Na Mwali Ibrahim
CHAMA cha Mpira wa Gofu Tanzania (TGU), kinatarajia kufanya mchujo wa kuwapata wachezaji wanne watakaowakilisha nchi kwenye michuano ya All Africa itakayofanyika
Oktoba 24 hadi 29 mjini Johanesburg, Afrika kusini.
Mchujo huo utafanyika wakati wa mashindano ya Gross Match Play kuanzia Septemba 21 hadi 22 mkoani Arusha.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya mchezo huo, Farai Chitengwa, alisema wachezaji 16 watachuana katika mashindano hayo na kuwapata wanne.
"Tutachagua wachezaji kwa kuangalia uwezo wao, kuanzia mashindano ya nyuma hadi mashindano hayo, watakaopatikana wataingia katika mchujo wa pili ambao utatoa watakaowakilisha nchi kwenye mashindano ya Afrika," alisema Chitengwa.
No comments:
Post a Comment