16 September 2011

Mashoga Dar wataka kutambuliwa kikatiba

Stella Aron na Mohamed Hamad

SERIKALI imeombwa kuangalia kwa upana suala la mchakato wa uandaaji wa katiba mpya kwa kuweka kifungu kitakachowasaidia mashoga kuondokana na
adha na kero ya kunyanyapaliwa.

Ombi hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na Bw. Abdul Zungu ambaye ni shoga na mwanaharakati katika tamasha la jinsia lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

Alisema kuwa kutokana na hali waliyonayo asilimia watu wengi katika jamii wamekuwa wakiwatenga na kuwanyanyapaa na kusababisha kuishi
kwa hofu na hata kutishiwa kuuawa kwa silaha.

Alisema pia wapo baadhi ya mashoga waliopoteza maisha kutokana na kuuawa na wanapofuatilia huwa kesi zao hazitiliwi maanani kutokana na kukosa utetezi.

"Tuna haja ya sisi kupata mwakilishi katika ngazi za maamuzi na ndio maana tunataka katiba yenye kututambua kama sehemu ya  jamii inayopaswa kulindwa na kupata huduma za kibinadamu, "  alisema Abdul.

Bw. Zungu alisema wanashangazwa na jamii kuwatenga na kuwanyima
kuwapa huduma muhimu kwa tuhuma kuwa vitendo wanavyofanya havimpendezi Mungu.

"Tunaiomba Serikali iangalie upya kwa kuweka kifungu ambacho
kitatulinda kwani kutokana na hali yetu tumekuwa tukikumbana na
kero mbalimbali ikiwemo ya kutengwa na jamii, " alisema.

Mshiriki huyo alisema kuwa licha ya umoja wao kuwa na sifa mbalimbali lakini wanapofanya maombi ya kazi katika ofisi mbalimbali wamekuwa wakinyimwa bila ya sababu.

Alidai kuwa si kwamba hawana uwezo wa kufanya kazi yoyote ya kuwapatia maslahi bali kinachofanyika ni kukosa nafasi hizo na kujikuta hawana kazi ya kufanya na badala yake huendeleza
ushoga ili kupata kipato cha kuwawezesha kuishi.

"Kama Mungu angekua hatupendi basi hata leo sisi tusingeweza kuishi hapa duniani nanyi hivyo hakuna sababu ya kututenga kuishi nanyi. Haya ni matwakwa yake," alisema.

Kwa upande wa suala la afya alisema wamekuwa wakinyanyapaliwa hasa pale
wapohitaji huduma hizo na wakati mwingine huduma hizo huzipata
kwa ubabe kwa baadhi ya madaktari ama kutopata kabisa.

Alisema ni vyema Serikali ikawatambua mahali walipo ili nao  waweze kuchangia katika mapambano ya kuunda katiba mpya ambayo itajibu mahitaji yao.

"Kama katiba haitatutambua hakuna mtu ambaye anaweza akasimama kidete kututetea na badala yake ushoga utaendelea kila kukicha huku makundi yasiyokuwa na maadili yakiibuka ndani ya jamii," alisema.

Alisema mbali ya kundi lao ambalo linaonekana kutengwa pia kuna makundi mengi ambayo Serikali imeshindwa kuyatambua na kusema katiba nzuri ni ile inayogusa makundi yote ndani ya nchi yao.

Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Ananilea Nkya alisema njia pekee ya kujibu matatizo ya wananchi ni kupatikana kwa katiba inayotokana na
matatizo ya wananchi wenyewe hivyo hakuna sababu ya kuanza kujadili idadi ya kurasa wakati matatizo hayajainishwa.

"Wakati mwingine utasikia viongozi wa Serikali wakikosoa jitihada za wanaharakati wakidai kuwa wanaleta mlolongo wa mambo mengi ni katiba gani tutakayoandika yenye kuingiza mambo yote hayo?, " alisema

Hata hivyo kulikuwa na idadi kubwa ya mashoga katika tamasha hilo na kuwa kivutio kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria ambao hawajapata kuwaona 'laivu' huku wengine baadhi ya wakiangua kilio na wengine kicheko.

27 comments:

  1. Dduh huu ni mtihani kweli, sasa tuko katika Ulimwengu mwingine na hizi ndio dalili za KIYAMA!!!Hakuna dini wala mila zinazoruhusu hili jambo lakini limeshaingia ktk jamii, na haliepukiki limeshashamiri na kuota mizizi.Wazazi na jamii tuwe makini na vizazi vyetu tuhakikishe tunawapa mafunzo na maadili mema tusije tukaingia ktk mmomonyoko huu!!

    ReplyDelete
  2. HUU NI UOVU MKUBWA NA NI CHUKIZO KUBWA MBELE ZA MUNGU. MSITAKE KUIGEUZA TANZANIA KUWA SODOMA HATUTAKI LAANA KWENYE NCHI YETU. TUONDOLEENI BALAA HAPA. TENA ZINATAKIWA ZITUNGWE SHERIA KALI ZA KUWADHIBITI

    ReplyDelete
  3. KATU HATUWEZI KUKUBALI TANZANIA IWE SODOMA. RAIS, WABUNGE NA WADAU WOTE KATIKA KUINDAA KATIBA MPYA WATAKUWA PUNGUWANI IWAPO WATAKUBALI KUFANYA UOVU HUU. MUNGU AWALAANI. PELEKENI USHENZI WENU KWINGINE SI TANZANIA.

    ReplyDelete
  4. DHAMBI NI DHAMBI NA HAKUNA DHAMBI KUBWA WALA NDOGO WAPEWE HAKI YAO KUNA WATU WANAZALIWA WAKIWA NA HISIA HIZO MOJA KWA MOJA TUTAWAPELEKA WAPI WAKATI KADRI SIKU ZINAVYOZIDI KWENDA NDO WANAZIDI KUONGEZEKA WENZETU AFRIKA YA KUSINI WAMESHAPIGA HATUA

    ReplyDelete
  5. unajua tumezoea kuhukumu tu,lakini suala la ushoga ni zito sana,hizo ni hisia ambazo mtu anazaliwa nazo kabisa,japokuwa kuna wengine wamejifunza,mimi siongelei hao wanaojifunza,kuna watu kabisa wana hisia hizo tangu wakiwa wadogo kabisa,kabla hata hawajajua ushoga ni nini au mapenzi ni nini, na kuhusu huyo mchangiaji aliyechangia kuhusu laana KAMA LAANA MUNGU ALISHA ILAANI TANZANIA,KWA MAUAJI YA MAALBINO,UFISADI,UJAMBAZI,WIZI NA KILA AINA YA UCHAFU,TUSIONE TU KUWA USHOGA NDIO DHAMBI KUBWA,KUNA MADHAMBI MENGI TU WANAYOFANYA WATANZANIA AMBAYO YANASTAHILI LAANA TOKA KWA MUNGU

    ReplyDelete
  6. Ningemuona huyu Zungu haki ya Mungu ningemuua kwa mikono yangu miwili. Kufirwa afirwe yeye na aibu yake atuletee sisi ili kuonyesha watoto wetu au vijana wetu ujinga na upumbavu wake, Mbwa huyu, hivi risasi ziko wapi mimi nimmalizie laana mkubwa huyu. Anataka kuwafundisha nini watotowetu wa kiume, mbwa jike yeye, mtoeni hapa nchini, Mungu wangu mimi nikimuona nitamuua. Najuta, ningekuwa Nesi ningemchoma sindano ya sumu ili afe, Kenge huyu. Ana laana toka kwao, mtubisheni huyu shetani wa miguu saba.Aombewe fisi huyu.

    ReplyDelete
  7. Nawaomba wananchi kote nchini tumuwinde huyu shoga na amwagiwe acid (tindikali) ya uso iwe ni fundisho kwa wengine.

    ReplyDelete
  8. wapendwa ushaga ni kitu kibaya katika jamii ila kama alivyosema mchangiaji moja hapo juu kuwa ni hisia za mtu anakuwa nazo tangu utotoni japo wapo wanaoiga na kuanza kufanya hivyo ,hiyo ni kweli kabisa.napenda tu niwashauri wachangiaji wenzangu kuwa tusiwahukumu wala kuwlaani ila tukiwafahamu tujaribu kuwashauri wapo wanaweza acha.haya mambo yapo ulimwenguni kote nasema hivyo mimi nipo hapa ufaransa yaani mashoga wapo wazi sana na wana haki zao wapo wanakubali kuacha tabia hii wakipata washauri wazuri.Hivyo tuwaombee na tuwapokee wanapohitaji kushauriwa pengine pia ni kukata tamaa wanapoona jamii inawatenga.tusiwachoke bali tuwasaidie maana ni ndugu zetu.huu ndio ushauri wangu.asanteni.

    ReplyDelete
  9. mimi farida
    nasema kwakweli dunia imefika mwisho kwa hiyo na wanaume wadhihirishwe kufirwa aaaaaah tena m/mungu awapige laana wawe vipofu maisha yao yote kila anaye taka kufirwa hata wanawake wakiwemo wanaofirwa wapigwe laaana astakafirullah laadhim qiama kimeingia

    ReplyDelete
  10. Mwanaume anayeona ana hisia za kufirwa akae nazo hisia zake hukohuko mafichoni. Asijaribu kutuletea laana mbaya kwenye nchi kwa kudai katiba ihalalishe mambo ambayo ni machukizo kwa Mwenyezi.

    ReplyDelete
  11. Ni kweli kabisa wasituletee mafano yao ya ufaransa na hata marekani.Hawa wanao tetea hebu tuwaulize hivi wakisikia kijana wao anafanya matende hayo watajisikiaje?,alafu unakaa nae pamoja mezani mnakula chakula alafu aanze kukuelaza eti basha wake alimhuzunisha sana jana sinaunaweza ukamrukia na kumuua mara moja.Shenzi kabisa we Zungu inabidi tukutafute tukufanyishie usiendelee kuharibu jamii.

    ReplyDelete
  12. we unaejidai kuwapondea sana,wewe ni madhambi mangapi unayofanya yanayomuudhi MUNGU? je,una uhakika kuwa kila unachokifanya kinamfurahisha Mungu?au unajiona una haki zaidi kuliko wao? au ni msafi zaidi kuliko wao? watu wote ni sawa mbele ya Mungu uwe shoga au usiwe shoga

    ReplyDelete
  13. TANZANIA TUNAKWENDA PABAYA MNO ! NCHI SASA IMEGAWANYIKA KWA KUFUATA MAKUNDI YA KIJAMII. UTASIKIA NIMENYIMWA KAZI KWA SABABU MIMI NI MKRISTO, AU SIJATENDEWA HILI KWA KUWA MIMI NI MWISLAM ! ETI SASA WANATAKA WAPEWE KAZI KWA KUWA NI MASHOGA. BALAA HII

    ReplyDelete
  14. haki za binadamu kwa mashoga...............................May the Almighty GOD intervenes just for me.......................not in my lifetime, at least............

    ReplyDelete
  15. Kuna jamaa mmoja alishakamatwa mare tatu akiwafanya mbuzi. Je na huyo kama hisia kazaliwa nazo jamii na katiba zimfikirie? Jamani kumbuka kuna hata kitu kinaitwa "Natural Law" Hata Ng'ombe madume hayapandani na hata kuku kwa kuku au Jogoo kwa jogoo hawapandani. Imekuwaje we mwanaume na suruari (tena nasikia hata wanawake wapo)uanze kupigana serikali ikuruhusu uwatie watu nyuma?? Aombewe huyu na atafutiwe wanasaikolojia wamsaidie. Vijana wengi wamejifunza haya kutoka ulaya na america walikokumbwa na maisha magumu na kwa kuogopa kurudi nyumbani wakaingia ushogani. Wanalipwa na kulala bure. Hayo yote ni shida tu. Tuwapige vita mpaka mwisho. Huyu mwandishi anasema eti walikuwa kivutio! Kivutie cha namna gani wakati watu walikuwa wakiwalilia?? Kumlilia mtu mzima si ni dalili ya kusema ameshakufa!

    ReplyDelete
  16. Hawa ahayawani wako wengi. Ukichunguza sana ni mshiko toka majuu na kujilegeze. kama kila mtu atadai ni hisia alizozaliwa nazo je wezi? nao wakidai wamezaliwa hivyo na kwamba kwa kuwa wanaishi basi mungu ndio ametaka wawe wezi! Tusiingize tabia hizi ndani ya katiba yetu. Anayetaka kufira au kufirwa aende zake majuu akabamizwe huko huko sio hapa! Shetwaani wakubwa nyie! Mie nafikiri ndio kwanza katiba yetu ikatae tabia hizi. na hao TNGP hawana masuala muhimu zaidi ya kuwapa jukwaa mashoga? Au nao kuna mashoga na wasagwaji?

    ReplyDelete
  17. huu ni upuuzi na kuna haja ya kuwachunguza hawa TGNP pia kwa kuwakaribisha hawa wetu,mbele ya macho ya jamii yetu tena mbele ya wadogo zetu,sijui walitaka watoto wajifunze nini?

    ReplyDelete
  18. Ikiwezekana tungeomba kuoneshwa picha ya hili shoga humu mtandaoni nasi tukapata kuliona. Huyu angelimwagiwa tindi kali katika sehemu zake za makalio. Anataja kuwa kutokana na kazi hiyo ndio wanapata kipato chao. Kanichefuwa roho kwa kusema kuwa wanapendwa na Mungu. Huyu Mungu amlani.kwa kila aina ya laana. Hawa wakiachiwa kuishi basi vizazi vijazo navyo pia vitavutiwa na huluka hizi. Huyu infaa apambanishwe na Bau Seyab

    ReplyDelete
  19. Sijui sasa uovu ni nini? Kuua mwengine kwa mikono yako, kumwagia mwengine tindikali, kumuwinda binadamu mwenzio ili kumaliza uhai wake nao si uovu? Sidhani kama tutakuwa watetezi wazuri wa mila na utamaduni wa kitanzania kama tutafikiri kumaliza uovu kwa kutenda uovu mwingine. Ninyi mnaofikiri hivyo ni waovu zaidi ya huyu Zungu. "UOVU UTAMALIZWA KWA KUTENDA HAKI PEKE YAKE NA WALA SI VINGINEVYO". Naomba usalama wa maisha ya Zungu ulindwe kama binadamu mwenzetu.

    ReplyDelete
  20. Hawa wanaojidai wana hasira sana na kuandika kwa jazaba humu,ndio wa kwanza kufanya huo ushoga,huyo zungu amekuwa wazi na amesema mbele ya watu kuwa watu kama hao wapo na mambo kama hayo yapo ktk jamii,lakini ni wangapi hata mnaoandika humu mlishawahi kufanya mambo hayo?ni wengi tu,tena sana tu,watanzania wengi sana kwa sasa wanafanya mambo hayo,na ukiwaona njiani WANAYAPINGA kwa nguvu zote,sasa mnamdanganya nani?utaidanganya jamii lakini huwezi kumdanganya Mungu,pole zenu

    ReplyDelete
  21. Tabia na hisia zaanzia akilini. Ibilisi na mapepo yanakushawishi utii hisia zako. Ukimshirikisha Mungu uovu hauna nafasi.Na binadamu tofauti na mnyama aliumbwa na free choice. Hili la kufirwa si la haki ya binadamu wala Katiba huu ni uovu ambao hautofautiani na wizi na ufisadi. Kama vile sheria ya nchi haikubaliani na wizi iweje katiba yetu ikubaliane na ushoga? Nononono

    ReplyDelete
  22. Hivi hao mnaowaita mashaoga wamekuwa hatari kwa jamii yetu kuliko hao waliozembea hadi meli ikauaa malaki ya wananchi wenzetu? Wamekuwa hatari kuliko hao wanaua wazee wetu huku Shinyanga kwa tuhuma za uchawi? Wamekuwa hatari kuliko hao waliogawana nyumba zetu huku ufukweni? Wamekuwa hatari kuliko hao wanaosafirisha wanyama wetu mchana kweupe? Wamekuwa hatari kuliko hao ambao wameipora hii nchi kwa miaka 50 iliyopita? alichikifanya Zungu ni kutufumbua macho kwamba watu kama hao wapo pia katika jamii yetu, yeye amekuwa muwazi.

    ReplyDelete
  23. hao walioibia nchi hawakutumia maumbile hasi.walifanya chanya,na binadamu tumeumbwa tuwe chanya si hasi kwa maana kufanya matendo kinyume na maumbile ya Mungu, tufike mahali tutafakari, ndio maana mtanzania hatakubali jina la ushoga liingie katika katiba, ila ufisadi,wizi,na mengine yote ya kulinda jamii yataingia.

    ReplyDelete
  24. Hivi hao mnaowaita mashaoga wamekuwa hatari kwa jamii yetu kuliko hao waliozembea hadi meli ikauaa malaki ya wananchi wenzetu? Wamekuwa hatari kuliko hao wanaua wazee wetu huku Shinyanga kwa tuhuma za uchawi? Wamekuwa hatari kuliko hao waliogawana nyumba zetu huku ufukweni? Wamekuwa hatari kuliko hao wanaosafirisha wanyama wetu mchana kweupe? Wamekuwa hatari kuliko hao ambao wameipora hii nchi kwa miaka 50 iliyopita? alichikifanya Zungu ni kutufumbua macho kwamba watu kama hao wapo pia katika jamii yetu, yeye amekuwa muwazi

    ReplyDelete
  25. mungu ibariki nchi yetu isije pata uchafu ambao mashoga wanautakauingie kwenye katiba maana ni balaa tupu na laana ktk nchi yetu.

    ReplyDelete
  26. Mwl. Kalolo, C. E. Mwendisule!September 23, 2011 at 11:18 AM

    tanzania inamwitaji Yesu kabisa. ni kweli kabisa kuwa hatuwezi kumhukumu mtu tu kwa sababu ya yale anayoyafanya, lakini suala kubwa hapa ni kuangalia kwa mfano namna ambayo hao ndugu wataondokana na huo utumwa, yaani ushoga. njia pekee ya kuondokana na zigo hilo baya ni kumkubali YESU na kumkabidhi maisha yetu. hawawezi kushinda ushoga kwa kuwa tu wametambuliwa kikatiba au kwa kuwa tu hawanyanyapaliwi.
    ni yesu pekee yake anaweza kuwasaidia waachane na hilo balaa.
    watanzania tuache kuiga mambo ya magharibi na marekani. maendeleo haina maana kufanya kila kitu ambacho nchi za magharibi wako wanafanya, maana watu wa magharibi wametoka sasa kwenye ustarabu wamekuwa ni washenzi waliokubuhu.
    ili tuweze kupiga mbio ni lazima tuisalimishe nchi kwa YESU, enyi mashoga namuomba Mungu awasaidie

    ReplyDelete
  27. Sote tutambue hizi ni nyakati za mwisho. shetani anawaandaa walio wake (wanaomkubali na kumtii) na Yesu anawaandaa walio wake (wanaomkubali na kumtii). Ni chaguo lako uamue kumfuata YESU au shetani ! Nakushauri ufanye uamuzi wa busara wa kumfuata na kumtii Mungu ili akupe uwezo wa kuishinda dhambi. Furaha unayoipata katika dhambi ni ya muda mfupi sana lakini hukumu yake ni ya milele na milele, tafakari wewe binafsi na Mungu wako aliyekuumba kuwa ni njia ipi uifuate, usiangalie wengine au mwenzio anafanya nini maana kila mtu kaumbwa mwenyewe na atakufa mwenyewe, usimpe shetani nafasi ya kupumbaza ufahamu wako kiasi cha kumkana Mungu aliyekuumba.Tambua hili kuwa; mwisho wa mambo yote umekaribia, muda usiodhani wala kufikiri mwisho wako na wangu utafika na utakuwa huna nafasi ya kumchagua YESU TENA!!! FANYA UAMUZI SASA ! Mpingeni shetani nae atawakimbia, mkaribieni Mungu nae atawakaribia ninyi!!!

    ReplyDelete