LONDON, Uingereza
AMIR Khan hataki rafiki yake Victor Ortiz ampige Floyd Mayweather Junior kesho kwa kuwa anataka kupiga na mbabe huyo.Ortiz atapigana na Mayweather mjini
Las Vegas kesho na Khan anataka 'Pretty Boy', abakie kuwa bondia asiyepigwa hadi yeye atakapopambana naye katika mechi inayotarajiwa kuchezwa Agosti mwakani.
"Victor ni mpiganaji mzuri, lakini sipendi ashinde," alisema bingwa wa WBA na IBF uzani light-welter na kukaririwa na Daily Mirror.
"Ninataka kuwa wa kwanza kupigana naye na kumshinda."
"Sioni kama Ortiz atashinda, ingawa ana nguvu zaidi, Mayweather ana uzoefu zaidi na ufundi," aliongeza.
No comments:
Post a Comment