28 September 2011

Askofu TAG aishukia CCM

*Asema matamshi yake Igunga si salama kwa nchi
*Wanazuoni waagiza waislamu kukihama CHADEMA


Na Waandishi Wetu

ASKOFU Gloriuos Shoo wa Kanisa la Tanzania Asssemblies of God (TAG) jimbo la Kilimanjaro amesema matamshi yanayotolewa na viongozi mbalimbali wa
siasa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga ni kipimo pekee cha kubaini ni viongozi walioko tayari kuoa lugha za uchochezi zikitawala nchini.

Akizungumza na Majira ofisini kwake askofu huyo alisema kuwa
kumekuwepo na kauli mbalimbali za vitisho ambazo hutolewa lakini
hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na badala yake serikali iliyopo
madarakani inadhalilika.

Akimnukuu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Wilson Mukama kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeingiza makomandoo 60 kutoka katika nchi mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Igunga, alisema huko ni kuidhalilisha serikali kwamba haipo makini na ulinzi wa nchi

“Matamshi haya ni kuidhalilisha serikali, sasa kama hali ni hii basi
wananchi tuamini serikali imeshindwa kutulinda hadi tunaingiliwa na
wavamizi na hakuna jitihada zinazochukuliwa na serikali au
inaogopa?" alihoj askofu Shoo.

Askofu Shoo alisema kuwa CCM kimefanya vibaya zaidi ya wale wafuasi wa CHADEMA kukamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario baada ya kitendo hicho kutumika katika mjukwaa ya kisiasa huku jambo hilo likihubiriwa kiudini.

Alisema kuwa kila chama kimefanya makosa ila kitendo cha kuchukuliwa
suala lile kidini tayari ni kupandikiza chuki dhidi ya waislamu na
wakristo, jambo ambalo ni baya kwa nchi yoyote ile duniani.

"Nani ambaye ni mbaya aliyemkamata mkuu wa wilaya au mtu anayetumia
muda mwingi kuhubiri suala lile katika majukwaa ya siasa kuomba ridhaa
ya wananchi wampigie kura, eti ni kuudhalilisha uislamu, hii ni sahihi
kweli?" alihoji Askofu Shoo

Hali kadhalika askofu huyo aliwataka wakazi wa Igunga kuwa makini na
kufanya maamuzi magumu dhidi ya watu ambao hawajali utu wa mtu na
kutumia lugha za vitisho kuwa watashinda kwa gharama yoyote.

Wanazuoni waikomalia CHADEMA

Umoja wa wanazuoni wa Kiislamu Tanzania wameendelea kuikomalia CHADEMA safari hii wakiwaagiza waislamu wote nchini kukihama chama hicho mara moja kwa kupuuza agizo la kuwaomba radhi waislamu.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa Sekretarieti ya moja huo, Shekhe Sherally Hussein alisema wametoa tamko hilo baada ya wafuasi wa CHADEMA kumzalilisha Bi. Fatma Kimario kwa kumvua Hijab na kukataa kuomba msamaha.

Agizo hilo linakuja siku chache baada ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CHADEMA, Profesa Abdallah Safari kusema CHADEMA isingejibu hoja za wanazuoni hao kuhusiana na suala hilo kwa kuwa liko mahakamani, na mahakama ndiyo ingeweza kusema kama kweli walimvua DC Kimaria hijab, na kama walifanya hivyo makusudi au la.

Shekhe Hussein alisema waislamu na wapenda amani nchini wakihame CHADEMA  kuokana na kutoheshimu imani za wananchi na kujichukulia sheria mkononi wakati vyombo vya dola vipo.

"Tuliwapa siku nne za kuomba radhi viongozi wa CHADEMA kwa kuizalilisha Dini ya Kiislamu kwa kumvua hijabu Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario lakini wamekaidi agizo hilo ,waislamu wote hatuna budi kukihama chama hicho kwani kinalengo la kudhohofisha uislam"alisema.

9 comments:

  1. wnazuoni uchwara na elimu yao ya darasa la saba nyie ni akina nani kuingilia demokrasia ya waumini wenu, mbona hamjawambia waislam wahame CCM kwani iliua watu pemba na mwembe chai

    ReplyDelete
  2. WANAZUONI, SISI WAISLAMU WENZIO TUNAWAHESHIMU SANA ILA TUNAWASIHI SANA MSIWE MNATUPA MAAGIZO/USHAURI AMBAO HAUNA MANTIKI HASA KUHUSU HUYU BI. FATMA KIMARIO NA KISA CHA HIJAB. SISI WAISLAMU NI WATU WAZIMA NA AKILI ZETU. TUPENI MAWAZO TUYAJADILI NA SIO KUTOA AMRI AU MATAMKO KAMA YA AKINA OSAMA YALIYOPITWA NA WAKATI. AHIENI KILA MUUMINI WA DINI AFANYE MAAMUZI YAKE YA KISIASA PEKEE. KWA UPANDE MWINGINE SERIKALI NA VYAMA VYA SIASA VIACHIE VIONGOZI WA DINI WAFANYE MAAMUZI YAO BILA KUVUNJA SHERIA. KWA HILI LA IGUNGA MMENOA. WASIPOHAMA MTAFANYA NINI?

    ReplyDelete
  3. mnaojiirta wanazuoni waislamu ninyi ni UCHWARA NA HAMNA LOLOTE NJAA TU ZINAWASUMBUA KELBU WAKUBWA NYIE!!! TUKICHUNGUZA VYETI VENU TUTAVIKUTA NI UCHWARA....... WASOMI WAISLAMU TUNAWAJUA NA TUNAWAHESHIMU SIO NYIE MAMJUSI MAGULUGUJA

    ReplyDelete
  4. mbona nasikia dc mwenyewe alisha badili dini mda mrefu baada ya kuolewa na mzee kimario hili hijabu ana vaa kama pambo mume wake ni mchaga huyu mama nimkristo kama ni uislam mzee kimario amesha mtoa hko ss tuangalie yte sio kulazimisha watu wahame chama kwa ajili ya mama huyu

    ReplyDelete
  5. Sherrally akili zake azina akili,Asituletee udini katika siasa kama hana la kusema bora akae kimya tu.

    ReplyDelete
  6. Wanazuoni mara nyingi huwa wanatoa mawazo safi kwa waumini na kutoa tafsiri ya maandiko matakatifu (Qoran). Katika mafundisho nilowahi kupata, na uelewa wangu wa Qoran, sijaona mahali palipoandikwa kuwa adhabu ya mtu alomvua hijab mwanamke wa kiislamu na kuhama chama cha siasa. Labda haya ni mambo ambayo yamekuja baada ya Mtume!

    Lakini pia ni vema wanazuoni wakatupa na mahali pa kwenda bada ya waumini wa kiislamu kuhama CHADEMA. Maana ni kama wanatuacha hewani. Naomba wamalizie kabisa kwamba sisi waislamu baada ya kuhama CHADEMA twende chama gani (ambacho hakijawahi kuudhalilisha uislamu na waislamu-kwa kutenda, kufikiri, na kunena).

    ReplyDelete
  7. WANAZUONI WETU,NAOMBA MJIULIZE NA MJIBU SWALI HILI. IKIWA KUNDI LA WANANCHI LINALOANDAMANA LENYE MCHANGANYIKO WA MADHEHEBU LIKIFANYA FUJO KWA KUVUNJA MADIRISHA YA MADUKA,SERIKALI IKITOA AGIZO/USHAURI KUWA WAISLAMU WAICHUKIE NA KUUHAMA UISLAMU ETI KWA SABABU YA KITENDO HICHO; NYIE WANAZUONI MTAJISIKIAJE? KUONYANA NA KUREKEBISHANA KIDINI NDIO SULUHISHO!

    ReplyDelete
  8. Tofauti iko wapi kati ya waraka wa kanisa kuhusu kuwachagua wacha Mungu uchaguzi mkuu na uamuzi wa wanazuoni wa kutaka waislamu kuhama chadema.Bila maagizo ya maaskofu leo kusingekuwapo chadema yenye wabunge wengi na nguvu waliyonayo.Ni pale viongozi wa kidini wanapoamua kuingia kwenye masuala ya kisiasa ndipo vurugu zinapoanzia.

    ReplyDelete
  9. NAONA HUYU ASKOFU ANA KICHAA,ANANUKUU MANENO YA SLAA NDIO MAONI YAKE? SI APANDE TU JUKWAANI APIGIE DEBE CHADEMA. SISI TUNAWAJUA HAO KINA SHOO WAMEVAA MAJOHO MBELE YA WAUMINI WAO NA WAKITOKA WANAWAPIGIA KAMPENI CHADEMA. HAKUNA KIONGOZI WA CCM ANAYEWEZA KUPANDIKIZA UDINI HAPO KWANI CCM IMESHENI DINI ZOTE,KABILA ZOTE NA KILA AINA YA JAMII IKO HUKO CCM WALA HAKUNA UPENDELEO WA KABILA FULANI HUKO,WOTE NI WATZ

    ReplyDelete