26 August 2011

Wahadhiri Ustawi wa Jamii wawekewa ngumu

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda amesema serikali haiwezi kuwarudisha kazini wahadhiri 27 waliofukuzwa katika Chuo Kikuu cha Ustawi wa Jamii, na imetoa onyo juu ya
vitendo vya migomo na maandamano ambavyo havina tija.

Hayo yalisemwa, Bw. Pinda wakati akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Viti Maalum CCM, Bi Angellah Kairuki, ambaye alimtaka serikali ieleze kama  ina mpango wa kurejesha kazini wahadhiri hao.

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa; "Hatuwezi kufanya hivyo (kuwarudisha kazini) kwani nchi hii inaongozwa kwa taratibu zake za kisheria."

Alisema awali wahadhiri waliofukuzwa chuoni hapo walikuwa watano, ambapo serikali iliona ni vema iwaondoe chuoni kwa kuwa sifa zao zilionekana kutokidhi vigezo katika chuo hicho.

Alisema baada ya serikali kuwafukuza kazi wahadhiri hao watano, ndipo kundi la wenzao lilipoanza kuongezeka hadi kufikia saba. Alisema kama kuna mtu anahisi kuonewa,  sheria zipo wazi na anaweza kwenda mahakamani kudai haki zaidi.

Hata hivyo, alisema kuwa endapo wahadhiri hao waliofukuzwa wana hoja ya kisheria zaidi ya hatua zilizochkuliwa na serikali, basi serikali itakuwa tayari kukaa nao kuwasikiliza.

Alisema tayari serikali imeshapata wahadhiri wengine 18 chuoni hapo na tayari wameshaanza kufundisha. Aliwataka
watumishi kuacha wa serikali kuacha tabia ya kukimbilia maandamano  na migomo. Chuo hicho wiki iliyopita kilitangaza kuwasimamisha kazi wahadhiri wahadhiri 27 wa chuo hicho kutokana na kushiriki mgomo.

No comments:

Post a Comment