16 August 2011

Sare yamchefua kocha Chelsea

LONDON, England

LICHA ya baadhi ya watu kufurahishwa na pointi moja iliyopata Chelsea dhidi ya timu  ya Stoke City,katika mchezo uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Britannia, lakini
sare hiyo inaonekana kumkera kocha mpya wa timu hiyo, Andre Villas-Boas.

Gazeti la The Sun lilimnukuu, Villas-Boas, ambaye anaiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu England,  akisema kuwa, hawezi kufurahia pointi hiyo kwani alichokuwa akikitaka ni ushindi.

"Ningefurahi zaidi kama ningeshinda, siwezi kujivunia pointi hii, hali ilikuwa ni kuondoka na ushindi," alisema kocha huyo.

"Ingekuwa ushindi mkubwa hapa, hasa kutokana na matokeo ya Jumamosi ya Arsenal na Liverpool na Manchester City bado kucheza. Suala si pointi, ingawa siyo mwisho wa mechi," aliongeza.

Alisema kuwa, ingawa ni vigumu kucheza ugenini, lakini akasema kuwa, bora kuachana na hali hiyo ili kujaribu kuangalia cha kufanya wakati wa mechi  zitakazoikutanisha timu yake dhidi Norwich na West Brom.

Villas-Boas, ambaye timu yake ilizinduka kipindi cha pili, alisema matokeo hayo siyo mwanzo mzuri kwenye michuano ya hiyo ya Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment