30 September 2011

Kaijage aibukia Uwakala wa soka

Na Mwandishi Wetu

MTIHANI wa uwakala wa wachezaji (players agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) umefanyika jana kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).

Watanzania wanane walijisajili kwa ajili ya kufanya mtihani huo, ambapo watano kati yao, wamejitokeza na kufanya mtihani huo uliokuwa na sehemu mbili.

Maswali hayo yalitoka FIFA na mengine kutoka TFF.

Walioomba uwakala na kufanya mtihani huo ni Adam Kapama, Aziz Sharif, Cyprian Maro, Florian Kaijage na Valence Mayenga.

Mtihani mwingine wa uwakala utafanyika Machi mwakani.

Mpaka sasa Tanzania ina mawakala saba wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA ambao ni Ally Mleh wa Manyara Sports Management, Damas Ndumbaro, John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.

Wakati huo huo, mechi ya yanga na Coastal Union ya Tanga, iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, iliingiza sh. milioni 29,146,000.

Wambura alisema watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 7,982, ambapo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 rangi ya chungwa, sh. 7,000 kwa VIP C, sh. 10,000 kwa VIP B na sh. 15,000 kwa VIP A.

Eneo lililoingiza watazamaji wengi ni kwenye viti vya bluu na kijani, ambapo waliingia 6,760 wakati lililoingiza watazamaji wachache ni la VIP A, ambapo waliingia 27.

Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo ambazo ni sh. 10,606,400 na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,446,000, kila klabu ilipata sh. 4,228,080.

Mgawo mwingine ulikwenda kwa gharama za mchezo ni sh. 1,409,360, uwanja sh. 1,409,360, TFF sh. 1,409,360, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF sh. 704,680, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA sh. 563,744 na Baraza la Michezo la Taifa- BMT sh. 140,936.

No comments:

Post a Comment