30 September 2011

Dewji ampasha Angetile Osiah

Na Mwandishi Wetu

MFANYABIASHARA na mwanamichezo maarufu nchini, Azim Dewji amesema, kamwe haafikiani na utetezi unaotolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah anayedai Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen hawezi kufukuzwa kazi kwa sababu ana mkataba wa miaka miwili.

Dewji aliyewahi kuifadhili Simba na kuipa mafanikio makubwa Afrika, alisema Dar es Salaam jana kuwa wadau wana nafasi kubwa katika ustawi wa soka la Tanzania, hivyo wasipuuzwe kwa majibu ya juu juu.

“Nimesoma taarifa inayomnukuu Katibu Mkuu wa TFF kwamba, Paulsen hawezi kutimuliwa kwa sababu ana mkataba wa miaka miwili, tena kwa sababu ya maoni ya wadau.

“Binafsi nasema hii si sahihi. Kocha anapimwa kwa vigezo vingi, lakini kama ameshindwa kazi na haoneshi dalili za kuelekea kufanikiwa, kwanini aendelee kuachwa kazini? Nahisi Osiah amepotoka na kamwe siafiki utetezi wake,” alisema Dewji.

Dewji aliongeza kuwa, kocha huyo raia wa Denmark alipaswa kuifanyia mapinduzi ya soka Stars, lakini anashangazwa kuona kila kukicha akifanya sawa na waliomtangulia, kuita kikosi kwa ajili ya mechi fulani huku akiwatumia wachezaji 'wazee', badala ya kuibua na kulea vipaji vipya kwa ustawi wa soka katika miaka ijayo.

“Hakuna jipya na wadau wanakata tamaa, ndiyo maana wanatoa ushauri kwa sababu wanaipenda timu yao. Wakiendelea kukatishwa tamaa, nani atakwenda uwanjani na TFF itapata wapi fedha? Ni vyema wakalitafakari hili, kwani tunashuhudua makocha wenye mikataba wakiachishwa kazi baada ya kushindwa kukata kiu ya waajiri wao,” alisema Dewji.

Osiah, jana alikaririwa na vyombo vya habari akimtetea Poulsen baada ya wadau mbalimbali wa michezo nchini kuhoji uhalali wa kocha huyo kuendelea kutafuta fedha za Watanzania, ilhali haoneshi mwelekeo wowote, zaidi ya kuporomosha kiwango cha wachezaji wa Taifa Stars.

3 comments:

  1. Wewe Dewji una matatizo hivi matatizo yako kwa kocha au wachezaji wenyewe?Kila siku tunaona jinsi washambuliaji wa timu zetu walivyokuwa wazembe kila wanapokaribia goli la adui.Yanga,Simba,Azam na timu nyine wote wana hayo matatizo ma kikubwa hapa ni kutokuwa na mafunzo ya kutosha toka utotoni.Msifiki wenzetu wa Nigeria,Cameroon,Ivory coast,Senegal na nchi nyingine nyingi tu wana mafanikio makubwa pasipo kuwa na mipango mahsusi kwa ajili ya kuendeleza vipaji.Wenzetu huwa wanaibua vipaji vya wachezaji kutoka mitaani na sio hapa kwetu mpaka uchezee Simba au Yanga ndio uonekane kuwa wewe ni mchezaji mzuri.Kwa staili hii ya kwetu kila siku tutakuwa wasindikizaji.

    ReplyDelete
  2. DEwji kama una la kusema bora unyamaze.Hivi Tatizo ni la kocha au wachezaji?Kila siku tunaona washambuliaji wa timu zetu walivyo wazembe kila wanapokaribia goli la adui huwa wanafanya vitu vya ajabu.Labda kocha aingie wenyewe sasa ili afunge.Wenzetu wa Afrika magharibi wanamafanikio kwa sababu wana matayarisho mazuri kwa wachezaji wao toka utotoni na sio hapa kwetu mpaka Uchezee Simba au Yanga ndio uonekana mzuri.Kwa staili hii ya kwetu kila siku tutakuwa wasindikizaji.Angalia miaka ya sabini tulikuwa na wachezaji wazuri sana na hii ilitokana na matayarisho ya kutosha Simba na Yanga walikuwa na timu A,B,Na mpaka chekechea sio sasa hivi viongozi wao kazi yao ni kula fedha na kupanga vingilio badala ya kujali soka kwanza.

    ReplyDelete
  3. DEwji kama una la kusema bora unyamaze.Hivi Tatizo ni la kocha au wachezaji?Kila siku tunaona washambuliaji wa timu zetu walivyo wazembe kila wanapokaribia goli la adui huwa wanafanya vitu vya ajabu.Labda kocha aingie wenyewe sasa ili afunge.Wenzetu wa Afrika magharibi wanamafanikio kwa sababu wana matayarisho mazuri kwa wachezaji wao toka utotoni na sio hapa kwetu mpaka Uchezee Simba au Yanga ndio uonekana mzuri.Kwa staili hii ya kwetu kila siku tutakuwa wasindikizaji.Angalia miaka ya sabini tulikuwa na wachezaji wazuri sana na hii ilitokana na matayarisho ya kutosha Simba na Yanga walikuwa na timu A,B,Na mpaka chekechea sio sasa hivi viongozi wao kazi yao ni kula fedha na kupanga vingilio badala ya kujali soka kwanza.

    ReplyDelete