17 September 2011

Chadema, DC Igunga walalamika polisi

Mkuu wa Wilaya adai amedhalilishwa
Chadema walalamika amevuruga kampeni
Wengi walaani DC kuburutwa hadharani


Na Mwandishi Wetu, Igunga

SAKATA la Mkuu wa Wilaya ya Igunga Bi. Fatuma Kimario kupigwa katika kata ya Isakamaliwa na kusabisha vurugu kati yake na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limechukua sura mpya baada ya kila upande kuvutana kwa kufungua jalada la malalamiko polisi wote wakidai kufanyiwa fujo.


Bi. Kimario alikuwa wa kwanza kufika katika kikuu cha polisi Igunga na kudai kwamba alishambuliwa juzi na wanachama wa CHADEMA kwa kushikwa sehemu zake za siri
kutukwana matusi ya nguoni na kuitwa malaya, simu yake aina  ya Sumsung yenye thamani sh.400,000 kupotea na kusababisha
kikao chake kuvunjika.

Kutokana na hali hiyo ya mvutano ililazimika kufanya  mikutano na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti kueleza
malalamiko yao.

Akizungumza na wandishi wa habari, Mkurugenzi wa  Oganizasheni na Mafunzo wa CHADEMA Bw. Singo Benson alidai kuwa Bi.Kimario amefanya makosa nane yakiwemo ya jinai na kimaadili na kuyabainisha ni kuingilia na kuvuruga kampeni za Chadema  ambazo zilikuwa kisheria, alikusanya na kujadili barua za  maombi ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura huku akijua  yeye sio mhusika.

Pia anadaiwa kutumia mali za umma katika shughuli zake binafsi kinyume cha sheria huku akitumia gari la serikali na muda
wa serikali, kufanya kikoa tofauti na muda uliokuwa umejionesha katika nyaraka zake na kuhusika na kuweka wasimamizi na waelekezaji katika uchaguzi kitendo ambacho
alidai ni hujuma na kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Inspekta  Jenerali wa Polisi Igunga, Mkuu wa Kitendo cha Tathimini na
Ufuatiliaji, Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Bw. Isaya  Mngulu alisema kuwa kwa mujibu wa ratiba ya kampeni Chadema
ilitakiwa kufanya mkutano wao katika mkata ya Isakamaliwa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa sita mchana.

Alisema wakati huo huo Bi. Kimario alikuwa na mkutano wa  ndani na watendaji wa serikali kitendo kilichosababisha   kuingiliana na Chadema hali iliyosababisha pande moja kuchukia na kupelekea vurugu huku kila upande ukidai ndio wenye haki.

Bw. Mngulu alisema kuwa kutokana na hali hiyo wafuasi wa Chadema waliamua kuvamia kiko hicho na kukivunja kikao hicho ambapo Bi. Kimario amedai kwamba alivuliwa kilemba kichwani, viatu, kukatiwa mkufu ambao thamani yake  haijajulikana, kupotea simu yake, kutukanwa kwa kuitwa  malaya.

Alisema taarifa za kuwepo vurugu eneo hilo zilitolewa na Ofisa Tawala wa Wilaya Bw. Sumera Manoti ambapo polisi walikwenda hapo haraka kukabili vurugu lakini walipofika walikuta hakuna vurugu na hakuna uvunjifu wa amani huku Bi. Kimario akiwa amekaa katika gari lake STK 3806 ambaye  alidai amefanyiwa fujo na wafuasi wa Chadema.

Bw. Mngulu alisema kuwa kutokana na hali hiyo polisi  wanaendelea upelelezi wa tukio hilo ili kukusanya vilelezo na tayari majalada mawili yamefunguliwa. Alisema watu watano wanahojiwa na polisi kutokana na tukio hilo.

Baadhi ya watu wanaohojiwa ni Mbunge wa Maswa Mashariki Bw. Slyvester Kasulumbai, Bi. Suzan Kiwanga mbunge wa Viti  Maalumu CCHADEMA Morogoro na aliyekuwa mmoja wa wagombea  nafasi ya ubunge kupitia Chadema Bw. Anuwari Kashanga ambapo wawili ni kutoka upande wa mkuu wa wilaya ambao
hawakutajwa majina yao.


Naye David John anaripoti kuwa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imesema kitendo cha kukamatwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, Bi.Fatuma Kimaro na watu wasiojulikana kimetafsiriwa kuwa ni cha kihuni na hakikufuata taratibu za kisheria.

Hayo yalisemwa na Mkurugezi wa Tume ya  Taifa ya Uchaguzi NEC Bw. Rajabu Kiravu Akizungumza Dar es saam jana katika mkutano ulioshirikisha wadau wote wa vyama vya siasa nchini kukumbushana mambo mbalimbali hususani kuelekea uchaguzi mdogo wa Igunga.

Alisema kitendo hicho kilichotokea katika kampeni zinazoendelea huko siyo kizuri na hakipendezi.

Alisema hawajapa taarifa rasmi  mpaka sasa kuhusiana na jambo hilo lakini wameona, na kusoma kupitia vyombo vya habari. "Ninachoweza kusema ni kwamba utaratibu na sheria hazijafuatwa kuhusiana na jambo hili,"alisema.

Naye Godfrey Ismaely anaripoti kuwa watu mbalimbali wamelaani kitendo cha wafuasi wanaodaiwa kuwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) cha kumfanyia fujo na kumdhalilisha Mkuu wa Wilaya ya Igunga Bi. Fatuma Kimario.

Wananchi hao walisema kitendo cha kumdhalilisha kiongozi huyo wa serikali mkuu kinaonesha kwamba CHADEMA hawajakomaa kisiasa na badala yake wanapaswa kupewa semina elekezi ili kufundwa kwa muda.

"Kwa kweli jambo CHADEMA walilifanya jana (juzi) Igunga siyo la kusifiwa hata kidogo ni la kupigwa vita. Sisi Watanzania tulianza kuweka matumaini kwa chama hicho lakini kinapoelekezwa si mahala sahihi," alisema Bi. Ester Japhet mkazi wa Bungoni Ilala, Dar es Salaam.

Kwa upande wake Bw. Anthony  Sangawe mkazi wa Mchikichini, Dar es Salaam alisema kuwa kitendo kilichofanywa na watu wanaodaiwa wafuasi wa CHADEMA kwa kumshambulia Mkuu wa Wilaya kinaonesha picha mbaya ndani ya jamii.

8 comments:

  1. mwandishi wa habari hi ni kada wa CCM au hata anaweza akawa ni kiongozi wa CCM kwa maana amepika habari kwa kuandika kiushabiki vitu ambavyo havikutokea. DC MAELEZO YAKE YOTE ATAUMBUKA KWA MAANA HAJUI KUWA ALIKUWA ANAREKODIWA NA MKANDA HAUNA HAYO YOTE ANAYODAI KUFANYIWA, KUHUSU SWALA LA MKUFU NA SIMU HUO NI UONGO MTUPU KWANI HATA PICHA ALIZOPIGWA ZINAONYESHA MKUFU HUKIWA SHINGONI MBELE YA WAANDISHI WA HABARI. ALIYEVUNJA SHERIA NA UTARATIBU HAPA NI DC LAKINI KWA KUWA TUME YA UCHAGUZI SIYO HURU HATA HAWATHUBUTU KULAANI KITENDO CHA MKUU WA WILAYA KUENDESHA MKUTANO MAHALA AMBAPO CHADEMA INAFANYA MKUTANO WAKE.

    ReplyDelete
  2. mhandishi vipi mbona umeandika upande mmoja tu unaodai DC kapigwa mbona hujapata maelezo kutoka chadema wanaodai kuwa DC hakupigwa isipokuwa ana hasira zake tu za kuhumbuliwa baada ya kufumaniwa kwa vitendo vyake vya hujuma alizokuwa akizifanya KUWEKWA HADHARANI. Jitahidini waandishi kuwa FAIR/na usawa kwa kuandika habari kutoka pande zote mbili za shillingi kwani msema peke ushinda siku zote.

    ReplyDelete
  3. SERIKALI DHALIMUN SANA HII TENA SHWAIN KABISA,MWEZI JANUARY HAPA ARUSHA POLISI WAMEMDHALILISHA MBUNGE WETU MHESHIMIWA SANA GODBLESS LEMA,HATUA ZOZOTE HAZIJACHUKULIWA,LEO ETI DC AMEDHALILISHWA HATA HAJAPIGWA...

    ReplyDelete
  4. WALIOTOA MAONI KABLA NA BAADA YA MAPINDUZI SAID NAO NI WALEWALE WAUPANDE MMOJA, LAWAMA KWA MWANDISHI KUWA AMETOA UPANDE MMOJA NA WAO WAPO UPANDE WAO.

    KUSHIKA DOLA SI LAZIMA WATU WATOKE DAMU, TUJIFUNZE KUPITIA IRAQ, BAADA YA KUTOKA SADAM WAZUNGU WALIDHANI NDIO MWISHO WA MACHAFUKO, KINACHOTOKEA WALIOWEKWA NA WAO WAMEGEUKANA MAUWAJI YANAENDELEA.

    WATANZANIA TUELIMIKE JAZBA SIO SULUHISHO LA KUPATA MADARAKA. KUWATOA CCM MADARAKANI NI RAHISI SANA KULIKO MNAVYOFIKIRIA, FANYENI JITIHADA WATU WAELEWE SERA ZENU, WAZIKUBALI, KISHA WAHAMASISHENI WAJITOKEZE WAPIGE KURA WAKIWA NA HAKI ZOTE ZA KUPIGA KURA, HAKUNA ATAKAE WEZA KUCHAKACHUA.

    MFANO MZURI NJOONI MJIFUNZE MOSHI, NDESAMBURO ALIMZIDI MGOMBEA WA CCM KURA MARA 1000, HATA ZIKIIBIA KIASI GANI UKWELI UNABAKI PALEPALE KWAMBA CCM HAWAKUBALIKI, MWISHO MSIMAMIZI ANATANGAZA MSHINDI SAHIHI,.

    ACHENI JAZBA MTAFANYA CHAMA KIONEKANE NI CHAMA CHA WENYE JAZBA AMBAPO HILI LILIONEKANA LA CHAMA KINGINE CHA UPINZANI

    ReplyDelete
  5. Kwani hamjui CHADEMA inaipeleka wapi chi hii. Ni uchaga na fujo ya wenye hela. Na hawafanyii haya Moshi bali huko Arusha , Mbeya, Tabora nk. Mwisho wa yote Mbowe na mkwe wake Mtei na akina Godbless nk wanarudi Moshi kuchekelea

    ReplyDelete
  6. Ni vema maoni yakawa ya kujenga na siyo ya utani. Unapotoa maoni ya upande moja au chuki tena ya ukabila unapaswa uione boriti jichoni mwako nawe uwe wa kwanza kulitoa kabla ya kujaribu kutaka kuitoa jichoni mwa mwingine. Upinzani una nia njema, si siri kila mtu anajua mchango wake Bungeni. CHDM ni chama cha Watanzania wote na siyo ya ukanda fulani. Ukanda unaoonekana ndiko inapopata sapoti wakati kwingine CCM ina sapoti kubwa. Kumtaja mkwewe Mbowe si jambo la ustaarabu, zungumzia hoja zisizo na chki binafsi. Fikiria taifa tunalotaka kujenga na watoto wetu liwe liwe lintoa tafsiri JEMA TOKA KWETU SISI.KILA LILILO JEMA TULISAPOTI BILA KUJALI LIMETOKA CCM AU UPINZANI. TUSOME ISHARA ZAN NYAKATI NA PIA TUJIFUNZE TOKA KWA WENZETU KM MAREKANI KUHUSU USHIRIKIANO WA MAMBO YA KITAIFA KATI YA CHAMA TAWALA NA UPINZANI.

    ReplyDelete
  7. Mwisho itafahamika tu....hata waandike kuiponda CHADEMA au la Mungu yupo kwa ufupi Watz tumechoka na siasa za kudanganywa wengi tumeelimika na kujua lipi giza na upi mawanga.

    ReplyDelete
  8. Kwa wale wanaojua ishara za mapinduzi basi wakuwa wanaelewa nini kinaendelea, HAKI haibembelezwi, haki hudaiwa. CHADEMA ni mkombozi. |Serikari gani itawale zaidi ya miaka 40, huku hali ikizidi kuwa mbaya miaka 10 ya mwisho?

    ReplyDelete