25 August 2011

Yanga yabanwa na Moro United

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga, jana walibanwa na Moro United, katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro na kwenda sare ya bao 1-1.

Mchezo huo ulianza kwa kasi, ambapo Moro United walikuwa wa kwanza kulifikia lango la Yanga, lakini washambuliaji wake, hawaku makini kukwamisha mpira wavuni.

Yanga walijibu mashambuliaji dakika ya 12, ambapo Hamis Kiiza aliwatoka mabeki wa Moro United na kupiga shuti kali lililogongwa mwamba goli na mpira kutoka nje.

Wakizidisha mashambulizi, Yanga walipata nafasi nyingine kupitia kwa Pius Kisambale akiwa amebaki na kipa wa Moro United, Lucheke Mussa, lakini kali lilitoka nje ya lango.

Dakika ya 19, Gaudence Mwaikimba wa Moro United, alipata nafasi nzuri, lakini beki ya Yanga, ikiongozwa na Chacha Marwa, iliondosha hatari hiyo langoni kwao.

Yanga walipata bao lao dakika ya 68, lililofungwa na Haruna Niyonzima kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Godfrey Bonny.

Bao hilo liliizindua Moro United ambapo walisawazisha bao hilo kupitia kwa Jeremo Lambele dakika ya 87, akiunganisha mpira uliopigwa na Salum Mpakala.

Yanga ilipata pigo baada ya kiungo wake Juma Seif 'Kijoto', kutolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Ibrahim Kidiwa wa Tanga.

Yanga: Shaaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Bakari Mbegu, Chacha Marwa, Juma Seif 'Kijiko', Godfrey Taifa, Haruna Niyonzima, Pius Kisambale, Nurdin Bakari, Hamis Kiiza.

Moro United: Lucheke Mussa, Erick Mawala, Jafari Gonga, Gidion Sepo, Tumba Swedy, Rajab Zahir, Benedict Ngassa/Jerome Lembele, Godfrey wambura, Gaudence Mwaikimba, Sultan Kasikasi.

1 comment:

  1. Yanga wacheni kukaanga Domo na badala yake mnatakiwa kucheza mpira kiwanjani na sio kwenye magazeti mnajisifu kupita kiasi.Wewe Sendeu unasikia?Kocha ameanza kukimbia waandishi wa habari sasa.

    ReplyDelete