16 August 2011

Barton akiri kumponza Gervinho

LONDON, Uingereza

JOEY Barton wa Newcastle, juzi alikiri kuwa, alijifanyisha kupigwa na kusababisha mchezaji wa Arsenal,
Gervinho kutolewa nje.Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, mchezaji
huyo alisema alikuwa amepigwa na mchezaji kutoka Ivory Coast, lakini alisukumwa na Alex Song na kusababisha kuanguka.

Barton alisema: "wakati mwingine unakuwa na hasira. Sijivunii jinsi gani nilivyofanya. Kujiangusha kirahisi. Nilikuwa nimepigwa kwa nguvu na watu wa shuleni.

"Nilijifanyisha kwa hilo, lakini fahamu kuwa, Song alinisukuma. Nilijihisi kutotendewa vyema."

Barton alimvuta, alimsimamisha Gervinho wakati mchezaji huyo mpya alipoanguka, akidai kuwa, alijifanyika ili kupata penalti dakika ya 72, katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa St James' Park na kumalizika kwa suluhu.

Aliongeza: "sikutakiwa kumnyanyua Gervinho kwa kumkunja jezi yake. Nilitakiwa kumwachia mwamuzi kushughulika na hilo.

"Kwa Song, ilikuwa ni kuhusu tabia yake."

Televisheni ilionesha kwamba, kulikuwa na hali ya kugusana kati ya Cheik Tiote, aliyemgusa Gervinho katika eneo la hatari.

Barton aliongeza: "Kulikuwa na hali ya kugusana kidogo, lakini yeye alijifanyisha zaidi.

"Nilimnyanyua na kumwambia, aache kujifanyisha, lakini alikuwa na matumaini ya kupata penalti.

No comments:

Post a Comment