25 August 2011

Madereva vyombo vya usafiri watakiwa kutembea na leseni

Na Grace Ndossa

JESHI la Polisi limewataka madereva wote wa vyombo vya usafiri, kutembea na leseni zao wanapoendesha vyombo hivyo ili ziweze kukaguliwa.Ukaguzi huo utafanyika
nchi nzima ambapo dereva anaposimamishwa askari wa usalama barabarani, anapaswa kuonesha leseni yake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, alisema ukaguzi huo utaanza wakati wowote.

“Mambo ambayo yataangaliwa katika ukaguzi huu ni kuhakiki leseni za madereva, uhalali wake na muda wa matumizi na bima za vyombo husika, madereva wanapaswa kutoa ushirikiano ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima kwa abilia na polisi,” alisema.

Aliongeza kuwa, madereva ambao watakuwa hawana leseni watalazimika kuacha magari yao polisi hadi watakapowasilisha leseni zao na kama atabainika dereva hajakata leseni, arafikishwa mahakamani.

Alisema dereva ambaye ataendesha gari wakati leseni yake imekwisha muda, atazuiwa kuendesha gari hilo, kufikishwa mahakamani pamoja na  mmiliki wa gari husika.

Mwisho.
9999999

3TH:
Serikali yandaa rasimu sera ya chakula bora
Na Agnes Mwaijega

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama, Bw. Meck Sadick, amesema Serikali imeandaa rasimu ya sera ili kuhakikisha taifa linatumia chakula bora na salama ambayo itasambazwa kwa wananchi wa kanda zote nchini ili kupata maoni yao.

Bw. Sadick aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya chakula yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Alisema rasimu hiyo ikijadiliwa na Watanzania wote, kupitishwa na kuwekwa katika sheria, itasaidia kupunguza magonjwa yatokanayo na ulaji wa chakula kichafu.

“Sera hii itasaidia kudhibiti milipuko ya magonwa yatokanayo na matumizi ya chakula kisicho salama kwa binadamu, Watanzania wote wana wajibu wa kutoa maoni yao juu ya rasimu hii ili ipitishwe na kuleta manufaa,” alisema.

Aliongeza kuwa, upo umuhimu mkubwa wa kuzingatia suala la upatikanaji wa chakula safi na salama ili kupunguza gharama  zinazotumika katika matibabu kutokana na ulaji wa chakula ambacho kimeandaliwa katika mazingira machafu.

“Jamii kubwa bado inaandaa chakula katika mazingira ambayo sio masafi hivyo kusababisha magonjwa mbalimbali ya mlipuko,” alisema.

Alizitaka taasisi zinahusika na masuala ya chakula kuhakikisha zinafanya ukaguzi kwa vyakula mbalimbali vinavyoingizwa nchini kabla ya kusambazwa.

“Upatikaji wa chakula bora na salama ni muhimu sana kwa sababu itawasaidia Watanzania kuishi maisha marefu,” alisema.

Mwisho.
6666666

5TH:
Washtakiwa wapewa
ruhusa na Mahakama
Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, imemruhusu mshtakiwa wa nne na sita katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 1.7, kwenda katika vituo vyao vya kazi.

Watuhumiwa hao ni Mkuu wa Idara ya Sheria na Ulinzi wa Manispaa ya Ilala, Bw. Anderson Msumba na Mkadiriaji wa Ardhi na Majengo katika manispaa hiyo, Bw. Romuald Lutinah.

Ruhusa hiyo imetolewa na Mahakama hiyo jana na Hakimu, Bi. Joyce Minde ambaye alisisitiza kuwa, amri ya kumakatwa kwa aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo Bw. Mohamed Yakub, inapaswa kutekelezwa.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuisababishia Serikali hasara kwa kubomoa nyumba za makazi eneo la Tabata Dampo, Dar es Salaam mwaka 2008, kinyume cha sheria.

Ilidaiwa kuwa, Februari 29,2008 washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama na kutenda kosa la uvunjaji wa nyumba za makazi katika kiwanja namba 52 kilichopo Barabara ya Mandela.

Katika shtaka lingine, washtakiwa hao kwa pamoja, wanadaiwa kutumia vibaya ofisi walizopewa kuzisimamia kinyume na kifungu namba 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

No comments:

Post a Comment