*Makada wake wakamatwa kwa kuchoma bendera za Chadema
*Mukama awaangukia wananchi, adai ametumwa na Kikwete
*Prof. Safari awajibu wanazuoni wa kiislamu kuhusu DC
*Nyumba ya Katibu Kata wa CUF Nyandekwe yachomwa moto
Na Waandishi Wetu, Igunga, Dar
JESHI la Polisi Wilayani Igunga mkoani Tabora, linawashikilia kiongozi mmoja na kada mwingine wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kosa kuchoma mabango ya picha ya mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kushusha bendera za chama hicho.
Waliotiwa mbaroni juzi jioni ni Katibu wa Msaidizi wa CCM ambaye pia ni Mhasibu wa CCM Wilaya ya Sikonge, Bw. Bakari Luasa na Bw. Rajabu Said ambao walikamatwa katika kijiji cha Chagana Kata ya Itumba.
Viongozi hao, walikamatwa saa 5:00 asubuhi juzi muda mfupi kabla ya msafara wa mgombea wa CCM, Dkt. Dalaly Kafumu na Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Wilson Mukama na viongozi wengine kuwasili eneo hilo.
Bw. Mukama na msafara wake walikuta tafrani baada ya wafuasi wa Chadema kuwashikilia viongozi hao na kuwadhiti hadi walipowakabidhi kwa polisi.
Makada hao wa CCM walipandishwa kwenye gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili PT 1946 hadi Kituo cha Polisi mjini Igunga ambako walikabidhiwa kwa Mkuu wa
Kitengo cha Tathmini, Ufuatiliaji na Upelelezi wa Makosa ya
Jinai katika uchaguzi huu, Bw. Isaya Mngulu.
Wakazi wa kijiji hicho wakiwamo wafuasi wa Chadema walikuwa na marungu, mapanga na mikuki ili kuwashughulikia, lakini jitihada zilizofanywa na kiongozi mmoja wa Chadema, Bw. Kibende Mwang’ombe ziliwatuliza.
Mwang’ombe aliiambia Majira kuwa waliokamatwa walifika katika
eneo hilo kufanya uhalifu wakiwa na mtu mwingine ambaye jina lake halikufamika mara moja, lakini alikimbia baada ya ugomvi kuanza.
“Siku zote CCM wemekuwa mabingwa wa kueneza siasa za
propaganda kwamba Chadema tunafanya fujo, nadhani ninyi
wenyewe mmejionea. Jambo lililonifurahisha ni kwamba viongozi waandamizi wa CCM wamejionea wenyewe,” alisema Mwang’ombe.
Mwenyekiti wa Wazazi CCM Wilaya ya Igunga, Bw. Selemani Majilanga, aliwaomba wananchi na wafuasi wa Chadema wasiwafanyie fujo wahalifu hao.
“Nawaomba ndugu zangu wananchi msifanye fujo kwa watu hao, wako
mikononi mwa polisi, basi acheni sheria ichukue mkondo wake, watashughulikiwa kwa taratibu zote zinazostahili,” alisema Majilanga.
Baada ya watuhumiwa kuondolewa, mkutano huo, uliendelea huku, Bw. Mukama akijinadi kwa wananchi kuwa ametumwa na Rais Jakata Kikwete kuwaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo mgombea
wa CCM, Dkt. Kafumu ili awe mbunge wao.
Kwa upende wake, Mratibu wa Kampeni wa CCM ambaye pia ni
Katibu wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigulu Nchemba aliwataka
wananchi kutokuchagua wapinzani kwa sababu hawana serikali.
Katika mkutano huo, mwananchi mmoja alilipandisha dumu la
maji machafu lita 20 na kumuuliza mgombea wa CCM, Dkt. Kafumu atachukua hatua gani kuondoa adha ya kukosa maji iliyodumu miaka mingi.
“Nimekuletea maji haya unayoone mwenyewe, sisi tunakunywa
maji machafua kiasi hiki, je, ukipata ubunge utafanyaje ili
tuondokane na aibu hii ambayo sasa imeonekana kuwa ya
kawaida kila kukicha,” alihoji mwananchi huyo.
Madai ya wanazuoni wa kiislamu
Chadema kimesema kuwa hakiko tayari kujibizana na wanazuoni wa kiislamu bali kinasubiri uamuzi wa mahakama utakaoamua iwapo Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario alivuliwa hijabu kwa makusudi alipokamatwa na wafuasi wa chama hicho.
Hatua hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini (HAY AT) kukitaka chama hicho kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitaha yake na hivyo kumdhalilisha.
Akizungumza na wandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho, Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA Prof. Abdallah Safari alisema kuwa chama hicho hakiko tayari kujibizana na wanazuoni hao.
"Si vizuri kuzungumzia mambo ambayo yako mahakamani lakini mahakama itaamua kama DC Fatma alivuliwa hijabu na kama alivuliwa ni kwa makusudi gani, ni uamuzi wa mahakama pekee ndio utaokaomua," alisema Prof Safari.
Alisema kuwa Chadema haina sera ya udini kwa hiyo hakiwezi kushabikia mtu kuvuliwa hijabu kwa makusudi huku akionya viongozi wa dini kuacha kutoa taarifa zinazopotosha ukweli na zinazolenga kuvuruga mshikamano wa Watanzania.
Prof. Safari ambaye ni mwanasheria na mwanazuoni wa kiisalamu, alisema kauli hizo zina lengo la kufarakanisha umma wa waislamu na chama hicho ambacho kinalengo la kuwaondoa madarakani viongozi wanaodaiwa kunuka ufisadi wa CCM
Helkopta kukata anga
Wakati huo huo Chadema kinategemewa kuanza kutumia helkopta kurudia kampeni katika Kata zote 26, lengo likiwa ni kuwakumbusha wananchi na kuwahamasisha kukichagua chama hicho zikiwa zimebaki siku tisa kufika uchaguzi.
Nyumba ya Katibu CUF yachomwa
Nyumba ya Katibu Kata wa Kata ya Nyandekwa, Bw. Hamisi Makala imeteketea kwa moto na vitu vyote vilivyokuwemo ndani.
Mratibu wa CUF Kata ya Nyandekwa, Bw. Emmanuel Ezekiel alisema wakati akifungua mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho kuwa tukio linahusishwa na mambo ya kisiasa.
Kutoka na matukio ya kihalifu yanayoendelea katika jimbo la Igunga ambako kampeni za uchaguzi mdogo zikiendelea kushika kasi, CUF imewataka wananchi kuacha kujiingiza kwenye siasa za chuki.
Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa wa CUF, Bw. Mbarara Maharagande akimwombea kura mgombea Ubunge wa chama hicho, Bw. Leopold Mahona alisema siasa za kumwaga damu zisipewe nafasi kwani zinajenga uhasama kwa wana Igunga wakati waliosababisha hayo wakitanua Dar es Salaam na familia zao.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga alithibitisha kutokea tukio hilo la moto na kumwagiza Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya kufanya upelelezi haraka.
habari za kijinga hazina msaada kwetu hamna habari nyingine za kuandika mpaka uchafu wenu wa kijinga wa siasa?tumewachokka na ushenzi wenu hasa nyie mnaotafuta umaarufu wa kipumbavu ushenzi tu huu kuna mambomengi ya kufanya sio hiyo siasa mnachokitafuta kinakuja wala hakipo mbali
ReplyDeleteacheni ujinga wandishi! mnaandika mambo yasiyo maana kwa uroho wa fedha badala kuandika mambo ya muhimu aambayo mnayaruka kama mkojo na kukanya mavi.
ReplyDeletemhariri wa gazeti hili hana akili kabisa na utambuzi, hakuna kiongozi wake makini wakumuwajibisha? kama kiongozi wa kumuwajibisha hayupo basi mmiliki naye hana ufahamu.
lakini nasikia gazeti hili ni la kifamilia ndiyo sababu pia lina wahariri wenye kazi za kifamilia badala ya kijamii.
p o l e n i!
wewe inaonyesha hauna shule na kama umesoma basi shule za mabua na ukapata zero,hata hauoni aibu,kwa taarifa yako siasa ndiyo inayo athiri mambo yote,kila kitu kinategemea siasa tena siasa safi,hivyo hayo mambo unayoyataka ni lazima yaamuliwe na wanasiasa,usirudie kuandika huo utumbo wako.
ReplyDeletehabari za kijinga hazina msaada kwetu hamna habari nyingine za kuandika mpaka uchafu wenu wa kijinga wa siasa?tumewachokka na ushenzi wenu hasa nyie mnaotafuta umaarufu wa kipumbavu ushenzi tu huu kuna mambomengi ya kufanya sio hiyo siasa mnachokitafuta kinakuja wala hakipo mbali. SI UACHE KUZISOMA KWANINI UNAZISOMA KAMA NI HABA|RI ZA KIJINGA?KILA MTU ANAJUA AKIONA HEADING IMEANDIKWA IGUNGA NI HABARI ZA SIASA KWAHIYO KAMA HUTAKI KUSOMA HABARI ZA KIJINGA BAI NA WEWE UTAKUWA MJINGA KAMA UTAAMUA KUSOMA
ReplyDeleteUkisoma habari za kijinga na wewe utakuwa mjinga unayezisoma.
ReplyDelete"siasa safi na uongozi bora"ndio mengine yanafata.wosia wa baba wa taifa utatutafuna sana,mpaka tubadilike.siasa safi ni ile yenye sera za kumjenga mwanachi wake na uongozi bora ni ule uongozi adilifu kwa uma,yote hatuna.inabidi tubadilike!
ReplyDeleteCUf ni CCM B.kwa hiyo suala la kuchomewa Nyumba katibu wa CUF ni njama za CCM na CUF ili wapate kati yao.Ngugu msomaji ukumbuke kuwa CCM na CUF wanaongoza Serikali ya kitaifa kule Zanzibar.Kwa mwono wangu hilo tukio lina utata kwa upande wangu.
ReplyDeletetatizo mtanzania wa leo ukimweleza ukweli tunaishi katika laana ya mwalimu,anakataa,tunahitaji kujirudi kwa kweli,mpasuko ulioko ccm ni matokeo ya laana, kweli nakubali,sawa na familia,baba akiacha laana kutokana na maadili ya familia,inawakumba ambao hawakufata nyao zake nzuri.nimekubali.ccm warudi nyuma wajikague,tatizo hawapendi kuambizana ukweli wanaogopana kama mchongoma.kila mtu anamwona mwenzake katika nec ya chama mwiba.wataishia taratibu,maana wanaogopona na kulindana.
ReplyDeleteHivi kwanini waandishi wa magazeti wa Tanzania hawajui kuandika habari kiutaalamu? Ipo haja gani ya kutaja namba ya gari ya polisi iliyowabebe watuhumiwa hao. Msomaji anayo interest gani au itamsaidia nini kujua namba ya gari la polisi. Namba ya gari yaweza kutajwa tu pale gari imepotea au inatafutwa ili msomaji akiiona aweze kuitambua na kutoa habari kwa wanaohusika. Kwanini waalimu wa vyuo vya uandishi wa habari, wahariri na waandishi wenyewe hawasomi magazeti ya nchi nyingine zenye ukomavu wa uandishi wa habari na kujifunza hilo. Utadhani waandishi wetu ni mambumbumbu au wanataka tu kujaza kurasa ili waonekane wamefanya kazi. Shame on your lack of professionalism. I know you will defend yourselves like hell, but I couldn't care less if you continue to display your incompetence to the world.
ReplyDeleteHuyo Fatma Kimario alikuwa anafanya nini kama sio wizi wa kura na ufisadi uliobobea katika chama hicho cha aibu kiitwacho ccm?
ReplyDeleteYajulikana dhahiri wanavyoib kura kwa hiyo wasituletee kujua au kujitetea.
CCM ni kiama cha Watanzania
HUYO MUKAMA ANAYESEMA AMETUMWA NA RAIS ANADHANI ATAM-IMPRESS NANI? RAIS MWENYEWE NDIYE HUYO ANAYESIMAMIA SERIKALI NA CHAMA KILICHOOZA KWA UFISADI NA UONGO MWINGI, AMBAYE AMESHINDWA KABISA KUIENDESHA NCHI SASA ANABAKIA NA SAFARI ZA HUKU NA KULE. ZILE SUTI ALIZOPEWA NA VIJIHALUA VINGINE VIMELIINGIZA TAIFA PAHALI PABAYA. MBONA MUKAMA ASIELEZEE HAYO? NA JE, YALE MAGAMBA YATAONDOLEWA LINI. MR GENERAL SEC. yOU ARE THE LAUGHING STOCK OF ALL TIME.
ReplyDeleteMukama is just one inept and a drunk individual. How dare he refers us to an incompetent Pres in the name of JK? Its known all over the country that the man is just a msanii aliyebobea. Kazi kupanda ndege na kuvaa vijisuti vya kuhongwa! What a shame! Angalia sasa, wameanza kutembea na wake za makada wenzao wakati wa campaign. Such a shameless party with no moral values. Ndio kazi yao. Uchafu, Uharamia, Wizi, Ufisadi na Dhuluma. Ole wenu CCM your days are numbered.
ReplyDeleteacha kila mmoja atoe maoni yake. Huo ndio uhuru wa mawazo. kama itafikia mahali tunatukanana hadharani kama unavyofanya si vizuri. Tujifunze kuvumiliana. Nchi hii ni yetu sote, hivyo ni vema tuiweke katika mazingira ya kuendelea kuwa hai. Mungu ibariki Tanzania na watu wake
ReplyDeletejadili mada acha kujadili watu. Hili ndilo kosa tunalolifanya. Jenga hoja yako katika mazingira ya amani, utulivu na uvumilivu wa mawazo ya wengine. Igunga ni sehemu ya nchi yetu, lazima tujue ikanchoendelea huko. ni sawa na kiungo kimojawapo katika mwili wa binadamu kinavyowasiliana na viungo vingine, mshipa mkubwa ni waandishi wa habari. Naomba tuwaheshimu na kuwathamini
ReplyDeletejamani msibishane mpambvu msije mkawa wajinga nayie huyo aliye tukana hapo juu sidhani kama anadini wala wazazi au jamii inayo mzunguka huyo lazima atakuwa anakula jalalani
ReplyDeleteMbona na wewe unatukana.Ama kweli nyani haoni kundule!
ReplyDeleteUkiwa umeshiba unaweza kufanya chochote hatakusema ulichokula hakikupikwa vizuri. Hii ni sawa na amani ukiwa umekaa na familia yako unahakika namustakibari wako na familia yako unaweza kusema lolote hata kuandika chocho eg Mbunge wetu hapa ARUSHA tairi kava ya gari lake imeandikwa HERI VITA.............
ReplyDeletemi mbona sielewi ujinga upi unaoongelewa hapo juu?
ReplyDeletemimi nafikiri hao wenye upeo mdogo wa kufikiri kama wa Mukama watatufikisha pabaya,kwani always wanafanya mambo bila kufiri tunanataka nini Watanzania tulio na uchungu na nchi yetu,na hawa Mafisadi wanatupeleka wapi? nini Hatima ya Tanzania baada ya miaka kumi ijayo.
ReplyDeleteTukae chini tufikiri.
Tanzania mabadiliko ni lazima watanzania tusiburuzwe tena. an injury to one is an injury to all.
ReplyDeletelaiti wananchi wa igunga wangetafakari kwa kina wasinge shangilia helkopta ya ccm. wange shangilia ya CUF na chadema. kwasababu ccm wametawla miaka 50 igunga wameshindwa kuboresha miundombinu ya barabara za rami leo hii wapinzani wameshindwa kuwafikia wananchi wameamua kutumia miundombinu ya anga ambayo ni gharama kubwa nao ccm wameleta helkopta hivyo nikuwaonyesha wananchi kuwa nao ccm wanaunga mkono upinzani kwa kushindwa kuboresha barabara.
ReplyDeletekama iyo aitoshi juzi wamekili kuwa ndege imeshindwa kutua igunga kwakua uwanja auna taa,miaka 50 wametawala wameshindwa kuweka taa uwanjani, KWELI CCM WAMELAA FOFOFO
VIJANA WA SASA WALIOZALIWA MIAKA YA 1990-1997 NDIO WATAKUWA WAPIGA KURA WENGI SANA WA 2015, WAO MTAZAMO WAO NI MAISHA BORA NA SIO BRABRA ZA KWAMBA ETI TUDUMISHE AMANI AMBAYO TUNAYO, AMANI TUNAYO SAWA NA KILA MTU ANAIPENDA,LAKINI AMANI UKU UNANJAA NI UONGO NA KUDANGANYANA, LEO UTASIKIA MARA BILIONI KADHA ZIMEFISADIWA ALAFU UTASIKIA BEI ZA BIDHAA MUHIMU AMBAZO ATUJAZOEA KUONA ZINAPANDA BEI KAMA MAFUTA YA TAA ,MAFUTA YA KUPIKIA ,PETROLI,NGANO SUKARI SEMBE N.K ZINAPANDISHWA BEI ILI KUFIDIA MABILIONI YANAYOIBIWA NA WAHUJUMU UCHUMI WACHACHE, pia utashangaa kiongozi wetu wa juu akiwa kimya kanakwamba atune nchini kama utamsikia basi ujue anaondoka nchini kwenda ughaibuni au amekutana na mgeni kutoka ughaibuni lakini sio kumsikia eti bei za vyakula mafut zipungue, JE APO KUTAKUWA NA AMANI KWELI? nawakumbusha wana CCM wenzangu yanayotokea igunga ni trella picha kamili itaonekana 2015
ReplyDeleteCCM OYE,CCM OYE, CCM OYE.
ReplyDeleteHALI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA.
ATUPENDI KUONA YANAYOTOKEA MASHARIKI YA KATI LAKINI TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA ,NA TANZANIA NA CCM LAZIMA YATATOKEA YANAYOTOKEA MASHARIKI YA KATI NA KASIKAZINI YA AFRIKA,TANZANIA SIO KISIWA.
ONDOENI MAFISADI NA SIO BRABRA ZENU