18 September 2011

CHADEMA kwa hili mmechemka

Na Gladness Mboma

ALHAMISI ya wiki iliyopita wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walimkamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma  Kimario kwa
madai kuwa walimkuta akifanya kikao na viongozi wa vijiji na kata ndani ya ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Isakamaliwa.

Kwanza kabisa kwa mtazamo wangu CHADEMA walichofanya ni makosa lisha ya kwamba walimdhalilisha kiongozi wa wananchi kwa kumvuta huku na huko huku wakitambua wazi kwamba kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Kosa ambalo ama hakika bila ushabiki wowote wahusika wote wanapaswa kushtakiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

Ni hoji kwanza, hivi hawa wahuni wanaojiita makomandoo wa CHADEMA wameenda Igunga kwa misingi ya kumnadi mgombea wao ama kumdhalilisha kiongozi aliyewekwa madarakani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Awali nilikuwa ninawakubali CHADEMA kutokana na sera zao za kuleta maendeleo lakini kwa uhuni huu uliofanywa na wanachama hao Igunga katu siwezi kusita kutamka kwamba wakipata nafasi ya kutawala nchi hii awachelewi kuwanyanyasa Watanzania kijinsia.

Tuzingatie kwamba, Bi. Kimario ni kiongozi wa nchi hawakustahili kumdhalilisha kiasi hicho, tena kibaya zaidi wanaume ndio waliohusika kumvuta mama huyo huku  na huko kama mwizi.

Haiwezekani hizi ni vurugu ambazo zinatakiwa kupigwa vita na kukemewa kwa nguvu zote ina maana kiongozi ana mipaka ya kufanya mikutano?

Huyu ni kiongozi ana haki ya kufanya kikao mahali popote muda wowote na wananchi wake bila kubuguziwa ili mradi asivunje sheria.

Ina maana wakati huu kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea Igunga kiongozi yoyote wa serikali hatakiwa kufanya kikao na wananchi wake kwa kuhofia kuwa anapanga njama za ushindi wa chama fulani.

CHADEMA sasa mnakoelekea ni kubaya mlikuwa mnakwenda vizuri sasa vurugu zenu na ubabe wenu ndio utakaowakosesha kura na wala si vinginevyo.

Kwani mkifanya siasa na kampeni za ustaarabu hamtaonekana ndani ya jamii ama hadi kila siku muwe na jambo jipya linaloonesha udhalilishaji kwa ili nidhiriki kutamka kwamba wapumbavu siku zote huwa wanajitwalia makaa ya moto wenyewe hivyo siwafichi kwa stahili hii mnajiangusha wenyewe na mnajiua wenyewe.

Vurugu hazipendezi hata kidogo, huyu Mkuu wa Wilaya ana haki ya kufanya mkutano au kikao na viongozi wake kwa sababu kwa ni haki yake ya msingi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Katika suala hili hakuna ubishi ni lazima mchukuliwe hatua, watu waliomkamata na kumdhalilisha ni lazima sheria ichukue mkondo wake huu ni ukosefu wa nidhamu.

Hii ni hatari kwa maana hiyo kiongozi yoyote wa serikali wa Wilaya ya Igunga asifanye chochote kwa kuhofia vyama vya upinzani, jamani tuacha mawazo mgando huu ni uhuni kama siyo  ujinga katika vichwa vya watu walioelimika.

Hata kama huyo mama alikwenda kinyume, lakini hakustahili kufanyiwa kitendo hicho hata kidogo ni udhalilishaji.

8 comments:

  1. HAO NDIYO CHADEMA WANAOTAKA WAPEWE UONGOZI WA NCH HII. BORA NDUGU YANGU UMELIONA NAKUSEMA WAZI UKWELI BILA KIGUGUMIZI, WATANZANIA HATUJAFIKIA HAPO. WATANZANIA WENZANGU FIKIRINI MARA MBILIMBILI KABLA YAKUWAPA WAHUNI KURA ZENU HAWASTAHILI HATA CHEMBE. NAKUPENDA TANZANIA NA NITAKULINDA DAIMA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WANANCHI WA IGUNGA WAEPUKANE NA WAHUNI HAWA WA CHADEMA AMINA

    ReplyDelete
  2. mwandishi wa makala hii ni ccm. Pole! hivi huyo mkuu wa wilaya alikuwa amevaa nguo siku huyo hadi avuliwe? MUNGU IBARIKI CHADEMA NA UWAFUNGUE MACHO CCM ILI WAONE KUWA HUYO MKUU WA WILAYA ALIENDA BILA NGUO ANAZODAI KUVULIWA.

    BRAVO CHADEMA

    ReplyDelete
  3. LO CHADEMA CHAMA CHANGU UMETENDA JAMBO LA MAANA SANA, NA HUYO MAMA ALIKUWA NANJAMA ZAKE TU, CHADEMA FANYA KAZI YAKO KUWANG'OA MAFISADI INATAKIWA USHUJAA KAMA HUO.

    ReplyDelete
  4. haya ndio madhara ya kuwa kiongozi wa chama badala ya serikali. anadai amebakwa! ana nini hadi abakwe? tuajuaje labda hata madaraka aliyapata kwa kubakwa ndio maana kutolewa nje ya ofisi kwake anaita ubakaji. anakumbukia alivybakwa siku anapewa madaraka!

    ReplyDelete
  5. ZILE HABARI ZILIZOTOLEWA KUWA CCM INA MPANGO WA KUNUNUA MAGAZETI WAKATI WA UCHAGUZI WA IGUNGA SASA ZINAJIDHIIRISHA WAZI KABISA HAKUNA MWENYE MACHO ATAAMBIWA ATAZAME USHAHIDI HUKO MBELE YAKO NA MWENYEWE UNAONA.
    INAELEKEA GAZETI ZIMA LIMEKABIDHIWA KITENGO CHA PROPOGANDA CHA CCM WAANDIKE WANACHOTAKA.

    ReplyDelete
  6. Hatudanganyiki Ng`ooo hata kama mwandishi umenunuliwa hilo watu makini tunajua unafanya propaganda na kusafisha ccm na mkuu wa wilaya eti kwa kuwa kachaguliwa na Rais ndo avuruge kampeni,Gazeti limenunuliwa na ccm wala mwandishi hajawahi kuipenda CDM maana si mtu makini nyambaaaafuuuuuuuuuuuuuuu.

    ReplyDelete
  7. Hata sielewi kama hii ni story au ni maoni. Ni dhahiri kabisa mwandishi na mhariri wake wameweka taaluma pembeni na kuanza kuandika maoni yao. lakini sishangai make mmiliki wake ambaye ni marehemu alikuwa mbunge kwa tiketi ya ccm. Kwanza ni ajabu kweli, huyu mkuu wa wilaya alikuwa hajui kwa sasa kuna kampeni za siasa igunga? Kabla hajaenda huko kwanini hakufanya utafiti kujua mikutano ya kampeni ilikuwa wapi kwa siku hiyo? Kwanza kwanini yeye afanye vikao kwenye tawi wakati huu wa kampeni? alikuwa wapi kuzungumzia swala la mifugo kabla ya kampeni? mbona halijatangazwa na vyombo vya habari kuwa ni urgent? Dc inakuaje anachukua barua za maombi ya kusimamia kura, wasimamizi si wanachaguliwa na vyama vyao kisha majina kutumwa NEC? Huu ni uhuni tu umefanywa na mkuu wa wilaya pamoja na ccm. Na kesi hii ni ya kubambikizana tu, chadema walikuwa na haki ya kumkamata kwa kuwaingilia katika eneo lao la mkutano, raia yoyote ana haki ya kumkamata mhalifu yoyote bila kujali cheo chini ya katiba ya tanzania. Tatizo letu vigogo wanafanya uhalifu wanaachwa. Mama dc hata ukimsikiliza haonyeshi kama ni mama mwenye akili, ni mtupu kweli kichwani. Ndio ma dc wanaopewa tu vyeo kwa vile walikuwa wapiga debe wa ccm. Vyeo hivyo vinapaswa kuwa sio vya kisiasa kama walivyofifanya ccm.

    ReplyDelete
  8. umalaya wake ndiyo umemponza ,huyo msege wa kike alienda kutafuta nini uko mwache akome,na wewe mwandishi sijui CHOKO!,HUJUI hata cha kuandika mbona hujaandika yule mwanaccm aliyefumaniwa na mke wa kada mwenzake huko igunga fuck seek!

    ReplyDelete