALIMBWENDE wanaoawania taji la Miss Tanzania 2011, leo kwa kupitia bia ya Redd's Original watajimwaga jukwaani katika maonesho ya mitindo ya mavazi ya
kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Maonesho hayo ambayo yanatarajia kuwa na mvuto wa hali ya juu, yanatarajia kufanyika katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam
Redd's imandaa mashindano hayo kwa warembo hao ili kuwapa nafasi ya kuonesha vipaji vyao na kutoa hamasa ya kuleta ushindani katika fainali ya Miss Tanzania itakayofanyika mwezi huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa Redd's Original, Victoria Kimaro, alisema Kampuni ya Bia Tanzania, kupitia Redd's imeshiriki kikamilifu kudhamini mashindano ya urembo kwa kutambua umuhimu wa fani hiyo, hivyo wao hawana budi kuhakikisha inawajenga washiriki hao kimashindano zaidi.
"TBL kupitia Redd's Original tulishiriki kikamilifu kuhakikisha udhamini wa mashindano kuanzia ngazi ya vitongoji hadi kanda, hivyo tumeona kuna umuhimu kuandaa maonesho ya mavazi ili kuwatia hamasa washiriki wa Miss Tanzania," alisema.
Alisema mashindano hayo yatawakutanisha wanyange hao, wadau mbalimbali wa urembo pamoja na wabunifu maarufu wa mavazi na kampuni za matangazo ili kugundua vipaji vipya na kuvipa nafasi kuviendeleza.
Meneja huyo amewataka wadau mbalimbali, kujitokeza kwa wingi ili kujionea vipaji vya washiriki hao, ambao wamepania kuoinesha vipaji vyao.
Redd’s Original imeshiriki kikamilifu kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2011, kwa kudhamini vitongoji 35 na kuwa mdhamini mkuu wa Redd's Miss Ilala, Temeke na Kinondoni.
No comments:
Post a Comment