19 September 2011

Mgombea kuanzisha mashindano

Na Peter Mwenda, Igunga

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Igunga, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Leopold Mahona ameahidi kuanzisha mashindano ya Igunga Cup na kushirikisha michezo ya
soka, bao, kufukuza kuku, mbio za baiskeli na mingine.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Mwisi, ambako ni nyumbani kwa Mbunge aliyejiuzulu nyadhifa zake zote CCM Rostam Aziz, mgombea huyo alisema anajisikia uchungu kuona hakuna wachezaji wanaowika katika michezo kutoka jimbo la Igunga, wakati kuna vipaji vingi.

“Vijana wenzangu wanavyo vipaji vingi, ambavyo wanatakiwa kijengewa uwezo ili vipaji vyao vionekane, haiwezekani Jimbo la Igunga linakosa mchezaji anayechezea Ligi Kuu,” alisema Mahona.

Mgombea huyo alisema kipindi cha miaka minne atakayokuwa madarakani, atahakikisha Jimbo la Igunga linakuwa na timu ya soka ambayo itashiriki mashindano mbalimbali mkoani Tabora na nje ya nchi kwa sababu anaamini vijana wengi wataitikia.

Katika mkutano huo, msanii wa kizazi kipya, Juma Sahani aliomba mgombea huyo akichaguliwa akumbuke ahadi zake kwa sababu vijana wengi, wanahitaji kupewa mwelekeo wa kuonesha vipaji vyao katika sanaa.

No comments:

Post a Comment