12 September 2011

Ajali ya meli mtaji Igunga

*Yatumika kuonesha uzembe wa serikali
*CCM yasitisha kampeni,wengine kama kawa
*Muafaka Zanzibar watumika kuibomoa CUF
*Mkapa yaanza kumkuta,CUF sasa yamwandama


Benjamin Masese na Peter Mwenda, Igunga

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na  Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa  amesema
ajali ya kuzama kwa meli ya Mv SPICE katika kisiwa cha Nungwe, Zanzibar imetokana na uzembe wa serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Igunga jana, Dk. Slaa alisema serikali imeshindwa kujifunza kutokana na ajali nyingi ambazo zimekuwa zikitokea
nchini.

“Tumesikitishwa na ajali hii, kifo ni jambo la kusikitisha, nasikitika kuona serikali imeshindwa kujifunza kutokana na ajali mbaya ambazo zimekuwa zikitokea na kupoteza mamia ya watanzania wasiokuwa na hatia,

…serikali imeshindwa kujifunza kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba mwaka 1996 na kuua watu wengi,nilitarajia vyombo vinavyohusika vingekuwa makini, lakini hakuna chochote,”alisema Dkt. Slaa.

Alisema amesikitishwa kuona Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kushindwa kusimamia vyema majukumu yake kutokana na sheria kuupuzwa huku serikali ikiwa haijifunzi.

“Naomba kutumia fursa hii kuiambia serikali kwamba iwasake wahusika wote walioruhusu meli hii kuendelea na safari, taarifa zinasema ilizimika mara nane  na hakuna msaada wowote uliotolewa,”alisema Dkt. Slaa.

“Tunasikitika kuona serikali imeshindwa kuwathamini watu, sisi tunasema wakati umefika wa watu kubadilika,CHADEMA  inasikitishwa na hali  hii,”alisema Dk. Slaa.

Kuhusu maombolezo, Dkt. Slaa alisema kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete hakutangaza maombelezo ya kitaifa, CHADEMA inaendelea na kampeni zake, lakini ndani ya kampeni hizo itaendelea na  maombelezo kwa kila mkutano.

“Kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hajatangaza siku za maombolezo, sisi tunaendelea na kampeni kutokana na kubanwa, lakini kila mkutano wetu tutasimama na kuwakumbuka marehemu wote,”alisema Dkt. Slaa Dk. Slaa alisema amesikitishwa na wamiliki wa vyombo vya runinga kuendelea kuonyesha tamthilia baadala ya kukatisha matangazo na kuonyesha tukio la ajali hiyo.

Wakati huo huo CCM imesitisha kampeni zao kutokana na tukio la meli kuzama na kuua
abiria, huku CUF na CHADEMA vikiendelea na kampeni zake.

Wakati huo huo Dkt. Slaa amesema chama cha CUF kimepoteza mwelekeo baada ya kufunga 'ndoa' (kuingia muafaka) na CCM,hivyo kinashiriki uchaguzi mdogo wa Igunga kwa lengo la kupinga upinzani.

Alisema CUF ni chama cha kinachofananishwa na waarabu kutokana na mienendo ya viongozi wao na hata sura na tabia, hivyo hakina jipya wala mabadiliko yoyote
yanayoonekana machoni mwa jamii ya Watanzania.

Dkt. Slaa alitoa kauli hiyo wakati akihotubia wananchi wa Kata ya Simbo katika Jimbo la Igunga kwenye mkutano wa kampeni wa chama hicho.

Alisema kawaida mwanamke anapoolewa na mwanaume huungana na kuwa mwili mmoja, na kawaida mwanaume ndiye mwenye nguvu ya kuamua ambapo mwanamke hubaki
kunyenyekea na kutoa ushauri.

Alisema ndoa hiyo imedhoofisha CUF na kusababisha kuishi kwa hofu na kutojiamini.

Alisema ndiyo maana chama hicho kimeanza  kupinga upinzani kwa kutoa hoja zisizo na maana na za kitoto dhidi ya CHADEMA.

Dkt. Slaa alisema CUF haijui inapoelekea na inachokisema haikijui ndio maana inadai kuwa CHADEMA inatakiwa kuondoa mgombea wao kutokana na kuwa na mtaji mkubwa wa wananchi.

Alisema kuwa CHADEMA iliwachia jimbo hilo,lakini CUF haikufanikisha kulitetea, hivyo ni zamu ya CUF kujiondoa na si kutumia takwimu za mwaka jana kupotosha wananchi.

Alisema kuwa mbali ya hiyo Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ni mtu wa kutokuwa na takwimu sahihi za majimbo ambayo CHADEMA imekuwa ikiiachia CUF isimamishe wagombea.

Wakati huo huo  chama cha  CUF kimemshukia Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa  kuhusu hotuba yake ya kushambulia upinzani, kuwa amedanganya wananchi kuwa wameleta maendeleo nchini kwa sababu kipindi cha utawala  wake alichangia serikali yake kufanya biashara ikulu na baadhi ya vigogo kujinufaisha bila kujali maisha duni ya Watanzania.

Kaimu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Bw. Julius Mtatiro, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Bw. Mkapa  afahamu kuwa uongozi wa  CCM  akiwemo utawala wake ndiyo walioleta umasikini mkubwa nchini katika kipindi cha miaka 50 na maendeleo yake hayalingani na umri huo.

Bw. Mtatiro alisema CCM imetawala Tanzania kwa miaka 50 lakini bado  haitoi umeme kwa asilimia 90 ya wananchi ,hakuna mtandao wa uhakika wa barabara, Shirika la Ndege  Tanzania (ATC) halina ndege hata moja,mashirika yote ya umma yako mikononi  mwa walowezi wachache, mifugo yake inayofikia matrilioni haina uwezo wa kupeleka nyama na maziwa ya kutosha soko la dunia.

Bw. Mtatiro alisema wakati wa utawala wa Rais Mkapa serikali ilinunua ndege ya rais kwa bei ya anasa na Waziri wa Mkapa kutukana wananchi kuwa ikibidi watakula nyasi, ili ndege inunuliwe na rais huyo kumtetea waziri husika na hatimaye ndege hiyo ya anasa  ilinunuliwa.

”Ndege ya kifahari ilinunuliwa huku raia wa Igunga hawana maji,wakulima na wafugaji wa Igunga na kwingineko wakiwa hawana dawa wala pembejeo,lazima wananchi wajiulize kati ya kununua ndege ya anasa ya Rais badala ya  kujenga daraja la Mbutu ambalo linawatesa na kupoteza maisha ya wananchi wa Igunga  nani anayemdanganya Mkapa?alisema Bw. Mtatiro.

Alisema wananchi wa Igunga watakuwa wamejikomboa kama watamchagua mgombea wa CUF ,Bw. Leopold Muhona.

8 comments:

  1. Kweli watu wakamatwe liwe fundisho! Roho za watu haziwezi kwenda hvhv!

    ReplyDelete
  2. Ninaungana na mawazo ya kuthibiti hali ya usalama wa vyombo vya Usafirishaji wa watu na bidhaa. Ninafahamu ya kwamba ajali zote hazitokani na uzembe tu bali ni kama ule msemo wa wahenda "ajali haina kinga". Kwa upande wa sababu ya ajali nyingi ni lazima pia tuangalie pande zote mbili: sehemu ya kwanza sheria zilizopo zifuatwe na wote: mwenye chombo hicho ahakikishe anafuata utaratibu wa kujua uwezo wa chombo chake; kina uwezo wa kubeba abiria wangapi na mizigo tani ngapi; tena mimi msafiri nikiona chombo hicho kimejaa basi nisilazimishe kukipanda na pia niwe mwepesi wa kutoa taarifa kwa vyombo vya sheria, na pia serikali iwe makini kukagua usalama wa vyombo hivyo. Ni MSIBA mkubwa wa taifa letu kwa ajali hii Bahari ya Hindi, nami kama mja wake Mwenyezi Mungu naomba Mwenyezi Mungu awalaze pema waliotutangulia na awafariji waliliofiwa na awaponye wanaougua. Pia nataka kusema tu ya kwamba Dr. Slaa asitumie msiba huu kuilaumu serikali kwa jambo hili maana hata yeye alilikuwa mmoja wa wabunge wa serikali zilizopita hivyo basi hawezi kujito na kuwapakazia wengine. Naungana na mawazo ya kuwakamata wahusika ili wafikishwe mahakamani.

    ReplyDelete
  3. Kuwa mbunge mmoja ndani ya bunge la ccm 80% hauwezi kuleta tofauti kubwa ya maamuzi huo ndo ukweli, pili swala kusimamia usalama wa majini ni la serikali siyo bunge, bunge kazi yao ni kutunga sheria za kuipa mamlaka serikali kusimamia usalama wa watu. Hivyo usimtuhumu dr Slaa kwa jambo ambalo hakuwa na mamlaka nalo! Naungana na Dr Slaa na mtoa maoni hapo juu kuwa walio husika wasakwe na wapelekwe kwenye vyombo vinavyohusika haki ichukue mkondo wake!

    ReplyDelete
  4. Unatushangaza wengi Slaa na Udaktari wako huwezi kujiangalia wewe mwenyewe na kujifahamu. Huwezi kutoa mifano juu ya ndoa wakati wewe mwenyewe unachemka na kuishi na wanawake wa watu. Walio wengi Igunga hatuna imani nawe Slaa. Kwanza nenda Zanziba ukatoe Rambirambi. CHADEMA haijatoa RAMBIRAMBI na Zito alienda kivyake kama kawaida yako. Mna uchu wa madaraka.

    ReplyDelete
  5. ukweli siku zote unauma sana. Slaa kuonesha jinsi watu walivyo wazembe katika utendaji wao wa kazi, walio na mgando wa fikra wanambeza. kama si uzembe ni nini??
    Meli ina uwezo wa kupakiwa watu 500 sasa hao waliozidi ni mungu alipanga wazidi au ni uzembe. kama meli inabeba mizigo tani 100 tu ikizidisha na kubeba tani 200 ni mungu au uzembe wa watu.
    Hakuna haja ya lawama hizi kumpa mungu kwa kudai kuwa ajali haina kinga!!! kuna ajali zenye kinga, visivyo na kinga ni matetemeko ya ardhi, vimbunga na katrina ila kwa hili la zanzibar waliohusika kwa aina yoyote katika ajali hii wawajibike kama sio kuwajibishwa!!!

    ReplyDelete
  6. unayemshangaa Slaa ni wewe peke yako ulio na mgando na uvundo wa akili. Wenye kutumia vichwa vyao wote wamemuelewa ila wewe uliyeolewa na mke wako hauwezi kuelewa.
    Slaa alimuibia nani mke? au kamuiba mama yako? mwenye mke yuko wapi?? mbona baada ya uchaguzi haendeleei kudai mke wake.
    Wewe ndio miongoni mwa wanaume wanaowauza wake zao ili wapate pesa kwa kuwashika ugoni.

    ReplyDelete
  7. Sio kweli, tu wengi tunaomshangaa Slaa na kama we hapo juu unabisha basi njoo hapa Igunga ujionee mwenyewe CHADEMA anavyoshindwa. Kama ni uaminifu basi Slaa ndo ulimshinda hata hakuweza kuishi kiapo cha upadre. Kama vile alilaaniwa hakuweza kuishi na mke wake wa kwanza. Nani anasema anamwelewa kama sio kutapatapa. Utatumiaji msiba kama huu kuufanya mtaji wa kupatia kura??? Ushindwe kabisa.

    ReplyDelete
  8. Watakataa matokeo hao. kuna mijibwa ya wachaga kazi yao kumtetea Slaa ili awafanikishie kisha wamuue, na iko siku huyo Slaa atawachukulia mama zao kwa sababu baba zao wamechacha na watasherehekea,nadhani kuna laana fulani ndani yao. IGUNGA BORA JINI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKWISHA. WAULIZENI KIGOMA NA KWINGINEKO KUNA MAENDELEO GANI WALIYOPELEKA ZAIDI YA POROJO?

    ReplyDelete