06 September 2011

Hassanoo na wenzake wapata dhamana

Na Rehema Mohamed

WASHITAKIWA katika kesi ya wizi wa tani 26 za madini aina ya shaba yenye thamani ya sh. milioni 40 akiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Pwani (COREFA), Hassan Othman 'Hassanoo', na wenzake watatu wamechiwa kwa dhamana.

Hassanoo na wenzake waliachiwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu, Devota Kisoka wakati kesi hiyo ilipofikaa kwa ajili ya kuangalia kama washitakiwa hao wametimiza masharti ya dhamana.

Wakili wa Serikali Elizabert Kaganda, aliiambia mahakama kuwa upande wa utetezi tayari umewasilisha mahakamani hapo hati tano za nyumba, ambazo zimehakikiwa kuwa za kweli.

Alisema pamoja na kuhakikiwa bado ripoti ya tahmnini ya hati hizo, haijawasilishwa mahakamani hapo ili kujua thamani ya mali hizo na kuiomba mahakama iahirishe kesi hiyo, wakati wakisubiri tahmnini hiyo.

Wakili huyo aliiomba mahakama hiyo iwape washitakiwa haki yao ya dhamana na kutaka hati hizo zibaki mahakamani ambapo Hakimu Kisoka, aliwaachia kwa dhamana na kuihairisha kesi hiyo hadi Septemba 20 mwaka huu.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Wambura Mahega (32), Dkt. Najim Msenga (43) na Salim Mhidini (29).

No comments:

Post a Comment