30 August 2011

Poulsen ataja silaha zake

Na Zahoro Mlanzi

KOCHA Mkuu wa timu za vijana nchini, Kim Poulsen, ametangaza kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), kwa
ajili ya kujiandaa na michuano ya vijana iliyoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu kwa nchi zilizo Kusini mwa Afrika (COSAFA).

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza kikosi hicho, Poulsen alisema timu hiyo imefanya mazoezi tangu mwanzoni mwa mwezi uliopita wakibadilisha programu na timu nyingine ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Kombaini ya Copa Coca-cola).

Alisema timu hizo zilikuwa zinafanya mazoezi kila baada ya wiki moja ambapo Serengeti boys ilikuwa ikijiandaa na michuano ya Chalenji iliyotakiwa kufanyika Nairob, Kenya ambayo mpaka sasa hawana uhakika kama itakuwepo.

"Nahitaji kutengeneza timu kimbinu na vitu vingine ambapo itaanza kambi rasmi baada ya Septemba 10, mwaka huu baada ya Serengeti boys kutoka katika mashindano ya Copa coca-cola yatakayofanyika Uingereza," alisema Poulsen.

Alisema mwaliko walioupata kutoka COSOFA unaeleza kwamba mashindano hayo yatafanyikia Botswana kuanzia Desemba 10 ambapo kabla ya kwenda huko watafanya mazoezi kwa wiki mbili na baadaye watapisha mashindano ya Uhai Cup.

Aliwataja wachezaji hao ambao wamechujwa kutoka 50 mpaka kufikia 30 ni Saleh Ally (TSA), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Sugar), Yassin Mustapha (Polisi Dodoma), Andrew Kasembe (Moro United), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Ally Teru (Simba), Said Ruhava (Kagera Sugar) na Samuel Mkomola (Azam).

Wengine ni Frank Damayo (JKT Ruvu), Omega Seme (Yanga), Atupele Green (Yanga), Thomas Ulimwengu (ABC Sweden) na Jerome Lambele (Moro United),Simon Msuvan (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Alex Joseph (Majimaji), Ibrahim Rajab (Azam) na Renatus Patrick (Polisi Dodoma).

Pia wapo Abdallah Kilala (AFC), Rajab Zahir (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Alfred Amede (Russia), Khelf Hassan (Kenya), Emily Mgeta (TSC Mwanza), Ramadhan Salum (Simba), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting).

No comments:

Post a Comment