*Yaichapa Coastal Union bao 1-0
Na Mashaka Mhando, Tanga
MABINGWA wa Ngao ya Jamii, Simba, jana walivunja mwiko wa kufungwa na Coastal Union katika Uwanja wa CCM Mkwakwani mkoani Tanga, baada ya
kuilaza Coastal Union bao 1-0.
Coastal Union katika vipindi tofauti, kila inapokutana Simba kwenye uwanja huo, huibuka na ushindi, ambapo kwa mara ya mwisho mwaka 2007 ilishinda bao 1-0, bao lililofungwa na Sunday Peter.
Kwa upande wa Simba, mara ya mwisho kuifunga Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani ilikuwa mwaka 2002, ambapo ilitoka uwanjani na mabao 3-0 na kuishusha daraja, wakati huo ikifundishwa na marehemu Kinanda Zakaria.
Simba ilianza mchezo kulisakama lango la wapinzani wao, ambapo Gervais Kago alipata nafasi nzuri dakika za mwanzo na kuzitikisa nyavu za wapinzani wao, lakini mwamuzi wa mchezo huo, alilikata kwa madai kuwa, mfungaji alikuwa ameotea.
Simba ilipata bao la kwanza dakika ya 24, lililofungwa na kiungo Patrick Mafisango, kwa shuti kali lililogonga mwamba wa juu wa goli na mpira kuvuka mstari, lakini ukatoka nje.
Bao hilo liliwafanya wachezaji wa Coastal Union kumzonga mwamuzi Thomas Mkombozi , wakipinga bao hilo.
Bao hilo lilitokana na mpira wa kona uliopigwa na Amir Maftah, na kuokolewa na mabeki wa kosa, kabla ya kumkuta tena Maftah aliyempasia NasoroMasoud 'Cholo' na kumsukumia pasi safi mfungaji wa bao hilo.
Coastal Union: Omari Hamis, Mbwana Hamis, Soud Abdi, Jamal Macheranga, Salim Omari, Sabry Makame, Francis Busungu, Hassan salum, Rashid Mandawa, Aziz Gila.
Simba: Juma Kaseja, Said Nasoro 'Cholo'/Obadia Mungusa, Amir Maftah, Juma Nyosso, Victor Costa, Patrick Mafisango, Ulimboka Mwaingwe, Jerry Santo, Gervais Kago, Haruna Moshi 'Boban', Emmanuel Okwi.
No comments:
Post a Comment