Na Amina Athumani
KLABU za ngumi za mkoa wa Pwani na Dar es Salam zimetakiwa kujiandaa vyema kwa ajili ya michuano ya kuwania Kombe la Kamanda Kova 'Kova Cup' itakayofanyika
Oktoba 24 mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Makore Mashaga alisema klabu hizo zitakapojitokeza kwa wingi zitatoa changamoto kwa timu ya taifa, ambayo inajiandaa na mashindano mbalimbali ya kimataifa.
"Kwa sasa mabondia wetu wanaendelea na mazoezi kama kawaida, chini ya Kocha Mkuu Hurtado Primentel, ambapo nao watashiriki michuano ya Kova Cup kwa ajili ya kujiweka sawa," alisema Mashaga.
Alisema michuano hiyo itatoa mabondia mbalimbali kutoka mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, ambapo watashiriki kama klabu huku kila moja ikiwania kombe hilo ambalo limeandaliwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Timu hiyo ya taifa kwa sasa, inafanya mazoezi yake katika Uwanja wa ndani wa Tafa, Dar es Salaam tangu iliporejea nchini kutoka Maputo, Msumbiji ilipokuwa ikishiriki michuano ya Mataifa ya Afrika.
No comments:
Post a Comment