LONDON, England
TIMU ya taifa ya Brazil, ikiwa na mchezaji wake nyota Ronaldinho, imejikuta katika wakati mgumu kuifunga Ghana bao 1-0 ikiwa na wachezaji 10 katika mchezo wa kirafiki
uliofanyika kwenye Uwanja wa Craven Cottage nchini Engalnd.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza, Reuters bao hilo lilipatikana dakika za mwisho za kipindi cha kwanza kupitia kwa Leandro Damiao, baada ya kukatiza katikati ya mabeki wa Ghana na kuwahi mpira aliotengenezewa na Fernandinho na kisha kuachia mkwaju uliojaa wavuni.
Kwa mujibu wa shirika hilo, mtanange huo ulianza kwa kila timu kukamiana, lakini baada ya kutolewa kadi nyekundu, mambo yakabadilika na kuifanya Ghana icheze kwa kujihami hususani kutokana na kutolewa beki wake, Daniel Opare dakika ya 32 baada ya kuonywa mara kadhaa kabla ya mwamuzi kutoka England, Mike Dean kumuonesha kadi nyekundu.
Hata hivyo mechi hiyo ilionekana kama itamalizika vibaya, baada ya mwamuzi Dean kutoa kadi za njano saba zikiwemo mbili alizooneshwa Opare.
No comments:
Post a Comment