Na Rehema Mohamed
KAMPUNI ya Brands International Limited imefungua kesi katika Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara ikiilalamikia Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaa (UDA) kwa
madai ya kuingilia sehemu yake ya biashara.
Kesi hiyo namba 68 ya mwaka 2011,ilifunguliwa Agosti 17 mwaka huu mahakamani hapo na ipo mbele ya Jaji Amiri Mruma.
Katika kesi ya msingi,inadaiwa kuwa UDA na Kampuni ya Brands International Limited walikuwa na makubaliano ya upangaji eneo la UDA,lakini shirika hilo lilionekana kuvunja makubaliano hayo.
Kutokana na hali hiyo,Kampuni ya Brands International Limited inaitaka UDA kulipa fidia ya sh.milioni 133,400,000 kama hasara iliyopata kwa kuvunjiwa ukuta.
Pia inataka kulipwa fidia dola 16,493 kufia hasara ambayo kampuni hiyo ilipata kila mwezi kuanzia Julai 2010.
Kesi hiyo jana ilitajwa mbele ya Jaji Mrumi kwa ajili ya kusikiliza maombi ya mlalamikaji.
Hata hivyo kampuni ya UDA imeamriwa kupeleka mahakamani hapo hati ya kiapo kujibu maombi ya mlalamika kabla ya Septemba 9, mwaka huu.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment