23 September 2011

HSC yaipiga 'jeki' Polisi Dar

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Home Shopping Center (HSC), imetoa msaada wa sh. milioni 60 kwa ajili ya kuisaidia timu ya Polisi Dar es Salaam inayoshiriki ligi daraja la kwanza.Akizungumza
Dar es Salaam juzi Mkurugenzi Mtendaji wa HSC, Said Mohamed alisema kampuni yake imedhamiria kuisaidia timu hiyo hadi ipande daraja.

Alisema kwa kuwa HSC, imekuwa ikishirikiana na jamii itahakikisha inaisaidia timu hiyo kwa hali na mali, ili ipande daraja.

"Tumetoa sh. milioni 60 kwa ajili ya kuisaidia timu ya Polisi iweze kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili ili iweze kushiriki ligi vizuri na kuingia hatua nyingine, " alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema HSC itaendelea kuisaidia timu hiyo hadi itakapofuzu kucheza Ligi Kuu Bara.

Akishukuru msaada huo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema kutokana na msaada huo ana imani timu yake itafanya vyema katika ligi inayotarajia kuanza kutumia vumbi hivi karibuni.

"Tunakushukuru kwa msaada huo kwani nasi tuna imani timu yetu itaanza kufanya vizuri katika Ligi Daraja la Kwanza," alisema Kamanda Kova.

No comments:

Post a Comment