Na Salim Nyomolelo
WAKUFUNZI watatu wa mchezo wa kujihami wa shoulinj Kempo, wametua nchini juzi wakitokea Japan kwa ajili kuangalia maendeleo ya mchezo huo na kutoa semina
kwa makocha wake.
Akizungumza Dar es Salaam jana kocha wa shoulinj Juu Kensh Omary Majid, alisema kwamba wakufunzi hao wakiwa nchini watatoa mafunzo ya mchezo huo pamoja na semina kwa walimu na wanafunzi.
Kocha huyo aliwataja waamuzi waliowasili nchini kuwa ni Sensea Akia Tamura, Sensei Hiroki Kobayashi na Sensei Akira Kato.
Alisema mafunzo yatashirikisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali kutoka mikoani, ambao wanatakiwa kufika mapema ili kuhudhuria semina hiyo.
Kocha huyo alisema baada ya mafunzo na semina hiyo Jumapili kutafanyika maonesho ya mbinu mbalimbali za kujihami, katika Ukumbi wa hoteli ya Starlight iliyopo Dar es Salaam.
"Tunapenda kuwaalika watu wote watakaopata nafasi kufika Starlight Jumapili kushuhudia mbinu mbalimbali za kujihami kwa kuwa hakutakuwa na kiingilio.
No comments:
Post a Comment